Mafarisayo Kukemewa na Bwana Yesu
10. Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu
Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.
11. Mafarisayo Kukemewa na Yesu
Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.
Mat 23:13-15 Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.
Kunazo dondoo mbili tofauti hapo juu—hebu kwanza tuangalie dondoo ya kwanza: Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu.
Katika Biblia, tathmini ya Mafarisayo kwa Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “walisema, Yeye si wa akili sawa. … Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Mafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa ikiiga mambo au ikifikiria tu kutoka popote—ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho yao ilitolewa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele ya watu ni kana kwamba ilikuwa imeshughulikiwa vyema, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kuvumilia. Nguvu zao mchafukoge za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua maono yao binafsi yasiyo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na maumbile yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na maono yao yasiyo na misingi, ya wivu, na hali ya ubovu na ubaya na ukatili wao dhidi ya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, walimshambulia bila mpango, bila subira, kwa njia za kishenzi, na kwa makusudi ya kijicho pamoja na kutupilia mbali kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilikuwa hadi kufikia kiwango cha kutupilia mbali Roho Wake bila kubagua, Yaani, Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu. Hivi ndivyo waliyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli,” na “mkuu wa pepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa pepo. Waliweza kupatia sifa ya kazi ambayo Roho wa Mungu mwenye mwili alikuwa amevalia kama kurukwa akili. Hawakukufuru tu Roho wa Mungu kama Beelzebuli na mkuu wa pepo, lakini waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upingaji wao na kukufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kutumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na watumishi wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na mapambano yao na Mungu yasiyoisha. Kiini cha upingaji wao kwa Mungu na mwelekeo wao wa ukatili kwake Yeye, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa ya na yale waliyoyasema na kufanya, na akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusameheka ulimwenguni humu na hata ulimwengu unaokuja, kama vile tu maandiko yafuatayo yanasema: “Wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” na “Yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Leo, hebu tuzungumzie maana halisi ya maneno haya kutoka kwa Mungu “hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Hii ni, acha tuweke wazi namna ambavyo Mungu hukamilisha matamshi yake: “haitasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.”
Kila kitu ambacho tumezungumzia kuhusu yote haya kinahusiana na tabia ya Mungu, na mweleko Wake kwa watu, masuala na mambo, na mambo. Kikawaida, dondoo hizo mbili hapo juu haziwezi kuachwa. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi mbili za maandiko? Baadhi ya watu husema wanaiona ghadhabu ya Mungu. Baadhi ya watu husema wanauona upande wa tabia ya Mungu ambao hauvumilii kosa la wanadamu, na kwamba watu wakifanya kitu ambacho kinamkufuru Mungu, hawatapata msamaha Wake. Licha ya ukweli kwamba watu wanaona na kutambua ghadhabu na kutovumilia makosa ya wanadamu kwa Mungu katika vifungu hivi viwili, bado hawaelewi kwa kweli mtazamo Wake. Dondoo hizi mbili zinao ufafanuzi wa mwelekeo na mtazamo wa kweli wa Mungu kwa wale wanaomkufuru na kumghadhabisha Yeye. Dondoo hii katika maandiko inashikilia maana halisi ya mwelekeo na mtazamo Wake: “Yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Watu wanapomkufuru Mungu, wakati wanapomghadhabisha Yeye, Yeye hutoa hukumu, na hukumu hii ndiyo matokeo yaliyotolewa na Yeye. Hali hii inafafanuliwa hivi katika Biblia: “Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” (Mat 12:31), na “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki!” (Mat 23:13). Hata hivyo, imerekodiwa katika Biblia matokeo yapi yalikuwepo kwa wale waandishi na Mafarisayo, pamoja na wale watu waliosema Alikuwa amerukwa na akili baada ya Bwana Yesu kuyasema mambo hayo? Je, imerekodiwa kama walipata adhabu yoyote? Kuna uhakika kwamba hakukuwa na adhabu: Kusema hapa kwamba “hakukuwa” si kwamba haikurekodiwa, lakini kwa hakika hakukuwa na matokeo yoyote ambayo yangeonekana kwa macho ya binadamu. Neno hili “hakukuwa” linaelezea suala, yaani, mwelekeo na kanuni za Mungu katika kushughulikia mambo fulani. Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga, au hata wale wanaomkashifu—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mwelekeo wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mwelekeo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao. Hata hivyo, baada ya Mungu kusema mambo haya, watu bado wangeona kwa nadra ukweli wa namna ambavyo Mungu angeshughulikia watu hao, na wasingeelewa kanuni zinazotawala matokeo ya Mungu, hukumu Yake kwao. Hiyo ni kusema, wanadamu hawawezi kuuona mwelekeo na mbinu fulani za Mungu katika kuwashughulikia. Hali hii inahusu kanuni za Mungu za kufanya mambo. Mungu hutumia ujio wa hoja katika kushughulikia tabia yenye uovu ya baadhi ya watu. Yaani, Hatangazi dhambi yao na haamui matokeo yao, lakini Anatumia moja kwa moja ujio wa hoja ili kuwaruhusu kuadhibiwa, wao kupata adhabu wanayostahili. Wakati hoja hizi zinapofanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia ya uovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuona ya kuadhibiwa au kuuawa. Hii ni kwa sababu katika hali zile ambazo Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, kutoonyesha tena rehema au uvumilivu kwao, kutowapa fursa zaidi, mwelekeo Anaouchukua kwao ni kuwaweka pembeni. Ni nini maana ya “kuweka pembeni”? Maana ya kauli hii kibinafsi ni kuweka kitu kwa upande mmoja, kutokizingatia tena. Lakini hapa, wakati Mungu “anapomweka mtu pembeni,” kuna fafanuzi mbili tofauti kuhusu kile Alicho: Ufafanuzi wa kwanza ni kwamba Amempa Shetani kuyashughulikia maisha ya mtu huyo, na kila kitu cha mtu huyo. Mungu hatamwajibikia tena na Hataweza kumsimamia tena. Kama mtu huyo amerukwa na akili, au ni mpumbavu, na kama katika maisha au kifo, au kama angeshushwa jahanamu ili kupata adhabu yake, hayo yote yasingemhusu Mungu. Hiyo ingemaanisha kwamba kiumbe hicho hakitakuwa na uhusiano wowote na Muumba. Ufafanuzi wa pili ni kwamba Mungu ameamua kwamba Yeye Mwenyewe anataka kufanya kitu na mtu huyu, kwa mikono Yake mwenyewe. Inawezekana kwamba Ataweza kutumia huduma ya mtu wa aina hii, au kwamba atatumia mtu wa aina hii kama foili[a]. Inawezekana kwamba Atakuwa na njia maalum ya kushughulikia mtu wa aina hii, njia maalum ya kumshughulikia—kama tu Paulo. Hii ndio kanuni na mwelekeo katika moyo wa Mungu kuhusu namna Alivyoamua kumshughulikia mtu wa aina hii. Hivyo basi wakati watu wanapompinga Mungu, na kumkashifu na kumkufuru Yeye, kama wataendelea kusema ubaya kuhusu tabia Yake, au kama watafikia ile hali ya kimsingi ya Mungu, athari zake hazifikiriki. Athari zile mbaya zaidi ni kwamba Mungu anayakabidhi maisha yao na kila kitu chao kwa Shetani, mara moja na kabisa. Hawatasamehewa daima dawamu. Hii inamaanisha kwamba mtu huyu amekuwa chakula katika kinywa cha Shetani, mwanasesere katika mikono yake, na kuanzia hapo, Mungu hahusiki naye. Mnaweza kufikiria ni aina gani ya masikitiko iliyokuweko wakati Shetani alipomjaribu Ayubu? Katika hali kwamba Shetani hakuruhusiwa kuyadhuru maisha ya Ayubu, Ayubu aliteseka pakubwa. Na huoni kwamba ni ngumu hata zaidi kufikiria kupitia kwa mateso ya Shetani namna ambavyo mtu atakavyopitia ambaye amekabidhiwa Shetani kabisa, ambaye yumo katika mashiko ya Shetani kabisa, ambaye amepoteza kabisa utunzaji na rehema ya Mungu, ambaye hayuko tena katika utawala wa Muumba, ambaye amenyang’anywa haki ya kumwabudu Yeye, na haki ya kuwa kiumbe katika utawala wa Mungu, ambaye uhusiano wake na Bwana wa uumbaji umekatizwa kabisa? Kuteswa kwa Ayubu na Shetani kulikwa jambo ambalo lingeonekana kwa macho ya binadamu, lakini Mungu anapomkabidhi Shetani maisha ya mtu, athari zake zitakuwa jambo ambalo mtu hawezi kufikiria. Ni sawa tu na baadhi ya watu kuweza kuzaliwa tena wakiwa ng’ombe, au punda, au baadhi ya watu wakichukuliwa kabisa, na kupagawa na roho chafu, za uovu, na kadhalika. Haya ndiyo matokeo, mwisho wa baadhi ya watu ambao Mungu anawakabidhi kwa Shetani. Kwa nje, yaonekana kwamba watu hao waliomdhihaki, waliomkashifu, kumshutumu, na kumkufuru Bwana Yesu hawakupata athari zozote. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Mungu Anao mwelekeo wa kushughulikia kila kitu. Huenda Asitumie lugha wazi kuwaambia watu matokeo ya namna Anavyowashughulikia kila aina ya watu. Wakati mwingine Haongei kwa njia ya moja kwa moja, lakini Anafanya mambo kwa njia ya moja kwa moja. Kwamba haongelei jambo haimaanishi kwamba hakuna matokeo—yawezekana kwamba matokeo ni mabaya zaidi. Inavyoonekana, yaelekea Mungu haongei na watu fulani ili kufichua mwelekeo Wake; kwa uhakika, Mungu hajataka kuwaza juu yao kwa muda mrefu. Hataki kuwaona tena. Kwa sababu ya mambo ambayo wamefanya, tabia yao, kwa sababu ya asili yao na kiini chao, Mungu anawataka tu watoweke machoni Mwake, Anataka kuwakabidhi moja kwa moja kwa Shetani, kumpa Shetani roho yao, nafsi yao na mwili wao, kumruhusu Shetani kufanya atakacho. Ni wazi ni hadi kiwango gani Mungu anawachukia, ni hadi kiwango gani Ameudhika nao. Kama mtu atamghadhabisha Mungu kufikia kiwango ambacho Mungu hataki kumwona tena, kwamba Atakata tamaa kabisa naye, hadi katika kiwango ambacho Mungu hataki tena kushughulika naye Yeye mwenyewe—kama itafikia kiwango hiki ambapo Atawakabidhi kwa Shetani ili aweze kufanya apendavyo, kumruhusu Shetani kumdhibiti, kumtumia, na kumtendea kwa njia yoyote—mtu huyu kwa kweli amemalizika. Haki yake ya kuwa binadamu imebatilishwa kabisa, na haki yake ya kuwa kiumbe imefikia mwisho. Je, huoni kwamba hii ndiyo adhabu mbaya zaidi?
Yote haya yaliyo hapo juu ni maelezo kamilifu ya maneno: “hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja,” na pia ni utoaji maoni mwepesi kuhusu dondoo za maandiko haya. Nafikiri kwamba mnao ufahamu wake sasa!
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?