Kukua: Awamu ya Pili

10/09/2019

Kutegemea na aina gani ya familia ambayo wamezaliwa ndani, watu hukua katika mazingira tofauti ya nyumbani na wakajifunza mafunzo tofauti kutoka kwa wazazi wao. Hali hizi huamua masharti ambayo mtu anafikisha umri wa kubaleghe na kukua inawakilisha awamu ya pili muhimu ya maisha ya mtu. Inajulikana kwamba, watu hawana chaguo katika awamu hii, vilevile. Hii pia imepangwa, ilipangwa kabla.

1. Hali Ambazo Mtu Hukulia Ndani Zimepangwa na Muumba

Kukua: Awamu ya Pili

Mtu hawezi kuchagua watu, matukio au vitu anavyoadilishwa na kushawishiwa navyo anapokua. Mtu hawezi kuchagua ni maarifa au mbinu gani atapata, ni mazoea gani ataishia kuwa nayo. Mtu hana kauli kuhusiana na wazazi na watu wake wa ukoo, aina ya mazingira ambayo atakulia ndani; mahusiano yake na watu, matukio, na mambo yaliyo katika mazingira yake na namna yanavyoathiri maendeleo yake, vyote ni zaidi ya udhibiti wake. Ni nani anayeamua mambo haya, basi? Ni nani anayeyapangilia? Kwa sababu watu hawana chaguo katika suala hili, kwa vile hawawezi kuamua mambo haya wao wenyewe, na kwa sababu bila shaka hayajipangi yenyewe kwa kawaida, ni wazi kabisa kwamba kuundwa kwa watu, matukio na vitu hivi vyote kunategemea mikono ya Muumba. Bila shaka, kama vile tu Muumba anavyopanga hali fulani za kuzaliwa kwa kila mtu, Yeye hupangilia pia hali mahususi ambazo mtu hukulia. Kama kuzaliwa kwa mtu kutaleta mabadiliko kwa watu, kwa matukio, na mambo yanayomzunguka yeye, basi kukua na maendeleo ya mtu huyo vyote vitaweza kuwaathiri vilevile. Kwa mfano, baadhi ya watu wanazaliwa katika familia fukara, lakini wanalelewa wakiwa wamezungukwa na utajiri; wengine wanazaliwa katika familia tajiri lakini husababisha utajiri wa familia zao kupungua, kiasi cha kwamba wanalelewa katika mazingira ya kimaskini. Hakuna kuzaliwa kwa yeyote kunatawaliwa na kanuni isiyobadilika, na hakuna anayelelewa katika hali zisizozuilika, na zisizobadilika. Haya si mambo ambayo binadamu anaweza kufikiria au kudhibiti; mambo haya yote ni mazao ya hatima ya mtu, na yanaamuliwa na hatima ya mtu. Bila shaka, kimsingi ni kwamba yote haya yaliamuliwa kabla katika hatima ya mtu na Muumba, yanaamuliwa na ukuu wa Muumba juu ya, na mipango Yake ya, hatima ya mtu huyu.

2. Hali Mbalimbali Ambazo Watu Hukulia Ndani Husababisha Wajibu Tofauti

Hali za kuzaliwa kwa mtu huanzisha katika kiwango cha kimsingi mazingira na hali ambazo hukulia ndani, na hali ambazo mtu hukulia ndani vilevile ni zao la hali za kuzaliwa kwake. Kwenye wakati huu mtu anaanza kujifunza lugha, na akili za mtu zinaanza kukumbana na kuchanganua mambo mengi mapya, na katika mchakato huu mtu anakua bila kusita. Mambo ambayo mtu anasikia kwa masikio yake, anaona kwa macho yake, na anang’amua kwa akili zake huboresha na kuhuisha kwa utaratibu ulimwengu wa ndani wa mtu. Watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo, maarifa ya kawaida, maarifa, na mbinu anazojifunza, na njia za kufikiria ambazo mtu anaathiriwa nazo, anaambiwa au kufunzwa, vyote vitamwongoza na kuathiri hatima ya maisha yake. Lugha anayojifunza mtu anapokua na njia yake ya kufikiria haviwezi kutenganishwa kutoka kwenye mazingira ambayo yeye analelewa katika ujana wake, na hayo mazingira yana wazazi, ndugu zake, na watu wengine, matukio, na mambo yanayomzunguka. Kwa hivyo mkondo wa maendeleo ya mtu unaamuliwa na mazingira ambayo yeye anakulia ndani, na pia unategemea watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo kwenye kipindi hiki cha muda. Kwa sababu masharti ambayo mtu hukulia ndani yaliamuliwa kabla na tena mapema mno, mazingira anayoishi kwenye mchakato huu pia, kwa kawaida, yaliamuliwa kabla. Hayaamuliwi na chaguo na mapendeleo ya mtu, lakini yanaamuliwa kulingana na mipango ya Muumba, yanaamuliwa na mipangilio makinifu ya Muumba, na ukuu wa Muumba juu ya hatima ya mtu huyo katika maisha. Kwa hivyo watu ambao mtu yeyote hukumbana nao katika mkondo wa kukua, na mambo ambayo mtu hukutana nayo, vyote vimeunganishwa bila kuzuilika kwa mipango na mipangilio ya Muumba. Watu hawawezi kutabiri aina hizi za mahusiano mapevu, wala hawawezi kuyadhibiti au kuweza kuyaelewa. Mambo mengi tofauti na watu wengi tofauti wanao mwelekeo wa mazingira ambayo mtu hukulia, na hakuna binadamu anaweza kupangilia na kupanga mtandao mpana kama huo wa muunganisho. Hakuna mtu au kitu isipokuwa Muumba anaweza kudhibiti kujitokeza, kuwepo, na kutoweka kwa watu mbalimbali, matukio na mambo, na ni mtandao mpana ajabu wa muunganisho unaounda maendeleo ya mtu kama ilivyoamuliwa kabla na Muumba, na kuunda mazingira tofauti ambayo watu wanakulia ndani, na kuunda wajibu mbalimbali unaohitajika kwa minajili ya kazi ya Muumba ya usimamizi, kuweka misingi thabiti, yenye nguvu ili watu waweze kukamilisha kwa ufanisi kazi yao maalum.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Iliyotangulia: Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza
Inayofuata: Uhuru: Awamu ya Tatu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Uhuru: Awamu ya Tatu

Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye...

Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza

Mahali ambapo mtu amezaliwa, ni familia gani alimozaliwa, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa—haya ndiyo maelezo ya awamu ya...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp