Tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu

22/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto” (Mathayo 3:11).

Maneno Husika ya Mungu:

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. …

… Mungu Mwenyewe hana mambo ya kuasi; dutu Yake ni nzuri. Yeye ni udhihirisho wa uzuri wote na wema, vile vile upendo wote. Hata katika mwili, Mungu hafanyi lolote linalomuasi Mungu Baba. Hata kwa gharama ya kutoa sadaka maisha Yake, Angekuwa kwa ukamilifu tayari na kutofanya uchaguzi mwingine. Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelaghaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni

Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mkubwa, Yeye ni mwenyezi, mtakatifu, na mwenye haki—na vilevile ndivyo ambavyo mwili Wake ulivyo pia mkubwa, wenye uwezo, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni chenye haki na manufaa kwa mwanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, chenye utukufu, na uweza, na hakiwezi kukifanya chochote ambacho kinakiuka ukweli au uadilifu na haki, isitoshe hata kile ambacho kinaasi dhidi ya Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na hivyo basi mwili Wake hauwezi kuharibiwa na Shetani; mwili Wake una kiini tofauti na ule mwili wa mwanadamu. Kwani ni mwanadamu, wala si Mungu, ambaye anaharibiwa na Shetani, na mwili wa Mungu usingeweza kuharibiwa na Shetani. Kwa hivyo, licha ya ukweli kwamba mwanadamu na Kristo wanakaa mahala pamoja, ni mwanadamu tu ndiye ambaye anatawaliwa, anatumiwa, na kutegwa na Shetani. Kinyume cha hayo, Kristo daima hapenyezwi na uovu wa Shetani, kwa kuwa Shetani hataweza kamwe kupaa hadi mahala pa aliye juu zaidi, na hataweza kumkaribia Mungu. Leo, nyote mnapaswa kuelewa kuwa ni mwanadamu tu, aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ananisaliti, na kwamba daima tatizo hili halitakuwa linamhusu Kristo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Mungu mwenye mwili ana tofauti kubwa na wanadamu wanaotumiwa na Mungu. Mungu mwenye mwili Anaweza kufanya kazi ya uungu, lakini wanadamu wanaotumiwa na Mungu hawawezi. Mwanzoni mwa kila enzi, Roho wa Mungu huongea binafsi kuzindua enzi mpya na kuleta mwanadamu kwenye mwanzo mpya. Wakati Yeye Amemaliza kuongea, hili linaashiria kwamba kazi ya Mungu katika uungu Wake imekamilika. Baada ya hapo, wanadamu wote hufuata mwongozo wa wale ambao wametumiwa na Mungu kuingia katika uzoefu wa maisha.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Japo Mungu mwenye mwili Ana akili ya mwanadamu wa kawaida, kazi Yake haijatiwa doa na mawazo ya binadamu; Anafanya kazi katika ubinadamu na akili ya kawaida chini ya masharti ya awali kuwa atakuwa na ubinadamu na akili ya kawaida, na si na mawazo ya kawaida ya binadamu. Haijalishi mawazo ya mwili Wake ni bora kiasi gani, kazi Yake haionyeshi alama ya mantiki au kufikiria. Kwa maneno mengine, kazi Yake haiwazwi na akili ya mwili Wake, ila ni onyesho la moja kwa moja la kazi ya uungu katika ubinadamu Wake. Kazi Yake yote ni huduma Anayostahili kutimiza, na haiwazwi hata chembe kwa akili Zake. Kwa mfano, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kusulubishwa hayakuwa mazao ya akili Zake za binadamu, yasingeweza kutimizwa na mwanadamu yeyote mwenye akili za binadamu. Vivyo hivyo, kazi ya ushindi ya leo ni huduma ambayo ni sharti itekelezwe na Mungu mwenye mwili, lakini si kazi ya mapenzi ya mwanadamu, ni kazi ambayo uungu Wake unapaswa kufanya, kazi ambayo hakuna mwanadamu wa mwili anaiweza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Katika enzi zote, wanadamu ambao Mungu Ametumia wote wana uwezo wa mawazo na mantiki ya kawaida. Wao wote wanajua kanuni za mienendo ya binadamu. Wana mawazo ya kawaida ya binadamu, na wamejiandaa na vitu vyote ambavyo wanadamu wa kawaida wanapaswa kuwa navyo. Wengi wao wana vipaji vya pekee na werevu wa kiasili. Katika kuwafinyanga watu hawa, Roho wa Mungu Anatumia vipaji vyao, ambavyo ni zawadi zao Alizowapa Mungu. Roho wa Mungu Anayeleta vipaji vyao katika kazi, Akitumia uwezo wao kumhudumia Mungu. Hata hivyo, kiini cha Mungu hakina itikadi na hakina fikira. Hakiungani na mawazo ya binadamu na hata kinakosa vitu ambavyo binadamu wa kawaida huwa navyo. Yaani, Mungu hata hafahamu vizuri kanuni za maadili ya binadamu. Hivi ndivyo ilivyo Mungu wa leo Anapokuja duniani. Kazi Yake na maneno Yake hayajachafuliwa na nia au fikira za binadamu, bali ni dhihirisho la moja kwa moja la nia za Roho, na Anafanya kazi moja kwa moja kwa niaba ya Mungu. Hii ina maana kuwa Roho hunena moja kwa moja, yaani, uungu hufanya kazi moja kwa moja, bila kuchanganya ndani hata nia kidogo za mwanadamu. Yaani, Mungu katika mwili Anajumuisha uungu moja kwa moja, Hana mawazo ya binadamu au itikadi, na Haelewi kanuni za maadili ya binadamu. Kama kungekuwa na kazi ya uungu tu (kumaanisha iwapo ingekuwa Mungu mwenyewe pekee ndiye Anayefanya kazi hiyo), kazi ya Mungu haingeweza kufanyika duniani. Kwa hivyo Mungu Anapokuja duniani, lazima Awe na wanadamu wachache Anaowatumia kufanya kazi katika ubinadamu pamoja na kazi ambayo Mungu hufanya katika uungu. Kwa maneno mengine, Yeye Anatumia kazi ya mwanadamu ili kusaidia kazi Yake takatifu. La sivyo, mwanadamu hangeweza kuja katika mawasiliano ya moja kwa moja na kazi ya uungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Kazi ya Mungu Mwenyewe ni kazi ya Roho Mtakatifu; kazi za Mungu mwenye mwili hazitofautiani na kazi za Roho Mtakatifu. Kazi ya wanadamu wanaotumiwa pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwamba tu kazi ya Mungu ni onyesho kamili la Roho Mtakatifu, na hakuna tofauti, ilhali kazi ya wanadamu wanaotumiwa inachanganyika na mambo mengi ya kibinadamu, na wala sio uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu, wala uonyeshaji kamili. … Roho Mtakatifu anapofanya kazi kwa wanadamu wanaotumiwa, karama zao na tabia zao halisi zinatumiwa pia na wala haziachwi. Tabia zao halisi zinatumiwa zote kwa ajili ya kutoa huduma kwa kazi. Tunaweza kusema kuwa Anafanya kazi kwa kutumia sehemu zilizopo za wanadamu ili kupata matokeo yatendayo kazi. Kinyume chake, kazi inayofanyika katika mwili uliopatikana ni yenye kumwonyesha Roho moja kwa moja na wala haichanganywi na akili na mawazo ya mwanadamu, haifikiwi na karama za mwanadamu, uzoefu wa mwanadamu au hali ya ndani ya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Usemi Wangu unawakilisha asili Yangu, lakini kile Ninachokisema kiko nje ya uwezo wa mwanadamu. Kile Nikisemacho sio kile ambacho mwanadamu anakipitia, na sio kitu ambacho mwanadamu anaweza kukiona, pia si kitu ambacho mwanadamu anaweza kukigusa, lakini ndicho Nilicho. Baadhi ya watu wanakiri tu kwamba kile Ninachokifanyia ushirika ndicho kile Nimekipitia, lakini hawatambui kwamba ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Ni kweli, kile Ninachokisema ndicho kile Nimekipitia. Ni Mimi Ndiye Niliyefanya kazi ya usimamizi kwa kipindi cha zaidi ya miaka elfu sita. Nimepitia kila kitu kuanzia mwanzo wa uumbaji wa mwanadamu hadi leo; Nitashindwaje kukizungumzia? Linapokuja suala la asili ya mwanadamu, Nimeliona waziwazi, na Nimeliangalia toka zamani; sasa Nitashindwaje kuliongelea? Kwa kuwa nimeiona asili ya mwanadamu kwa uwazi, Nina sifa za kumrudi mwanadamu na kumhukumu, kwa sababu mwanadamu mzima ametoka Kwangu lakini ameharibiwa na Shetani. Kwa ukweli, Nimehitimu kutathmini kazi ambayo Nimeifanya. Ingawa kazi hii haijafanywa na mwili Wangu, ni uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho, na hiki ndicho Nilicho nacho na kile Nilicho. Kwa hivyo, Ninaweza kuonyesha na kufanya kazi ambayo Napaswa kufanya. Kile ambacho mwanadamu anakisema ni kile alichokipitia. Ni kile ambacho wamekiona, kile ambacho akili zao zinaweza kukifikia, na kile ambacho milango yao ya fahamu inaweza kuhisi. Hicho ndicho wanachoweza kukifanyia ushirika. Maneno yaliyosemwa na mwili wa Mungu ni onyesho la moja kwa moja la Roho na huonyesha kazi ambayo imefanywa na Roho. Mwili haujaipitia au kuiona, lakini bado huonyesha asili Yake kwa sababu kiini cha mwili ni Roho, na huonyesha kazi ya Roho. Ingawa mwili hauwezi kuifikia, ni kazi ambayo tayari imefanywa na Roho. Baada ya kufanyika mwili, kupitia uonyeshaji wa mwili, Anawasaidia watu kujua asili ya Mungu na kuwafanya watu kuiona tabia ya Mungu na kazi ambayo Ameifanya. Kazi ya mwanadamu inawawezesha watu kuelewa kwa uwazi kuhusu kile wanachopaswa kuingia kwacho na wanachopaswa kukielewa; inahusisha kuwaongoza watu kupata ufahamu na kuujua ukweli. Kazi ya mwanadamu ni kuwaendeleza watu; kazi ya Mungu ni kufungua njia mpya na kufungua enzi mpya kwa ajili ya binadamu, na kuwafunulia watu kile ambacho hakijafahamika kwa watu wenye mwili wa kufa, ikiwasaidia kuelewa tabia Yake. Kazi ya Mungu ni kuwaongoza wanadamu wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Mwanadamu anayetumiwa na Mungu siye Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili siye mwanadamu anayetumiwa na Mungu; katika hili, kunayo tofauti kubwa sana. … Maneno ya Mungu mwenye mwili yanaanzisha enzi mpya, yanaongoza wanadamu wote, yanafichua mafumbo, na kumwonyesha mwanadamu mwelekeo mbele katika enzi mpya. Nuru anayoipata mwanadamu ni utendaji au elimu rahisi. Haiwezi kuelekeza binadamu wote kuingia enzi mpya au kufichua fumbo la Mungu Mwenyewe. Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu yuko na dutu ya Mungu, na mwanadamu yuko na dutu ya mwanadamu. Iwapo mwanadamu anachukulia maneno yanayonenwa na Mungu kama kupewa nuru tu na Roho Mtakatifu, na kuchukua maneno yaliyonenwa na mitume na manabii kama maneno yaliyonenwa na Mungu Mwenyewe, basi mwanadamu anakosea.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp