Kuona Ugavi wa Mungu wa Wanadamu Kutoka kwa Mazingira Ya Msingi Ambayo Mungu Hutengeneza kwa ajili ya Wanadamu
Je, unaweza kuona, kutokana na jinsi Alishughulikia hali hizi tano za msingi za kuendelea kuishi kwa wanadamu, upeanaji wa Mungu kwa wanadamu? (Ndiyo.) Hiyo ni kusema kwamba Mungu aliumba msingi kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa wanadamu. Wakati huo huo, Mungu pia anasimamia na kudhibiti vitu hivi vyote, na hata sasa, baada ya wanadamu kuwepo kwa maelfu ya miaka, Mungu bado daima anabadilisha mazingira yao ya kuishi, kupeana mazingira ya kuishi yaliyo bora zaidi na ya kufaa zaidi kwa wanadamu ili maisha yao yaweze kudumishwa kwa kawaida. Haya yatadumishwa mpaka lini? Kwa maneno mengine, Mungu ataendelea kupeana mazingira kama haya kwa muda gani? Mpaka Mungu akamilishe kabisa kazi Yake ya usimamizi. Kisha, Mungu atabadilisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Huenda ikawa kupitia kwa mbinu zile zile, au huenda ikawa kupitia kwa mbinu tofauti, lakini kile ambacho watu wanahitaji kujua sasa ni kwamba Mungu daima anapeana mahitaji ya wanadamu, anasimamia mazingira ya kuishi ya wanadamu, na kutunza, kuhifadhi na kudumisha mazingira ya kuishi ya wanadamu. Ni kwa sababu ya mazingira kama hayo ndiyo watu waliochaguliwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kawaida hivyo na kukubali wokovu wa Mungu na kuadibu na hukumu. Vitu vyote vinaendelea kuwepo kwa sababu ya kanuni ya Mungu, wakati wanadamu wote wanaendelea kusonga mbele kwa sababu ya upeanaji wa Mungu kwa jinsi hii.
Je, sehemu hii ambayo Nimewasilisha sasa hivi imewaletea mawazo yoyote mapya? Je, sasa mnahisi tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu? Nani hasa ndiye bwana wa vitu vyote? Ni mwanadamu? (La.) Basi ni nini tofauti kati ya vile Mungu na wanadamu hushughulikia vitu vyote? (Mungu hutawala na kupanga vitu vyote, ilhali mwanadamu hufurahia vitu hivyo vyote.) Je, mnakubaliana na maneno hayo? Tofauti kubwa kabisa kati ya Mungu na wanadamu ni kwamba Mungu hutawala vitu vyote na hupeana vitu vyote. Mungu ni chanzo cha vitu vyote, na wanadamu hufurahia vitu vyote wakati Mungu anawapa. Hiyo ni kusema, mwanadamu hufurahia vitu vyote anapokubali maisha ambayo Mungu anatoa kwa vitu vyote. Wanadamu hufurahia matokeo ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote, ilhali Mungu ni Bwana. Kisha kutokana na mtazamo wa vitu vyote, ni nini tofauti kati ya Mungu na wanadamu? Mungu anaweza kuona vizuri mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote, na kudhibiti na kutawala mipangilio ya ukuaji wa vitu vyote. Yaani, vitu vyote vipo machoni mwa Mungu na katika eneo Lake la ukaguzi. Je, wanadamu wanaweza kuona vitu vyote? Kile ambacho wanadamu huona kimewekewa mipaka—ni tu kile wanachoona mbele ya macho yao. Ukiukwea mlima huu, unachoona ni mlima huu. Huwezi kuona kilicho upande mwingine wa mlima huo. Ukienda pwani, unaweza kuona upande huu wa bahari, lakini hujui upande ule mwingine wa bahari ulivyo. Ukiwasili katika msitu huu, unaweza kuona mimea iliyo mbele ya macho yako na inayokuzunguka, lakini huwezi kuona iliyo mbele zaidi. Wanadamu hawawezi kuona sehemu zilizo juu sana, mbali sana na kina sana. Kile wanachoweza kuona ni kilicho mbele ya macho yao na katika mpaka wa uwezo wao wa kuona. Hata kama wanadamu wanajua mpangilio wa misimu minne katika mwaka na mpangilio wa ukuaji wa vitu vyote, hawawezi kusimamia au kutawala vitu vyote. Kwa upande mwingine, vile Mungu aonavyo vitu vyote ni kama vile Mungu angeona mashine Aliyotengeneza binafsi. Angejua kila kijenzi vizuri kabisa. Kanuni zake ni zipi, mipangilio yake ni ipi, na kusudi lake ni lipi—Mungu anajua vitu hivi vyote wazi na dhahiri. Kwa hiyo Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu! Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli. Ndiyo maana ukitumia ufahamu na kile ulichojifunza kumsoma Mungu, hutaweza kamwe kujua au kuelewa Mungu. Lakini ukitumia njia ya kutafuta ukweli na kumtafuta Mungu, na kumtazama Mungu kutokana na mtazamo wa kuanza kumjua Mungu, basi siku moja utakubali kwamba matendo na hekima ya Mungu viko kila mahali, na utajua pia hasa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote na chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kadiri unavyokuwa na maarifa kama hayo, ndivyo utakavyoelewa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote. Vitu vyote na kila kitu, pamoja na wewe, daima vinapokea mtiririko thabiti wa upeanaji wa Mungu. Utaweza pia kuhisi dhahiri kwamba katika ulimwengu huu, na miongoni mwa wanadamu hawa, hakuna yeyote isipokuwa Mungu anayeweza kuwa na nguvu kama hizo na kiini kama hicho kutawala, kusimamia, na kudumisha kuwepo kwa vitu vyote. Ukitimiza ufahamu kama huo, utakubali kwa kweli kwamba Mungu ni Mungu wako. Ukifikia kiwango hiki, umemkubali Mungu kwa kweli na kumruhusu awe Mungu wako na Bwana wako. Ukiwa na ufahamu kama huo na maisha yako yakifikia kiwango kama hicho, Mungu hatakujaribu na kukuhukumu tena, wala Hatakushurutisha ufanye mambo, kwa sababu unamfahamu Mungu, unajua moyo Wake, na umemkubali Mungu kwa kweli ndani ya moyo wako. Hii ni sababu muhimu ya kuwasilisha mada hizi kuhusu utawala na usimamizi wa Mungu juu ya vitu vyote. Ni kuwapa watu maarifa na ufahamu zaidi; sio tu kukufanya ukubali, lakini kukupa maarifa zaidi na ufahamu wa utendaji wa matendo ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?