Mungu Huumba, Hutawala na Kusimamia yote kwa ajili tu ya Kuendelea Kuishi kwa Wanadamu
Kuhusu hadithi mbili ambazo Nimezisema, ingawa zinaweza kuwa na maudhui ambayo si ya kawaida na zinaweza kuwa zimesimuliwa na kuwasilishwa kwako kwa mtindo wa kipekee, hata hivyo Nilitaka kutumia lugha ya moja kwa moja na njia rahisi ili kwamba ungeweza kukubali na kuelewa kitu ambacho ni cha kina zaidi. Hili ndilo lilikuwa lengo langu tu. Nilitaka mwone na kuamini kuwa Mungu ni Mtawala wa vitu vyote kutokana na hadithi hizi ndogo na matukio. Lengo la kusimulia hadithi hizi ni kuwafanya mwone na kujua matendo ya Mungu yasiyokuwa na kikomo ndani ya hadithi yenye kikomo. Kuhusu ni lini mtafikia kikamilifu matokeo haya ndani yenu inategemea uzoefu wako binafsi na maendeleo yako binafsi. Ukifuatilia ukweli na ikiwa unatafuta kumjua Mungu, basi mambo haya yatafanya kazi kama kumbusho lenye nguvu na imara kwako; yatakufanya uwe na utambuzi wa kina sana, ubayana katika uelewa wako, na polepole utasogea karibu na matendo ya kweli ya Mungu, ukaribu ambao utakuwepo bila umbali na bila hitilafu. Hata hivyo, kama hutafuti kumjua Mungu, basi hadithi hizo ulizozisikia haziwezi kukudhuru. Mnaweza kuzichukulia kama hadithi za kweli.
Je, mlielewa kitu chochote kwenye hadithi hizi mbili? Kwanza, je, hadithi hizi mbili zinajitenga na mjadala wetu wa awali kuhusu Mungu kumjali binadamu? Je, kuna uhusiano usioepukika? Je, ni kweli kwamba ndani ya hadithi hizi mbili tunaona matendo ya Mungu na kujali kwa kiwangi kikubwa Anakokipa kila kitu Anachopanga kwa ajili ya binadamu? Je, ni kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya na mawazo Yake yote yanaelekezwa kwa uwepo wa binadamu? (Ndiyo.) Je, sio kwamba fikra makini za Mungu na kujali kwake binadamu kuko dhahiri? Binadamu hana haja ya kufanya chochote. Mungu amewaandaliwa watu hewa—kile wanachohitaji kufanya ni kuivuta tu. Mboga na matunda wanayokula vinapatikana kwa urahisi. Kutoka kaskazini hadi kusini, kutoka mashariki hadi magharibi, kila kanda ina rasilimali zake asili na mazao na matunda tofauti na mboga zimeandaliwa na Mungu. Tukizungumza juu ya mazingira mapana, Mungu aliumba vitu vyote viimarishane, vitegemeane, vitiane nguvu, vishindane na viishi pamoja. Hii ni mbinu Yake na sheria Yake ya kudumisha kuendelea kuishi na kuwepo kwa vitu vyote; kwa njia hii, binadamu ameishi kwa utulivu na kwa amani na amekua na kuzaliana kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira haya hai hadi siku ya leo. Yaani, Mungu anaweka uwiano katika mazingira ya asili. Kama kusingekuwa na udhibiti na ukuu wa Mungu, hakuna mwanadamu ambaye angeweza kudumisha na kuweka wiano katika mazingira, hata kama bado yangekuwa yaliumbwa na Mungu, bado yangukuwa zaidi ya uwezo wa mtu yeyote kuyalinda na kuyaweka katika usawa. Katika baadhi ya maeneo hakuna hewa, hivyo watu hawawezi kuishi hapo na Mungu hatakuruhusu uende kwa wao. Hivyo, usivuke mipaka inayostahili. Hili ni kwa ajili ya usalama wa binadamu—kuna siri ndani yake. Kila kipengele cha mazingira, urefu na upana wa dunia, na kila kiumbe hai duniani—vilivyo hai na vilivyokufa—viliandaliwa na Mungu na Alivifikiria: Kwa nini kitu hiki kinahitajika? Kwa nini sio cha lazima? Lengo la kuwa na kitu hiki hapa ni nini na kwa nini kiende hapo? Mungu alikuwa amekwishafikiria hii yote na hakuna haja ya watu kuyafikiria. Kuna baadhi ya watu wapumbavu ambao siku zote wanafikiri juu ya kuhamisha milima, lakini badala ya kufanya hivyo, kwa nini wasihamie kwenye tambarare? Kama huipendi milima, kwa nini unakwenda kuishi karibu nayo? Huu si upumbavu? Nini hutokea ikiwa utauhamisha mlima huo? Kimbunga kikali kitavuma au wimbi kubwa litapiga na makazi ya watu yataharibiwa. Je, hicho kisingekuwa kitu cha kipumbavu kufanya? Watu wanaweza tu kuharibu. Hawawezi hata kudumisha pahali pa pekee waliponapo pa kuishi, na ilhali wanataka kukimu vitu vyote. Hili haliwezekani.
Mungu anamwacha mwanadamu kusimamia vitu vyote na kuwa na utawala juu yao, lakini mwanadamu anafanya kazi nzuri? Mwanadamu ana tabia ya uharibifu; mwanadamu sio kwamba tu hawezi kutunza vitu kama Mungu alivyoviumba, kwa kweli ameviharibu. Binadamu ameifanya milima kuwa vifusi, ameijaza bahari kwa mchanga, na amezibadilisha tambarare kuwa majangwa ambapo hakuna kinachoweza kuishi. Halafu katika majangwa hayo mwanadamu amejenga viwanda na kujenga vinu vya nyuklia na uharibifu unaendelea katika pande zote. Mito si mito tena, bahari si bahari tena…. Binadamu anapovunja uwiano na kanuni za maumbile, siku yao ya maafa na kifo haipo mbali na haiepukiki. Maafa yanapokuja, watajua viumbe vya Mungu ni vya thamani kiasi gani jinsi vyote ni muhimu kwa binadamu. Mwanadamu kuishi katika mazingira yenye hali ya hewa nzuri ni sawa na kuwa peponi. Watu hawatambui baraka hii, lakini wakati ambapo wataipoteza yote ndipo watatambua ni jinsi gani yote ni adimu na ya thamani. Ni kwa jinsi gani mtu anaweza kuirudisha hii yote? Watu wangefanyaje ikiwa Mungu Asingekuwa tayari kuitengeneza tena? Mngefanyaje? (Tusingeweza kufanya chochote.) Kwa kweli, kuna kitu mnachoweza kufanya na ni rahisi sana na Nitakapowaambia ni nini, mara moja mtajua kwamba hiyo inawezekana. Kwa nini mwanadamu amejikuta katika mashaka yake ya kimazingira ya sasa? Je, ni kwa sababu ya tamaa na uharibifu wa mwanadamu? Ikiwa mwanadamu atasitisha uharibifu huu, je, mazingira ya kuishi hayatakuwa sawa taratibu yenyewe? Ikiwa Mungu hafanyi chochote, ikiwa Mungu hatamani tena kufanya kitu chochote kwa ajili ya binadamu—yaani, hataki kuingilia—njia bora zaidi ingekuwa ni binadamu kusitisha uharibifu huu na kurudisha vitu kuwa vile vilivyokuwa. Kusitisha uharibifu huu wote humaanisha kusitisha uporaji na uharibifu wa vitu ambavyo Mungu ameviumba. Hii itaruhusu mazingira ambamo mwanadamu anaishi kuboreka taratibu. Kushindwa kufanya hivyo kutasababisha uharibifu zaidi wa mazingira na hali itakuwa mbaya zaidi. Je, mbinu Yangu ni rahisi? Ni rahisi na inawezekana, siyo? Ni rahisi kweli, na inawezekana kwa baadhi ya watu, lakini je, hii inawezekana kwa watu walio wengi duniani? (Haiwezekani.) Kwenu nyinyi, angalau inawezekana? (Ndiyo.) Chanzo cha “ndiyo” yenu ni nini? Je, mtu anaweza kusema kuwa inahusisha kuanzisha msingi wa uelewa kuhusu matendo ya Mungu? Je, mtu anaweza kusema inahusisha kushikilia kanuni na mpango wa Mungu? (Ndiyo.) Kuna njia ya kubadilisha haya yote, lakini hiyo siyo mada tunayoijadili sasa. Mungu anawajibika kwa kila uhai wa binadamu na anawajibika hadi mwisho. Mungu Anawakimu, hata kama umeugua kutokana na mazingira yaliyoharibiwa na Shetani, au kuathiriwa na uchafuzi au kupata madhara mengine, haijalishi; Mungu Anakukimu na Atakuacha uendelee kuishi. Je, una imani katika hili? (Ndiyo.) Mungu hachukulii upotevu wa maisha ya binadamu kwa urahisi.
Mmehisi umuhimu wa kumtambua Mungu kama chanzo cha uhai kwa vitu vyote? (Ndiyo, tumehisi.) Mna hisia gani? Endelea, nitasikiliza. (Hapo awali, hatukufikiria kamwe kuhusisha milima, bahari na maziwa na matendo ya Mungu. Haikuwa hadi tuliposikia ushirika wa Mungu leo ndipo tulielewa kwamba vitu hivi vina matendo na hekima ya Mungu ndani yavyo; tunaona kwamba hata wakati ambapo Mungu alianza kuumba vitu vyote, Alikuwa tayari amekijaza kila kitu na hatima na nia Yake njema. Vitu vyote vinaimarishana na kutegemeana na binadamu ndiye anayenufaika mwishowe. Tulichokisikia leo kinaonekana ni kipya na kigeni, na tumehisi jinsi ambavyo matendo ya Mungu ni halisi. Katika dunia halisi, katika maisha yetu ya kila siku, na katika mwingiliano wetu na vitu vyote, tunaona kwamba hili liko hivyo) Unaiona kabisa, sio? Mungu kumkimu binadamu sio bila msingi imara, hatamki tu maneno machache na kuishia hapo tu. Mungu anafanya mambo mengi, hata vitu ambavyo huvioni anafanya kwa manufaa yako. Mwanadamu anaishi katika mazingira haya, ulimwengu huu ambao Mungu Aliutengeneza, na ndani yake watu na vitu vingine vinategemeana, kama tu ambavyo gesi inayotoka kwenye mimea inaitakasa hewa na kuwanufaisha watu wanaoivuta. Hata hivyo, baadhi ya mimea ni yenye sumu kwa watu, ilhali mimea mingine inakinza mimea yenye sumu. Haya ni maajabu ya uumbaji wa Mungu! Lakini hebu tuiache mada hii kwa sasa; leo, mjadala wetu hasa ulihusu kuishi pamoja kwa mwanadamu na viumbe vingine, ambavyo mwanadamu hawezi kuishi bila. Ni nini umuhimu wa uumbaji wa Mungu wa vitu vyote? Mwanadamu hawezi kuishi bila vitu vingine, kama ambavyo mwanadamu anahitaji hewa kuweza kuishi na namna ambavyo kama ungewekwa kwenye ombwe ungekufa upesi. Hii ni kanuni ya msingi sana kukufanya kuona kwamba mwanadamu anahitaji vitu vingine. Hivyo ni aina gani ya mtazamo ambao mwanadamu anapaswa kuwa nao kwa vitu vyote? Vithamini sana, vitunze, vitumie kwa ufanisi, usiviharibu, usivipoteze, na usivibadilishe kwa ghafula, maana vitu vyote vinatoka kwa Mungu na vinatolewa kwa binadamu na binadamu anapaswa kuvichukulia kwa uangalifu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?