Mungu hutegemeza nini uamuzi Wake wa mwisho wa mtu?

13/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, bali si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya lingine, njia ambayo kwayo wameitumia kunifuata, sifa zao asilia, na hatimaye jinsi ambavyo wamejistahi. Kwa njia hii, haijalishi ni mtu wa aina gani, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu, na wote watakuwa pamoja na wa aina yake kama Nilivyopanga. Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili. Sharti mtambue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa pia. Huu ni ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Kabla ya binadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu ni wa mwanadamu kumwamini, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa wanaoamini isiyo yakini bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati ya hawa wafuasi wote, kuna wale wanaohudumu kama makuhani, wale wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Nawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa

Mungu hutumia majaribio kuanzisha matokeo ya binadamu. Kunavyo viwango viwili vya kutumia katika majaribio yanayoasisi matokeo ya binadamu: Kiwango cha kwanza ni idadi ya majaribio ambayo watu hao wanapitia, na kiwango cha pili ni matokeo ya watu hawa katika majaribu haya. Ni viashirio hivi viwili vinavyoasisi matokeo ya binadamu. Sasa tutaweza kufafanua viwango hivi viwili.

…………

… Kama utakuwa hujakomaa, Mungu atakupa kiwango kidogo sana; wakati kimo chako kitakapokuwa kikubwa kidogo, Mungu atakupa kiwango cha juu zaidi kidogo. Lakini Mungu atakuwa vipi baada ya wewe kuuelewa ukweli wote? Mungu atahakikisha kuwa unakabiliana na hata majaribio makubwa zaidi. Katikati ya majaribio haya, kile Mungu anachotaka kupata, kile Mungu anachotaka kuona, ni maarifa yako ya kina zaidi ya Mungu na kumcha kwako Kwake kwa njia ya kweli. Wakati huu, mahitaji ya Mungu kwako wewe yatakuwa ya juu zaidi “makali zaidi” kuliko wakati ambapo kimo chako kilikuwa kidogo zaidi (kidokezo: Watu huona kwamba hali hii ni kali, lakini Mungu kwa hakika Huiona kuwa ya kustahimilika). Wakati Mungu anawapa watu majaribio, ni uhalisia gani ambao Mungu anataka kuunda? Mungu anauliza kila mara kwamba watu wampe Yeye moyo wao. … Wakati Mungu anapokupa jaribio, Mungu hutaka kujua kama moyo wako uko pamoja Naye, pamoja na mwili au pamoja na Shetani. Wakati Mungu anapokupa jaribio, Mungu anataka kujua kama unasimama katika upinzani na Yeye au kama unasimama katika hali ambayo inalingana na Yeye, na kutaka kuona moyo wako kama uko na Yeye. Wakati hujakomaa na wakati wa kukabiliwa na majaribio, kiwango cha imani yako kiko chini, na huwezi kujua hasa ni nini unachohitaji ili kutosheleza nia za Mungu kwa sababu unao uelewa finyu wa ukweli. Licha ya haya yote, bado unaweza kumwomba Mungu kwa dhati na uaminifu, kuwa radhi kuutoa moyo wako kwa Mungu, kumfanya Mungu kuwa mkuu wako, na kuwa radhi kumpa Mungu yale mambo unayosadiki kuwa yenye thamani zaidi. Hii ndiyo maana ya wewe kuwa tayari umempa Mungu moyo wako. Unaposikiliza mahubiri mengi zaidi na zaidi, na kuelewa ukweli zaidi na zaidi kimo chako kitaanza kukomaa kwa utaratibu. Kiwango ambacho Mungu huhitaji kutoka kwako si sawa na kile ambacho ulikuwemo wakati ulikuwa hujakomaa; Anahitaji kiwango cha juu zaidi kuliko hicho. Wakati moyo wa binadamu unapewa Mungu kwa utaratibu, unaanza kuwa karibu zaidi na karibu zaidi na Mungu; wakati binadamu anaweza kuwa karibu na Mungu kweli, wanaanza kuwa na moyo ambao sanasana unamcha Yeye. Mungu anataka aina hii ya moyo.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Kunao msemo ambao mnafaa kutilia maanani. Ninasadiki msemo huu ni muhimu sana, kwa sababu kwangu Mimi unakuja akilini mara nyingi kila siku. Kwa nini hivyo? Kwa sababu kila wakati Ninapokumbana na mtu, kila wakati Ninaposikia hadithi ya mtu, kila wakati Ninaposikia kile alichopitia mtu au ushuhuda wake wa kusadiki Mungu, siku zote Ninatumia msemo huu kuweza kupima kama mtu huyu binafsi ni mtu wa aina ambayo Mungu anataka au la, mtu wa aina ambayo Mungu anapenda. Hivyo msemo huu ni upi, basi? … Msemo ni “tembea katika njia ya Mungu: mche Mungu na kuepuka maovu.” Je, huoni kwamba kauli hii ni rahisi kupindukia? Ilhali ingawa msemo huu unaweza kuwa rahisi, mtu ambaye anao uelewa wa ndani na wa kweli wa msemo huu atahisi kwamba ni wenye uzito mkubwa; kwamba unao thamani nyingi ya kutenda; kwamba ni lugha ya uzima iliyo na uhalisia wa ukweli; ambayo ni lengo la maishani katika kulenga wale wanaotafuta kutosheleza Mungu; na hiyo ni njia ya maisha marefu itakayofuatwa na mtu yeyote anayejali nia za Mungu. … Lakini kwa nini Nikauzungumzia msemo huu? Licha ya mtazamo wenu, au kile mtakachofikiria, lazima Nizungumzie msemo huu kwa sababu unafaa ajabu namna ambavyo Mungu huasisi matokeo ya binadamu. Bila kujali kama uelewa wenu wa sasa wa msemo huu upo, namna mnavyouchukulia, bado Nitawaeleza: kama watu wanaweza kuyaweka maneno ya msemo huu katika vitendo na kuyapitia, na kutimiza kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi atahakikishiwa kuishi kisha atahakikishiwa kuwa mtu mwenye matokeo mazuri. Kama huwezi kutimiza kiwango kilichowekwa wazi katika msemo huu, basi inaweza kusemekana kwamba matokeo yako hayajulikani. Hivyo basi Ninaongea kwenu kuhusu msemo huu kwa matayarisho yenu ya kiakili, na ili mjue ni kiwango aina gani ambacho Mungu anatumia kuwapima.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakuna kosa lolote litakalotokea, na hakutakuwa na kosa hata moja litakalofanywa. Ni pale tu ambapo watu wanafanya kazi ndipo hisia za binadamu ama maana itaingilia. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp