Kuelewa na Kuukabili Ukweli wa Usimamizi wa Mungu wa Kudura ya Mwanadamu

10/09/2019

Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu

Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yenu ya hatima imebadilika? Mnaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama binadamu watayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!

Kuelewa na Kuukabili Ukweli wa Usimamizi wa Mungu wa Kudura ya Mwanadamu

Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu

Mwanadamu anatakiwa kuwa na mtazamo gani sasa katika kujua na kujali mamlaka ya Mungu, hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Hili ni tatizo la kweli linalokabili kila mmoja. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kweli ya maisha, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuangalia na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima wafuate, kuelewa matokeo ambayo Mungu ananuia kufanikisha katika binadamu na mafanikio Anayonuia kufikia ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kwa yote, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli katika binadamu. Mambo yote katika mipangilio na ukuu wa Mungu hutii sheria za kimaumbile, na kama utaamua kumwachia Mungu kupangilia na kuamuru kila kitu kwa niaba yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima mfanye kazi kwa bidii zaidi; na ndipo mnapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Iliyotangulia: Kifo: Awamu ya Sita

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kifo: Awamu ya Sita

Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya...

Uzao: Awamu ya Tano

Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili...

Uhuru: Awamu ya Tatu

Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye...

Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza

Mahali ambapo mtu amezaliwa, ni familia gani alimozaliwa, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa—haya ndiyo maelezo ya awamu ya...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp