Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?
Maneno Husika ya Mungu:
Wale ambao walipagawa na roho wabaya hapo zamani (tangu kuzaliwa) watafichuliwa sasa. Nitakufukuza nje! Je, bado unakumbuka yale ambayo Nimeyasema? Mimi—Mungu mtakatifu na Asiye na waa—Siishi katika hekalu chafu na la kuchukiza. Wale ambao walikuwa wamepagawa na roho wabaya wanajua wenyewe, na Sihitaji kufafanua. Sijakujaalia! Wewe ni Shetani mkongwe, ilhali unataka kupenya katika ufalme Wangu! Hasha!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 81
Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya. Na watu wanaotumiwa na pepo wabaya (wale wenye nia mbaya, wale wanaotamani mwili au utajiri, wale wanaojikuza, wale wanaolivuruga kanisa, nk.) kila mmoja wao pia amebainika na Mimi. Usifikiri kwamba kila kitu kimemalizika punde pepo wabaya watatupwa nje. Hebu Nikwambie! Kuanzia sasa na kuendelea, Nitawaondoa watu hawa mmoja baada ya mwingine, nisiwatumie kamwe! Yaani, mtu yeyote aliyepotoshwa na pepo wabaya hatatumiwa na Mimi, na atafukuzwa! Usifikiri kuwa Sina hisia! Fahamu jambo hili! Mimi ndimi Mungu mtakatifu, na Sitakaa katika hekalu chafu! Mimi huwatumia tu watu waaminifu na wenye hekima ambao ni waaminifu kabisa Kwangu na wanaoweza kuudhukuru mzigo Wangu. Hii ni kwa sababu watu kama hao walijaaliwa na Mimi, na bila shaka hakuna pepo wabaya wanaowafanyia kazi hata kidogo. Hebu Nieleze wazi jambo moja: Kuanzia sasa na kuendelea, wale wote ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wana kazi ya pepo wabaya. Hebu Nirudie: Simtaki hata mtu mmoja ambaye pepo wabaya humfanyia kazi. Wote watatupwa kuzimuni pamoja na miili yao!
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 76
Mara nyingi watu hutaja kuzimu na jahanamu. Lakini maneno haya mawili yanarejelea nini, na tofauti kati yao ni ipi? Je, kweli yanarejelea pembe fulani ya baridi, ya giza? Akili ya binadamu daima inakatiza usimamizi Wangu, wakifikiria kwamba kutafakari kwao kusio na mpango maalumu ni kuzuri sana. Lakini haya yote ni mawazo yao wenyewe. Kuzimu na jahanamu zote zinarejelea hekalu la uchafu ambalo limeishiwa na Shetani awali au na roho wabaya. Hiyo ni kusema, yeyote ambaye amemilikiwa na Shetani au roho wabaya awali, ni wao ambao ni Kuzimu na wao ndio jahanamu—hakuna kosa kuhusu hilo! Hii ndiyo sababu Nimesisitiza kwa kurudia katika siku za nyuma kwamba Siishi katika hekalu la uchafu. Je, Mimi (Mungu Mwenyewe) Ninaweza kuishi Kuzimu, au jahanamu? Je, huo hauwezi kuwa upuuzi usio na maana? Nimesema hili mara kadhaa lakini ninyi bado hamwelewi Ninachomaanisha. Ikilinganishwa na jahanamu, Kuzimu imepotoshwa zaidi na Shetani. Wale ambao ni wa Kuzimu ndio walio katika hali mbaya sana, na Sijawaamulia kabla watu hawa kabisa; wale walio wa jahanamu ni wale Niliowaamulia kabla, lakini kisha wameondolewa. Kwa maneno rahisi, Sijamchagua hata mmoja wa watu hawa.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 90
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Wale walio na mashetani huishi kwa kudhihirisha asili yao mbaya mno, na asili hii mbaya mno huja kutoka roho waovu ambao wanakaa ndani yao. Asili ya roho waovu huwa asili ya ndani ya mtu aliye na mashetani. Asili husika ya mtu hutegemea roho husika ndani ya mtu huyo, na sifa bainifu ya asili ya mtu huyo huamua sifa bainifu ya tabia zao zilizopotoshwa—hii ni kweli kabisa. Wale walioteuliwa na kuchaguliwa na Mungu ni watu wote wenye roho ya binadamu. Wale wasio na roho za binadamu ni wale ambao ndani yao aina zote za roho waovu huishi. Kwa hivyo, watu hawa ni wale ambao ni wa mashetani waovu na roho waovu, na si walengwa wa wokovu wa Mungu. Walengwa wa wokovu wa Mungu ni wale wenye roho za binadamu. Ingawa watu hawa wamepotoshwa na Shetani, na wamesababisha asili ya kumpinga Mungu, wanaweza kusafishwa na kuokolewa kabisa. Hii ni kwa sababu ndani yao wana roho za binadamu, na sifa zao asili za binadamu na asili yao ni nzuri. Wale wasio na roho ya binadamu ni wanyama ama waovu, dubwana ndani ya vazi la binadamu, na hivyo Mungu hawaokoi; hii ni kwa sababu wao si wa wanadamu, na wanadamu, na hawajumuishwi katika binadamu ambao Mungu anazungumzia.
Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?