Kuna tofauti ipi kati ya mtumishi mwema na mtumishi muovu?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu. Anaweza kuwaleta watu katika kanuni tu; kile anachowataka watu kufanya hakitofautiani kati ya mtu na mtu mwingine; hafanyi kazi kulingana na mahitaji halisi ya watu. Katika kazi ya aina hii kunakuwa na kanuni nyingi sana na mafundisho mengi sana, na haiwezi kuwaleta watu katika uhalisia au katika hali ya kawaida ya kukua katika uzima. Inaweza kuwawezesha watu tu kusimama kwa kanuni chache zisizokuwa na maana. Uongozi wa namna hii unaweza tu kuwapotosha watu. Anakuongoza ili uwe kama yeye; anaweza kukuleta katika kile anacho na kile alicho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kumfurahisha Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu anataka kufanya kinathibitishwa katika ushuhuda wa watu kama hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kama watu wanaomhudumia Mungu, kila mmoja wenu lazima aweze kulinda maslahi ya kanisa katika kila kitu mnachofanya, badala ya kuzingatia tu masilahi yenu wenyewe. Haikubaliki ninyi kutenda kila mtu peke yake, daima mkidhoofishana. Watu wanaotenda kwa namna hiyo hawafai kumhudumia Mungu! Watu kama hao wana tabia mbaya sana; hawana ubinadamu hata kidogo ndani yao. Wao ni Shetani asilimia mia moja! Wao ni wanyama! Hata sasa, mambo kama haya bado hutokea miongoni mwenu; hata mnafika kiasi cha kushambuliana wakati wa ushirika; mkitafuta visingizio kwa makusudi na kughadhabika sana mnapogombana kuhusu suala fulani lisilo la maana, pasiwe na mtu aliye radhi kujiweka kando, kila mtu akimfichia mwenzake fikira zake za ndani, akimtazama yule mwingine kwa makini na kuwa mwangalifu daima. Je, tabia ya aina hii inafaa katika kumhudumia Mungu? Je, kazi kama hiyo yako inaweza kuwapa ndugu zako chochote? Huwezi tu kuwaongoza watu kwenye njia sahihi ya maisha, lakini kwa kweli unawajaza ndugu zako tabia zako potovu. Je, huwadhuru wengine? Dhamiri yako ni mbaya na ni mbovu kabisa! Huingii katika uhalisi, wala huuweki ukweli katika vitendo. Aidha, unawafichulia wengine asili yako mbaya mno bila aibu. Huna aibu hata kidogo! Umeaminiwa ndugu hawa, lakini unawapeleka kuzimuni. Je, wewe si mtu ambaye dhamiri yake imekuwa mbovu? Huna aibu hata kidogo!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hudumu Jinsi Waisraeli Walivyohudumu

Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, lakini wanalitumia kanisa vibaya, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao ni doezi katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila dhidi ya ndugu zao na kuwadanganya, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kuvitupa vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kidogo, hata kama utaivunja miguu yako au mgongo wako ukitia bidii, au hata ukifa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha mambo ni kwamba: Atasema kwamba wewe ni mtenda maovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Viongozi wa kanisa na wafanyakazi wa ngazi zote wanaweza kuwekwa katika makundi matatu. Kuwaeleza wao kama watumishi waaminifu, watumishi waongo au watumishi waovu kunafaa zaidi. Aina ya kwanza wanaweza kweli kutii kazi ya Mungu, wanaweza kufanya kila wawezalo kulinda kazi ya Mungu huku wakitenda wajibu wao, wanaweza kuacha kila kitu ili kujitumia wenyewe kwa ajili ya Mungu, na wanaweza kutukuza na kushuhudia kwa Mungu. Kundi hili pekee la watu ndilo ambalo kweli hufuatilia ukweli, hutafuta kukamilishwa na huainishwa kama watumishi waaminifu wa Mungu. Aina ya pili hawana uhalisi wa ukweli kabisa, hawawezi kulinda kazi ya Mungu huku wakitenda wajibu wao, hawayashughulikii masuala kwa mujibu wa utaratibu wa kazi, hufanya chochote wanachotaka na hutenda bila hadhari, hutenda kulingana na upendeleo wao wa mwili, huwatendea watu kulingana na hisia zao, hawashiki kanuni za ukweli, wanashindwa kutenda ukweli, na mara nyingi wao hujaribu kufanya biashara na Mungu. Wako kwenye njia ya mpinga Kristo na huainishwa kama watumishi waongo. Aina ya tatu ni wenye kiburi na majivuno, hufuatilia hadhi, na wana tamaa ya makuu. Wao kila mara hutaka kuwadhibiti watu wa Mungu walioteuliwa, huwatawala wengine kimwinyi, na wao huwakandamiza na kuwabagua wale wasiokubaliana nao. Wao huwazuia, huwafunga na kuwanasa watu wa Mungu walioteuliwa, wao hujaribu kutumia uwezo wao kutawala watu wa Mungu walioteuliwa na kuanzisha ufalme wao ulio huru. Wanaainishwa kama watu waovu ambao ni wa namna sawa na viongozi wa uongo na wapinga Kristo, yaani, watumishi waovu. …

… Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya wale wenye ubinadamu mzuri ambao pia wanapenda ukweli. Wale ambao hawana ubinadamu mzuri na upendo wa ukweli hawana kazi ya Roho Mtakatifu. Mtu mwenye ubinadamu usio wa kutegemewa, mwovu na wenye kudhuru kwa siri ni mtu mwovu ambaye bila shaka anaainishwa kama mtumishi mwovu. Watumishi waovu ni maadui wa Mungu na walengwa wa hukumu na adhabu Yake. Kueleza aina hizi tatu za viongozi na wafanyakazi kama watumishi waaminifu (kama waaminifu ambao wasioamini huzungumza juu yao), watumishi wasio waaminifu (kama maofisa wa mahakama wasio waaminifu ambao wasioamini huzungumza juu yao), na watumishi waovu (kama watu wabaya kabisa ambao husaliti nchi na kwenda kwa adui ambao wasioamini huzungumza juu yao) kunafaa sana. Wale wanaoainishwa kama watumishi waaminifu ni wa kweli zaidi, wana dhamiri na hisia, na wao hutetea kazi ya Mungu katika vitu vyote wakati wa kufanya wajibu wao. Wao ni watiifu na waaminifu kwa Mungu. Viongozi na wafanyakazi wote kama hao ni walengwa wa wokovu na ukamilishaji wa Mungu. Wale wanaoainishwa kama watumishi waongo hawapendi ukweli, hawako tayari kufuatilia ukweli na hawaonyeshi utiifu wa kweli kwa Mungu. Katika kutekeleza wajibu wao, wao hufanya chochote wanachotaka. Wao huwatendea watu kulingana na hisia zao na si wenye haki au mantiki. Katika huduma yao kwa Mungu wao humpinga, hufuata mwili, na kufanya mambo bila kanuni, hata wakijaribu kufanya biashara na Mungu. Wakati mwingine wanaweza kusaliti ukweli na Mungu, na hata kufanya kazi dhidi ya maslahi ya nyumba ya Mungu, bila kulinda kazi ya Mungu hata kidogo. Watu kama hawa huainishwa kama watumishi waongo, kama vile tu viongozi waongo wa mahakama ambao wasioamini huzungumza juu yao. … Bila shaka, watumishi wote waongo huainishwa kama viongozi na wafanyakazi wadanganyifu. Hata hivyo, viongozi na wafanyakazi wengine wadanganyifu wana ubinadamu mzuri na wanaweza kabisa kutubu na kubadilika. Lazima watendewe kwa upendo na kupewa nafasi nyingine ya kutenda. Lakini wale ambao ni watumishi waovu wote ni viongozi wa uwongo na wapinga Kristo ambao wana asili mbovu sana. Bila shaka, watumishi wote waovu huainishwa kama watu waovu. Wana asili na kiini cha ibilisi, ndiyo sababu watu hawa waovu wana uwezo wa kutenda kila aina ya uovu na huwakandamiza na kuwatesa watu wa Mungu walioteuliwa kwa ukatili. Wao hufanya kila wawezalo kuvuruga na kukatiza kazi ya Mungu na kumpinga Mungu katika kila kitu, kama kwamba hawana hisia kabisa. Mioyo yao ni migumu na yenye ukaidi. Je, si huku ni kuwa adui wa Mungu? Watumishi waovu hawawezi kuokolewa. Kwa hivyo, nyumba ya Mungu lazima iwafukuze viongozi wowote waongo na wapinga Kristo wa asili ya pepo. Hakuna nafasi ya upatanisho.

Kimetoholewa kutoka katika Mipango ya Kazi

Kama wale wanaotoa huduma kweli wana uwezo, wale walio chini yao watashirikiana na wao—kutakuwa na hali ya jumla ya mvutano na upatanifu kamili wa nguvu, na maisha ya kanisa yatastawishwa kila uchao. Hakutakuwa na uhasi au kubaki nyuma. Haki itazidi kuwa na washirika wote wa kanisa watakuwa wa akili moja; wataungana katika jitihada zao. Wote wataweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kumtukuza. Haya ndiyo matokeo bora zaidi. Kama kanisa bado linachosha na watu wengi zaidi ni hasi, ni ushahidi kwamba hakuna njia katika mwongozo wako. Maisha ya kanisa ni kama gari la farasi na kiongozi ni kama farasi wa kuvuta gari. Farasi akitimiza kusudi lake, basi gari linaweza kuvutwa mbele; hutembea wakati anapaswa kutembea na hupiga hatua anapopaswa kupiga hatua. Hakuna kitu kinachoweza kumzuia. Wakati mtu amestahiki kabisa kumtumikia Mungu, matatizo yote yanaweza kutatuliwa popote aendapo; anaweza kuwasaidia kutatua matatizo yoyote waliyo nayo na kuwaonyesha suluhisho. Ni furaha kubwa kwa wengine, kama kwamba mzigo umeinuliwa kutoka mabegani mwao. Haijalishi hali ya mahali ilivyo ngumu kiasi gani, akikaa hapo siku chache na kuwakusanya watu kwa mikutano michache, mioyo yao itachangamka. Wao watajazwa na nguvu mara wanapoelewa ukweli na uhasi wao utatatuliwa kabisa. Ugomvi wa mwili utazimwa na maisha ya kanisa yataingia kwenye njia sahihi. Mtu anayemtumikia Mungu kweli anaweza kung’amua upungufu wa wengine, anajua ni aina gani ya lishe wanayohitaji watu tofauti, ni wapi pa kuanzia, na jinsi ya kutatua matatizo kabisa. Haijalishi kama ni mwumini mpya au wa zamani, mzee au kijana, anayeongoza au anayefuata, anaweza kuwatolea lishe ya kutosha. Matatizo yao yote yanaweza kutatuliwa na anaweza kuwasiliana na watu wote. Kwa wale ambao wanaweza kumtumikia Mungu kweli, hakuna sheria katika kushiriki juu ya ukweli; hawafanyi hivyo kwa ghibu, lakini wanazungumza kutoka kila upande na kutoka kila pembe. Wanaweza kuelezea mambo kwa maneno tofauti na kuleta pamoja kila aina ya ukweli, na watu wa kila tabaka wataelewa na kupata manufaa. Kila mtu hupenda kuwa karibu na wale wanaomtumikia Mungu kweli; wao wako tayari kufungua mioyo yao na kuwa na ushirika nao, wanawaheshimu, na wako tayari kufanya urafiki nao na kuwa na mazungumzo ya dhati. Ikiwa kila mtu anaogopa na kujificha kutoka kwako, basi una shida. Paka mweusi kuvuka njia yako ni bahati mbaya. Wale ambao mioyo yao inalingana na mapenzi ya Mungu daima wako kanisani, wakitembea miongoni mwa walengwa wa kazi yao, wakiishi na kula pamoja na watu, na kuongea na watu usiku kucha. Wanawahimiza watu mara kwa mara wanapowaaminia kazi; na wao wanaogopa kutofanya vitu vizuri na kamwe hawampuuzi mtu yeyote. Wanajua kwamba kuondoka mahali pa kazi ni kutowajibikia kazi—wale ambao wanawaacha watu wanaowafanyia kazi ni wadoezi tu. Je, inawezekana kutatua shida zote za vitendo bila kuwasiliana na viongozi na wafanyakazi wa umma ambao huratibu nawe? Je, inaweza kufanyika bila kupitia maisha ya kanisa katika ngazi ya msingi kwa kina? Je, kuna chochote kinachoweza kutimizwa bila mawasiliano ya dhati? Je, unaweza kuiacha kazi yako kabla sauti yako kupwelea? Je, bado wewe hubeba mzigo wako wakati huna juhudi moyoni mwako? Ikiwa hujapunguza uzito, je, wewe ni mwenye bidii kweli? Je, wale wanaolenga chakula na mavazi yao wanajali kweli kuhusu matunda yaliyotokana na kazi yao? Je, wanaweza kuyazingatia mapenzi ya Mungu? Je, wanaweza kweli kufanya kazi nzuri ikiwa wanawasiliana na watu wachache tu ambao wanawapendeza huku wakiwaepa wale wasiowapendeza? Je, wao sio wanyonyaji wanaotafuta maisha rahisi, yenye starehe na yenye kufurahiwa?

Wale ambao wanaweza kumtumikia Mungu kweli wanajua ni wapi walipopungukiwa; wanaweza kujitayarisha na kufidia upungufu wao wakati wowote huku pia wakiwasiliana ukweli ili kutoa lishe kwa wengine. Hata zaidi, wao hulenga kuingia katika ukweli wenyewe na kujijua kwa undani zaidi. Wanaweza kujizuia kuwa wenye kiburi, wenye kujidai na kujionyesha; wao pia wako tayari kujiweka wazi, kuwaruhusu wengine kuona udhaifu na upungufu wao. Kwa hiyo ushirika wao ni wa dhati na wa kweli bila ya kisingizio chochote cha wa uongo. Watu watakuwa na imani nao na wanaweza kuwaheshimu na pia kutii ukweli wanaoshiriki kuhusu. Wale wanaomtumikia Mungu kweli wanaelewa kazi ya Roho Mtakatifu na wanajua ni nini kinachotokana na uzoefu wao wenyewe na kile kinachotokana na nuru ya Roho Mtakatifu. Wao wana mioyo inayomcha Mungu na hawana kiburi wala hawajisifu. Hawawadharau wengine kwa sababu wana kazi ya Roho Mtakatifu, lakini wana uwezo zaidi wa kuwafikiria wengine, kuwajali wengine, na kuwasaidia wengine. Wanaona heri kuteseka ili wengine wawe na furaha. Wanaelewa ugumu ambao watu wanakabiliwa nao na pia wanaelewa kwa kina jinsi ilivyo uchungu kwa mtu asiye na ukweli kuanguka gizani. Zaidi ya hayo, wanaelewa raha za kupewa nuru na Roho Mtakatifu na wako tayari kushiriki nuru kama hiyo na wengine, na vile vile furaha inayoletwa na nuru hiyo. Hawachukulii kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu wao wenyewe kama mtaji wa kufurahia. Wanafurahia kazi ya Roho Mtakatifu na wanajali kuhusu mapenzi ya Mungu. Wao wako tayari kutatua shida na maumivu ya watu wengine na kupitisha raha wanayopata kutokana na kazi ya Roho Mtakatifu kwa wengine ili kumridhisha Mungu. Wanaweza kushirikiana kwa utendaji na kazi ya Roho Mtakatifu, kuonyesha kila fikira kwa mapenzi ya Mungu na kuacha furaha yao wenyewe ili kumridhisha Mungu. Wanakataa baraka za hadhi na hawatafuti kutendewa kwa namna ya kipekee; wao kwa hiari na kwa heshima wanamtumikia Mungu na hutenda wajibu wao kwa uaminifu. Ni watu wanaomtumikia Mungu kwa njia hii tu ndio hutenda kulingana na mapenzi ya Mungu.

Ili kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, mtu lazima kwanza apitie mabadiliko katika tabia ya maisha yake. Baada ya mabadiliko hayo, mtu anaweza kuanza kutumikia rasmi. Uzoefu wa miaka michache unahitajika, na bila ukweli hakuna matokeo mazuri yanayoweza kupatikana. Lakini kama watu wanaelewa kwa kweli maana ya kweli ya huduma, watajua jinsi ya kufanya wajibu wao vizuri. Kwa sababu wanaelewa kwa kina kwamba kufanya wajibu wa mtu ni kuwatolea wengine ukweli, njia, na uzima ambavyo mtu amepata kutokana na kazi ya Mungu, na kulipa kanisa uzoefu, maarifa ya Mungu na nuru iliyofichuliwa na Roho Mtakatifu, ili wengine waweze kushiriki, na ili wote waweze kufanikisha mabadiliko katika tabia zao, wapate kumjua Mungu, kumtii Mungu, kuwa waaminifu kwa Mungu na kupatwa na Mungu. Sio kujiandaa wenyewe na maarifa ya ukweli na kuwafundisha wengine maneno na mafundisho ili kuonyesha jinsi walivyo wastadi. Kutenda wajibu wa mtu ni kutunza, kusaidia, kufikiria na kuwajali wengine kwa upendo wa Mungu, kuwajali wengine kuliko kujijali, daima kufikiria kuwahusu wengine, kufanya kila kitu ukiwa na kanisa mawazoni, kupendelea kuteseka kwa ajili ya watu wengi zaidi kupata uzima na kuokolewa, na kulipa gharama yoyote ili watu waweze kuelewa ukweli na kujitumia wenyewe kwa ajili ya Mungu ili kuridhisha mapenzi ya Mungu. Sio kujivuna kwa sababu ya hadhi yako au kushikilia furaha za mwili bila kujali kiasi ambacho ndugu wako wanateseka, au kuridhisha tu hamu yako ya kula, kunywa na kutafuta raha huku ukiacha faida za ndugu zao. Watu wengine hata hufanya kazi kulingana na mapendeleo na hisia zao wenyewe. Mtu akiwapokea vizuri na kupata fadhila yao, watashirikiana nao, vinginevyo watakataa. Mtu anayedharauliwa zaidi ni yule anayefanya kazi yake na anataka kitu kama malipo. Kutenda wajibu wa mtu ni kuchukua mapenzi ya Mungu kama ya mtu mwenyewe, kuchulia kama dharura kile ambacho Mungu anachukulia kama dharura, kufikiria kile ambacho Mungu anafikiria, kuwa na wasiwasi juu ya yale ambayo Mungu ana wasiwasi nayo, na kuweka mbele maslahi ya familia ya Mungu wakati wote. Ni kufanya kazi kwa bidii sana kiasi kwamba mtu anasahau kula na kulala, na ni kujitahidi sana na kufanya kazi ambayo Mungu amemwaminia mtu kufanya na hisia ya jukumu la bwana. Sio kutarajia kupewa tuzo kwa kazi kidogo, au kutarajia kufurahia baada ya mateso kidogo, au kuwa na majivuno na kujisifu baada ya kufanikisha matokeo fulani, au kufurahia hadhi na kutenda kama dikteta. Wale ambao ni waaminifu katika kufanya wajibu wao hutii mipangilio ya Mungu, ni waaminifu, wanajitolea, na hufanya kazi kwa kujitolea na bila malalamiko kama watumishi wa Mungu, wakitamani tu kulipiza upendo wa Mungu na kumlipa Mungu kwa maisha yao. Wao wanajiona tu kuwa kipande cha udongo usio na heshima, na hata wasiostahili kufurahia neema ya Mungu, na wanatii kikamilifu mipangilio ya Mungu na wala hawalalamiki. Wao sio wanafiki batili na wasio na aibu wanaojali maisha yao wenyewe, ambao wana nia za kupokea baraka, na ambao wanatamani kuwa bora kuliko wengine na kufurahia kuwa wakubwa kuliko wengine. Kufanya wajibu wa mtu ni kuzingatia mapenzi ya Mungu na mzigo wa Mungu, kufikiria ndugu kama wazazi wa mtu, kuwa na hiari ya kuwa mtumishi wa kila mtu, kuzingatiana maisha ya ndugu, kuthubutu kuwajibika, kutokuwa na deni la yeyote, kuwaruhusu wengine kupata kitu chochote ambacho mtu amekipata, kumtumikia Mungu kwa dhamiri, na kuthubutu kukubali usimamizi wa kila mtu. Watu wengine husema mambo yanayopendeza lakini hawafanyi kazi halisi; wanafurahia ukarimu wa ndugu zao lakini bado wanawakandamiza, na wanawaomba wawafanyie jambo hili na lile, wafanye kila linalowezekana kuwahudumia. Nao huwakaripia na kuwashughulikia ndugu zao kila wakati, au wanawaambia waje wawatumikie wakati wao ni wagonjwa, na kuandamana nao inapohitajika. Mtu kama huyo anayewafanya watu kuwa watumishi wake hamtumikii Mungu hata kidogo; badala yake, anajitukuza, anajishuhudia, kujiinua na kuwafanya wengine wamtendee kama Mungu. Anaogopa sana kuwa mwenye sifa ya chini na kwa watu kutoshawishiwa naye. Yeye ni mwenye bidii katika jitihada zake na anastahimili maumivu yote ili awafanye watu wamtii na kumwabudu, na anaketi mahali pa Mungu akiwakaripia watu siku nzima. Anamdharau kila mtu, anafanya kila kitu awezacho kupanua uwanja wake wa ushawishi, na anafanya biashara zake mwenyewe ili kuwasababisha wengine wamweke katikati, wasikize maneno yake, watii mipangilio yake na kumweka Mungu upande mmoja ili wamwabudu badala yake. Baada ya yeye kufanya kazi kwa miaka kadhaa, watu anaowaongoza hawana ufahamu wa Mungu. Kinyume na hayo, wote wanamwogopa na kumtii yeye tu. Yeye mwenyewe amekuwa mungu. Kwa kufanya hivi, je, yeye hawaongozi watu mbele yake mwenyewe? Mtu wa aina hii ni mnyang’anyi, mwizi ndani ya familia, na ni mpinga Kristo.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp