Mungu huwaokoa watu gani? Yeye huwaondosha watu gani?
Maneno Husika ya Mungu:
Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuwa hai tena, ambao wanaweza kuuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa watii kwa Mungu, na wapo tayari kumtafuta Mungu. Anawaokoa wanaomwamini Mungu aliyepata mwili, na wanaamini katika kuonekana Kwake. Baadhi ya watu wanaweza kuwa hai tena, na baadhi hawawezi; inategemea na asili yao kama inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia sana kuhusu maneno ya Mungu lakini bado hawaelewi mapenzi ya Mungu, wameyasikia maneno mengi sana ya Mungu lakini bado hawawezi kuyaweka katika vitendo, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia kwa kukusudia kabisa wanaingilia kazi ya Mungu. Hawawezi kufanya kazi yoyote kwa ajili ya Mungu, hawawezi kujitolea chochote Kwake, na pia wanatumia kwa siri pesa za kanisa, na kula katika nyumba ya Mungu bure. Watu hawa ni wafu, na hawataokolewa. Mungu anawaokoa wale ambao wapo katika kazi Yake. Lakini kuna sehemu ya watu hao ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni idadi ndogo tu ndiyo inaweza kupokea wokovu Wake. Hii ni kwa sababu watu wengi wamepotoshwa kwa kina sana na wakuwa wafu, na wamepita kiwango cha kuokolewa; wametumiwa vibaya kabisa na Shetani, na ni wenye hila sana katika asili yao. Watu hao wachache pia hawawezi kumtii Mungu kikamilifu. Hawakuwa wale ambao walikuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au wale ambao walikuwa na upendo wa hali ya juu kabisa kwa Mungu toka mwanzo; badala yake, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo wake mkuu, kuna mabadiliko katika tabia zao kwa sababu ya tabia ya Mungu ya haki, na wanamjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, ambayo ni halisi na ya kawaida.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?
Mungu siku zote amewakamilisha wote wanaomhudumia. Hawatupilii mbali kwa urahisi tu. Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku
Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walio tayari kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walio radhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walio radhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni waakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasiotenda ukweli hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa makusudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasiotenda ukweli hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtu kufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasiotenda ukweli lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli
Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu
Watu wengine huacha kazi zao wakati kitu kibaya kinawafikia, na wanashindwa kusimama kwa miguu yao baada ya kila pingamizi. Watu hawa wote ni wapumbavu ambao hawapendi ukweli, na hawatapata faida i hata wakiishi maisha yao yote kwa imani. Watu wapumbavu kama hao watawezaje kufuata hadi mwisho? Iwapo jambo kama hili litatokea mara kumi lakini usipate chochote kutoka kwalo, basi wewe ni mtu duni na asiye na maana. Watu werevu na wale ambao wana ubora wa ndani wa kweli amabao wanaelewa masuala ya kiroho ni watafutaji wa ukweli; jambo likiwafanyikia mara kumi, basi mara nane kwa kumi pengine wataweza kupata ufunuo kiasi, kupata funzo fulani, kfikia nuru na kufanya maendeleo. Mambo yanapomfanyikia mpumbavu mara kumi—yule asiyeelewa masuala ya kiroho—haitamfaidi maishani hata mara moja, haitawabadilisha hata mara moja, na haitawasababisha waelewe asili yao hata mara moja, na huu ndio mwisho wao. Kila wakati kitu kinapowafanyikia, wanaanguka chini, na kila wakati wanapoanguka chini, wanahitaji mtu mwingine kuwasaidia kusimama tena, kuwabembeleza; bila kusaidiwa na kubembelezwa, hawataweza kuinuka. Iwapo, kila wakati ambapo kitu kinafanyika, wamo kwenye hatari ya kuanguka, na kila wakati wamokwenye hatari ya yeye kudhalilika, je, huu sio mwisho kwao? Je, bado kuna sababu zinginezo kwa watu kama hawa wasio na maana kuokolewa? Wokovu wa Mungu wa binadamu ni wokovu wa wale wanaopenda ukweli, wokovu wa sehemu ndani yao ambayo ina ari ya mapenzi na maazimio na sehemu yao inayotamani ukweli na haki mioyoni mwao. Azimio la mtu ni sehemu yao ndani ya mioyo yao inayotamani haki, wema na ukweli, na iliyo na dhamiri. Mungu hukoa sehemu hii ya watu, na kupitia hiyo Anabadili tabia yao potovu, ili waweze kuelewa na kupata ukweli, ili upotovu wao uweze kutakaswa na tabia ya maisha yao ikaweze kubadilishwa. Ikiwa kamwe huna vitu hivi ndani yako, basi huwezi kuokolewa. Ikiwa ndani yako hakuna upendo wa ukweli ama hamu ya haki na mwanga wakati wowote unapokumbana na uovu, hutakuwa na hiari ya kutupa mbali vitu viovu ama azimio la kupitia shida, au azimio la kuvumilia mateso, iwapo dhamiri yako ni yenye ganzi, iwapo welekevu wako wa kupokea ukweli pia ni wenye kuwa ba ganzi na, huna umakini kwa ukweli na masuala amabayo hutokea, na iwapo una dhamira katika mambo yote, na, huwezi kushughulika au kutatua mambo wewe mwenyewe, basi hakuna njia ya kuokolewa. Mtu wakama huyu hana chochote cha kumpendekeza, hana chochote cha thamani cha kufanya kazi Dhamiri yao imekufa ganzi, akili yake imevurugwa, na hawapendi ukweli wala kutamani haki katika kina cha mioyo yao, na haijalishi jinsi Mungu Anavyonena kwa wazi ama kwa dhahiri kuhusiana n ukweli, wao hawajibu, kana kwamba walikufa tayari. Je, mambo kwao hayajafika mwisho? Mtu aliye na pumzi bakshishi ndani mwao anaweza kuokolewa kwa upumuaji bandia,lakini iwapoi kama wamekufa tayari na roho yao imeondoka, basi upumuaji bandia hautafanya lolote. Iwapo, kila mara unapokabiliwa na jambo unajikunja kutokana na hilo na kujaribu kuliepuka, hii inamaanisha bado hujashuhudia; hivyo basi huwezi kuokolewa na hakika umefika mwisho.
Kimetoholewa kutoka katika “Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo
Wanadamu kama hawa hawaelewi kazi mpya lakini wamejawa na fikira zisizokoma. Hawafanyi chochote kanisani; badala yake, wanachochea na kusambaza uhasi kila pahali, hata kushiriki katika kila namna ya utovu wa nidhamu na vurugu kanisani, na hivyo kuwarusha wale wasiobagua katika vurugu na machafuko. Haya ibilisi wanaoishi, hawa mapepo mabaya wanapaswa kuondoka kanisani haraka iwezekanavyo, kanisa lisije likaharibiwa kwa sababu yako. Labda huogopi kazi ya leo, lakini huogopi adhabu ya haki ya kesho? Kuna idadi kubwa ya watu kanisani ambao ni vimelea, na pia kuna idadi kubwa ya mbwa mwitu wanaotafuta kuvuruga kazi ya kawaida ya Mungu. Vitu hivi vyote ni mapepo yaliyotumwa na Ibilisi, ni mbwa mwitu wakali wanaotafuta kuwala kondoo wasiojua. Iwapo wanadamu kama hawa hawatafukuzwa, basi wanakuwa vimelea kwa kanisa na nondo wanaokula sadaka. Hawa mabuu wenye kudharauliwa wajinga, duni, na wenye kuchukiza wataadhibiwa siku moja karibuni!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu
Wale wanaofikiria tu miili yao na wanaofurahia faraja, wale wanaoonekana kuamini lakini wasioamini kwa kweli; wale wanaojihusisha katika uganga na uchawi; wale ambao ni wazinzi, walio duni kabisa; wale wanaoiba sadaka za Yehova na mali Yake; wale wanaopenda hongo; wale walio na njozi za kupaa mbinguni; wale ambao ni wenye majivuno na fidhuli, wanaojitahidi tu kwa sababu ya umaarufu na utajiri wa kibinafsi; wale wanaoeneza maneno ya safihi; wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe; wale wanaotoa tu hukumu dhidi ya Mungu Mwenyewe na kumkashifu; wale wanaounda vikundi na kutafuta kujitegemea; wale wanaojitukuza juu ya Mungu, wale wanaume na wanawake wadogo, wa makamo na wakubwa ambao ni wapuuzi na wametegwa katika uasherati; wale wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu na utajiri wa kibinafsi na wanafuatilia hadhi ya kibinafsi miongoni mwa mengine; wale watu wasiotubu walionaswa katika dhambi—je, si wote hawawezi kuokolewa? Uasherati, kutenda dhambi, uganga, uchawi, matusi na maneno ya safihi yote yamejaa kwenu; na ukweli na maneno ya uzima yanakanyagwa miongoni mwenu, na lugha takatifu inachafuliwa miongoni mwenu. Ninyi Mataifa, mliojaa uchafu na uasi! Matokeo yenu ya mwisho yatakuwa yapi? Je, wale wanaopenda mwili, wanaotenda uchawi wa mwili, na waliotegwa katika dhambi ya uasherati wanawezaje kuwa na ujasiri wa kuendelea kuishi! Je, hujui kwamba watu kama ninyi ni mabuu wasioweza kuokolewa? Ni nini kinachowapa haki ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo katika wale wasiopenda ukweli na wanapenda tu mwili—watu kama hawa wanawezaje kuokolewa? Wale wasiopenda njia ya uzima, wasiomtukuza Mungu ama kumshuhudia, wanaopanga njama kwa ajili ya hadhi yao wenyewe, wanaojisifu sana—je, si bado wao wako vivyo hivyo, hadi leo? Kuna thamani gani katika kuwaokoa? Iwapo unaweza kuokolewa hakutegemei ukubwa wako ama ni miaka mingapi umekuwa ukifanya kazi, sembuse sifa ambazo umeongeza. Badala yake, kunategemea iwapo ufuatiliaji wako umezaa matunda. Unapaswa kujua kwamba wale waliookolewa ni “miti” inayozaa matunda, siyo miti iliyo na majani yaliyositawi sana na maua mengi lakini ambayo hayazai matunda. Hata kama umeshinda miaka mingi ukizurura mitaani, hilo lina maana gani? Ushuhuda wako uko wapi? Uchaji wako wa Mungu ni kidogo sana kuliko upendo wako kwako mwenyewe na hamu zako zenye tamaa—je, si mtu kama huyu ni mpotovu? Anawezaje kuwa kielelezo na mfano wa wokovu? Asili yako ni isiyorekebishika, wewe ni mwasi sana, huwezi kuokolewa! Je, si watu kama hawa ni wale watakaoondolewa? Je, si wakati ambapo kazi Yangu inakamilika ni wakati wa kufika kwa siku yako ya mwisho? Nimefanya kazi nyingi sana na kuzungumza maneno mengi sana miongoni mwenu—kweli mmeyasikiliza kiasi kipi? Mmewahi kutii kiasi kipi? Kazi Yangu ikamilikapo, huo utakuwa wakati ambapo unakoma kunipinga, wakati ambapo unakoma kusimama dhidi Yangu. Nifanyapo kazi, mnanipinga bila kukoma; kamwe hamyatii maneno Yangu. Nafanya kazi Yangu na wewe unafanya “kazi” yako mwenyewe, ukitengeneza ufalme wako mdogo. Ninyi ni kundi la mbweha na mbwa tu, mnaofanya kila kitu kunipinga! Mnajaribu kila wakati kuwakumbatia wale wanaowapa upendo wao wa dhati—uchaji wenu uko wapi? Kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu! Hamna utii wala uchaji, na kila kitu mfanyacho ni kidanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hawa wanaweza kuokolewa? Wanadamu ambao ni waasherati na wakware daima hutaka kuwavutia makahaba wenye ubembe kwao kwa ajili ya raha zao wenyewe. Sitawaokoa mashetani wa kisherati kama hawa hata kidogo. Nawachukia ninyi mashetani wachafu, na ukware na ubembe wenu utawatumbukiza kuzimuni. Mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi mashetani wachafu na pepo waovu ni wa kutia kinyaa! Mnachukiza! Watu ovyo kama ninyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi wanaweza kuokolewa bado? Leo, ukweli huu, njia hii, na uzima huu hauwavutii; badala yake mnavutiwa na utendaji dhambi, fedha, hadhi, umaarufu na faida; mnavutiwa na raha za mwili; sura nzuri za wanaume na uzuri wa wanawake. Ni nini kinachowastahiki kuingia katika ufalme Wangu? Sura yenu hata ni ya juu zaidi kuliko ya Mungu, hadhi yenu hata ni ya juu kuliko ya Mungu sembuse fahari yenu kubwa miongoni mwa wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hujageuka kuwa malaika mkuu? Wakati matokeo ya watu yanafichuliwa, ambao pia ndio wakati kazi ya wokovu itakaribia kuisha, wengi kati yenu mtakuwa maiti msioweza kuokolewa na lazima muondolewe.
Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa kufanya huduma ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya maangamizi. Kama mtu anaweza kweli kufanya jukumu lake, basi inamaanisha kwamba ni mwaminifu milele kwa Mungu na hatafuti tuzo, bila kujali iwapo anapokea baraka ama bahati mbaya. Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu lao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?