Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba

10/09/2019

Nyinyi nyote ni watu wazima. Baadhi yenu ni wa umri wa kati; baadhi mmefikisha umri wa uzee. Kutoka kwa yule asiyesadiki hadi kwa yule anayesadiki, na kuanzia mwanzo wa kusadiki kwa Mungu hadi kukubali neno la Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu, je, ni maarifa kiwango kipi mliyopata kuuhusu ukuu wa Mungu? Ni maono yapi mliyopata kwenye hatima yenu ya kuwa binadamu? Je, mtu anaweza kutimiza kila kitu anachotamani katika maisha? Je, ni mambo mangapi kwenye miongo michache iliyopita katika kuwepo kwenu mliyoweza kutimiza kama mlivyopenda? Ni mambo mangapi hayafanyiki kama yalivyotarajiwa? Ni mambo mangapi hutupata kwa mshangao mzuri? Ni mambo mangapi ambayo ungali unasubiri kutimia—unasubiri bila kufahamu muda sahihi, unasubiria mapenzi ya Mbinguni? Mambo mangapi yanakufanya uhisi kana kwamba huna wa kukusaidia na umezuiliwa? Watu wote wanayo matumaini kuhusu hatima yao, na hutarajia kwamba kila kitu katika maisha yao kitaenda sawa na wanavyopenda, kwamba hawatakosa chakula wala mavazi, kwamba utajiri wao utaongezeka pakubwa. Hakuna anayetaka maisha ya kimaskini na ya taabu, yaliyojaa ugumu, na kuandamwa na majanga. Lakini watu hawawezi kuona mbele au kudhibiti mambo haya. Pengine kwa baadhi ya watu, yaliyopita ni mchanganyiko tu wa yale mambo waliyoyapitia; hawajifunzi katu ni nini mapenzi ya Mbinguni, wala hawajali mapenzi hayo ni yapi. Wanaishi kwa kudhihirisha maisha yao bila kufikiria, kama wanyama, wakiishi siku baada ya siku, bila kujali kuhusu hatima ya binadamu ni nini, kuhusu ni kwa nini binadamu wako hai au vile wanavyostahili kuishi. Watu hawa hufikia umri wa uzee bila ya kufaidi ufahamu wowote wa hatima ya binadamu, na mpaka wakati ule wanapokufa hawana habari yoyote kuhusu maana ya maisha. Watu kama hao wamekufa; ni viumbe bila roho; wao ni wanyama. Ingawaje katika kuishi miongoni mwa mambo haya yote, watu hupata furaha kutoka kwa njia nyingi ambazo ulimwengu hutosheleza mahitaji yao ya anasa, ingawaje wanauona ulimwengu huu wa anasa ukiwa unapiga hatua bila kusita, hali yao binafsi waliyoipitia—kile ambacho mioyo yao na roho zao zinahisi na kupitia—hakina uhusiano wowote na mambo ya anasa, na hakuna kitu chochote cha anasa ambacho kinaweza kuchukua nafasi yake. Ni utambuzi ndani ya moyo wa mtu, kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa jicho vivyo hivyo tu. Utambuzi huu umo katika ufahamu wa mtu wa, na hisia za mtu za, maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Na mara nyingi humwongoza mtu katika kuelewa kwamba Bwana yule asiyeonekana anapanga vitu vyote, Anaunda kila kitu kwa ajili ya binadamu. Katikati ya haya yote, mtu hawezi kuepuka ila kukubali mipangilio na mipango ya hatima ya mambo; wakati uo huo, mtu hawezi kuepuka ila kukubali njia iliyo mbele ambayo Muumba amempangia, ukuu wa Muumba dhidi ya hatima ya mtu. Hii ndiyo hoja isiyopingika. Haijalishi ni maono na mtazamo gani ambao mtu anao kuhusu hatima yake, hakuna anayeweza kubadilisha hoja hii.

Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba

Pale utakapoenda kila siku, kile utakachofanya, yule au kile utakachokumbana nacho, kile utakachosema, kile kitakachokufanyikia—je, kati ya vyote hivi kipo kinachoweza kutabirika? Watu hawawezi kutabiri matukio haya yote, sikutajii kudhibiti namna ambavyo yanavyoendelea. Katika maisha, matukio haya yasiyotabirika hufanyika kila wakati, na ni tukio la kila siku. Mabadiliko haya ya kila siku na njia ambazo yanajitokeza, au ruwaza ambazo yanajitokeza, ni vikumbusho vya kila wakati kwa binadamu kwamba hakuna kinachofanyika bila mpango, kwamba njia ya maendeleo inayochukuliwa na mambo haya, na kutoepukika kwa mambo haya, haviwezi kubadilishwa na mapenzi ya binadamu. Kila tukio linaonyesha onyo kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu, na pia linatuma ujumbe kwamba, binadamu hawawezi kudhibiti hatima zao wenyewe; na wakati uo huo kila tukio ni upingaji wa malengo yasiyo na mwelekeo, yasiyo na maana ya binadamu na tamanio la kuchukua hatima yake na kutaka kuidhibiti mwenyewe. Ni sawa na makofi yenye nguvu juu ya masikio ya binadamu moja baada ya jingine, yanayolazimisha binadamu kufikiria upya ni nani, hatimaye, atatawala na kudhibiti hatima yao. Na kama vile malengo na matamanio yao yanavyokiukwa mara kwa mara na kusambaratika, binadamu kwa kawaida huishia kukubali kwa nadharia yao bila kufahamu kile ambacho hatima yao imesheheni, kukubali kwa uhalisi, kwa mapenzi ya Mbinguni na ukuu wa Muumba. Kutokana na mabadiliko haya ya kila siku katika hatima za maisha yote ya binadamu, hakuna kitu ambacho hakifichui mipango ya Muumba na ukuu Wake; hakuna kile ambacho hakiutumi ujumbe huu kwamba “yale mamlaka ya Muumba hayawezi kupitwa,” ambacho hakionyeshi ukweli wa milele kwamba “mamlaka ya Muumba ni ya juu zaidi.”

Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba? Ingawaje binadamu huona, kwenye sheria zile za malengo, ukuu wa Muumba na utaratibu Wake wa matukio yote na mambo yote, ni watu wangapi wanaweza kung’amua kanuni ya ukuu wa Muumba juu ya ulimwengu? Ni watu wangapi wanaweza kujua, kutambua, kukubali kwa kweli na kujinyenyekeza kwa ukuu na mpangilio wa Muumba dhidi ya hatima zao wenyewe? Nani, ambaye baada ya kusadiki hoja ya ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote, ataweza kusadiki kwa kweli na kutambua kwamba Muumba pia anaamrisha hatima hii ya maisha ya binadamu? Ni nani anayeweza kuelewa kwa kweli hoja hii kwamba hatima ya binadamu imo kwenye kiganja cha mkono wa Muumba? Aina ya mtazamo ambao binadamu wanafaa kuchukua katika ukuu wa Muumba, wanapokabiliwa na hoja kwamba Anatawala na kudhibiti hatima ya binadamu, ni uamuzi ambao kila binadamu ambaye kwa sasa anakabiliwa na hoja hii lazima ajiamulie mwenyewe.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kukua: Awamu ya Pili

Kutegemea na aina gani ya familia ambayo wamezaliwa ndani, watu hukua katika mazingira tofauti ya nyumbani na wakajifunza mafunzo tofauti...

Uzao: Awamu ya Tano

Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili...

Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza

Mahali ambapo mtu amezaliwa, ni familia gani alimozaliwa, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa—haya ndiyo maelezo ya awamu ya...

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp