Kwa nini Mungu hubariki tu kanisa ambalo huikubali na kuitii kazi Yake? Kwa nini Yeye huyalaani mashirika ya kidini?

24/09/2018

Maneno Husika ya Mungu:

Dhihirisho la wazi zaidi wa kazi ya Roho Mtakatifu ni kwa kuyakumbatia ya sasa, sio kushikilia ya zamani. Wale ambao hawajiendelezi na kazi ya leo, na wale ambao wametengwa na utendaji wa leo, ni wale wanaopinga na hawaikubali kazi ya Roho Mtakatifu. Watu kama hao wanaipinga kazi ya Mungu ya sasa. Ijapokuwa wanashikilia nuru ya zamani, hili halimaanishi kwamba inaweza kukanwa kwamba hawajui kazi ya Roho Mtakatifu. … Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio katika dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana. Huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga, na huduma ya aina hii huenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

Wale wote ambao huweza kutii matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Kwa kuwa mwanadamu anamwamini Mungu, ni sharti afuate kwa ukaribu nyayo Zake, hatua kwa hatua; anapaswa “kumfuata Mwanakondoo popote Aendapo.” Hawa tu ndio watu wanaotafuta njia ya kweli, na wao tu ndio wanaoifahamu kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaofuata tu kanuni na mafundisho ya dini kiutumwa ni wale ambao wameondolewa na kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? … Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? Wakristo ulimwenguni kote ambao hawajazingatia kazi mpya ya sasa wote wameshikilia imani kwamba wao ni wenye bahati na kwamba Mungu atawatimizia kila mojawapo ya malengo yao. Lakini hawawezi kueleza mbona Mungu atawapeleka katika mbingu ya tatu na wala hawafahamu jinsi Yesu atakavyokuja juu ya wingu jeupe na kuwachukua, wala kusema kwa uhakika kamili kama kweli Yesu atawasili akiwa juu ya wingu jeupe siku ambayo wanaiwaza. Wote wana wasiwasi, na kukanganywa; wao wenyewe hata hawafahamu kama Mungu atachukua kila mmoja wao, watu wachache sana, wanaotoka katika madhehebu yote. Kazi ambayo Mungu anafanya kwa sasa, enzi ya sasa, mapenzi ya Mungu—ni vitu ambavyo watu hawavifahamu, na hawana cha kufanya bali kusubiri na kuhesabu siku katika vidole vyao. Ni wale tu wanaofuata nyayo za Mwanakondoo hadi mwisho kabisa ndio wanaoweza kufaidi baraka za mwisho, huku wale “watu werevu,” ambao hawawezi kumfuata hadi mwisho ilhali wanaamini wamepata yote, ndio wasiokuwa na uwezo wa kushuhudia kuonekana kwa Mungu. Wote huamini wao ndio werevu zaidi duniani, na wanasitisha maendeleo ya kazi ya Mungu bila sababu yoyote kabisa, na huonekana kuamini pasi na shaka kwamba Mungu atawachukua mbinguni, wao “wenye uaminifu wa juu zaidi kwa Mungu, humfuata Mungu, na hutii neno la Mungu”. Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao? Wengi hata wanaamini kuwa wale wanaokana sheria ya zamani na kukubali kazi mpya hawana dhamiri. Watu hawa, ambao huongea tu kuhusu “dhamiri,” na hawajui kazi ya Roho Mtakatifu, hatimaye watapata kuwa matarajio yao yamekatizwa na dhamiri yao yenyewe. Kazi ya Mungu haizingatii mafundisho, na ingawa ni kazi Yake Mwenyewe, bado Mungu haishikilii. Kile kinachopaswa kukataliwa kinakataliwa, kile kinachopaswa kuondolewa kinaondolewa. Lakini mwanadamu anajiweka kwenye uadui wa Mungu kwa kushikilia sehemu moja ndogo ya kazi ya usimamizi wa Mungu. Si huu ndio upuuzi wa mwanadamu? Si huu ndio ujinga wa mwanadamu? Kadri watu wanakuwa waoga na wenye tahadhari sana kwa sababu wanachelea kutopata baraka za Mungu, ndivyo wanavyopungukiwa zaidi na uwezo wa kupata baraka zaidi, na wa kupata ile baraka ya mwisho. Watu wale wanaoshikilia kiutumwa sheria huwa wanadhihirisha uaminifu wa hali ya juu kwa sheria, na kadri wanavyodhihirisha uaminifu jinsi hiyo kwa sheria, ndivyo wanavyokuwa waasi wanaompinga Mungu. Kwa kuwa sasa ni Enzi ya Ufalme na wala si Enzi ya Sheria, na kazi ya leo haiwezi kulinganishwa na kazi ya zamani wala kazi ya zamani haiwezi kulinganishwa na kazi ya sasa. Kazi ya Mungu imebadilika, na vitendo vya mwanadamu pia vimebadilika; si kushikilia sheria au kuubeba msalaba. Basi, uaminifu wa watu kwa sheria na msalaba hautapata kibali cha Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[1] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba si chochote zaidi ya nzi katika kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kutegemea nguruwe na mbwa wa wazazi wao. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno.[2] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu anajua kidogo kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujazwa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza kazi yao tena ya utesaji, wakiendeleza kazi yao yenye umri wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)

Watu hawa ambao wanamwamini Mungu wa kweli kwa maneno tu lakini ambao Mungu anawaamini wao kuwa sehemu ya kikundi cha dini—wanaitembea njia gani? Je, inaweza kusemekana kwamba watu hawa wanaitembea njia ya kupeperusha bendera ya imani bila kamwe kufuata njia Yake au kumwabudu, na badala yake kumtelekeza Mungu? Yaani, wanaitembea njia ya kumwamini Mungu lakini wanamwabudu Shetani, wakitekeleza usimamizi wao wenyewe, na kujaribu kuanzisha ufalme wao wenyewe—je, hiki ni kiini cha hilo? Je, watu kama hawa wana uhusiano wowote na mpango wa Mungu wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu? (La.) Bila kujali ni watu wangapi wanamwamini Mungu, mara tu imani zao zinapofafanuliwa na Mungu kama dini au kikundi, basi Mungu ameamua kuwa hawawezi kuokolewa. Kwa nini nasema hivi? Katika kundi au umati wa watu ambao hawana kazi na mwongozo wa Mungu na ambao hawamwabudu hata kidogo, wanamwabudu nani? Wanamfuata nani? Katika mioyo yao wanamtambua Mungu, lakini kwa kweli, wao huathiriwa na utawala wa hila na udhibiti wa binadamu. Kwa jina, labda wanamfuata mtu fulani, lakini kimsingi, wanamfuata Shetani, ibilisi; wanafuata nguvu ambazo zina uhasama kwa Mungu, ambazo ni maadui wa Mungu. Je, Mungu anaweza kuokoa kundi kama hili la watu? Je, wana uwezo wa kutubu? Wao hupeperusha bendera ya imani, wakitekeleza shughuli za binadamu, wakitekeleza usimamizi wao wenyewe, na wanakwenda kinyume na mpango wa Mungu wa usimamizi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Matokeo yao ya mwisho ni kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; Mungu hawezi kamwe kuwaokoa watu hawa, hawawezi kamwe kutubu, tayari wamekamatwa na Shetani—wamo mikononi mwa Shetani kabisa.

Umetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Tanbihi:

1. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

2. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp