Mabadiliko ya tabia hudhihirishwaje?

13/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Ikiwa tabia yako inaweza kubadilika au la inategemea na ikiwa unaweza kuendelea na maneno halisi ya Roho Mtakatifu au la na una ufahamu wa kweli. Hili ni tofauti na kile mlichoelewa awali. Kile ulichoelewa kuhusu mabadiliko katika tabia awali kilikuwa kwamba wewe, ambaye ni rahisi kuhukumu, kupitia kwa kufundishwa nidhamu na Mungu huzungumzi ovyo ovyo tena. Lakini hii ni hali moja tu ya mabadiliko, na hivi sasa suala muhimu zaidi ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Unafuata chochote asemacho Mungu; unatii chochote asemacho Yeye. Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari. Mabadiliko katika tabia yalipozungumziwa hapo awali, imekuwa hasa kuhusu kujinyima mwenyewe, kuruhusu mwili kuteseka, kufunza nidhamu mwili wa mtu, na kujiondolea mapendeleo ya mwili—hii ni aina moja ya mabadiliko katika tabia. Watu sasa wanajua kwamba maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia ni kutii maneno halisi ya Mungu na vilevile kuweza kuwa na ufahamu halisi wa kazi Yake mpya. Kwa njia hii, ufahamu wa awali wa watu kumhusu Mungu, ambao ulipotoshwa na fikira zao wenyewe, na kutimiza ufahamu wa kweli wa na utiifu Kwake. Hii tu ndio maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa wako na ukweli. Bidii ya watu inaweza tu kuwafanya wazingatie mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida halisi, na mafundisho hayawezi kushikilia nafasi ya ukweli. Wana ukweli ndani yao, wanatambua masuala yote, wanajua jinsi ya kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kutenda kulingana na kanuni za ukweli, jinsi ya kutenda ili kumridhisha Mungu, nao wanaelewa asili ya upotovu wanaoufichua. Mawazo na dhana zao wenyewe vinapofichuliwa, wanaweza kutambua na kuunyima mwili. Hivi ndivyo mabadiliko katika tabia yanavyoonyeshwa. Kitu cha muhimu kuhusu mabadiliko katika tabia ni kwamba yana ukweli na uwazi, na unapotekeleza mambo, yanauweka ukweli katika matendo kwa usahihi wa karibu na upotovu wao hauonekani mara nyingi. Kwa jumla, mtu ambaye tabia yake imebadilika huonekana kuwa na busara na mwenye utambuzi, na kutokana na kuelewa kwake kwa ukweli, kujidai na kiburi havifichuliwi sana. Anaweza kuona kila kitu kwa uwazi, basi hawi mwenye kiburi baada ya kupata uwazi huu. Anaweza kuwa na ufahamu wa taratibu kuhusu ni ipi nafasi ya mwanadamu, jinsi ya kutenda kwa busara, jinsi ya kuwa mtiifu, nini anachofaa kusema na nini asichofaa kusema, na nini cha kusema na nini cha kutenda kwa watu gani. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa watu wa aina hii ni wenye busara kiasi. Wale ambao wana mabadiliko katika tabia zao wanaishi kwa kudhihirisha sura ya binadamu kwa kweli, nao wana0 ukweli; hawategemei ushawishi wa wengine. Wale ambao wamekuwa na mabadiliko katika tabia wako imara zaidi, hawasitasiti, na haijalishi wako katika hali gani, wanajua jinsi ya kutimiza wajibu wao sawasawa na jinsi ya kufanya mambo ili kumridhisha Mungu. Wale ambao tabia zao zimebadilika hawalengi nini cha kufanya ili kujifanya waonekane wazuri katika kiwango cha juujuu—wanao uwazi wa ndani kuhusu kile cha kufanya ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo, kutoka nje wanaweza kukosa kuonekana wenye shauku sana ama kama wamefanya jambo lolote kubwa, lakini kila kitu wanachofanya kina maana, kina thamani, na kina matokeo ya kiutendaji. Wale ambao tabia zao zimebadilika wana uhakika kuwa na ukweli mwingi—hii inaweza kuthibitishwa kwa mitazamo yao kuhusu mambo na kanuni zao katika vitendo vyao. Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko yoyote katika tabia hata kidogo. Mabadiliko katika tabia haimaanishi kuwa na ubinadamu uliokomaa au wenye uzoefu. Kwa kiasi kikubwa, inahusu matukio ambapo baadhi ya sumu za kishetani katika asili ya watu zinabadilika kama matokeo ya kufikia maarifa kuhusu Mungu na ufahamu wa ukweli. Hiyo ni kusema, sumu hizo zinatakaswa, na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unaanza kustawi ndani ya watu hawa, unakuwa maisha yake, nao unakuwa msingi wa kuwepo kwake. Hapo tu ndipo wanakuwa watu wapya, na hivyo tabia yao inabadilika. Mabadiliko katika tabia hayamaanishi kwamba tabia za nje za watu ni za upole kuliko hapo awali, kuwa walikuwa na kiburi awali wanazungumza kwa busara, au kwamba hawakuwa wanamsikiza mtu yeyote lakini sasa wanaweza kuwasikiza wengine; mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko katika tabia. Bila shaka, mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yao ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yao hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mitazamo yao imebadilika kabisa, na hakuna kati ya hiyo inakubaliana na ile ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.

Kimetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Mabadiliko katika tabia yana sifa bainifu. Yaani, kuweza kukubali kile ambacho ni sahihi na kinacholingana na ukweli. Haijalishi ni nani anayekupa mapendekezo—awe ni kijana au mzee, iwe mnashirikiana vizuri, na iwe uhusiano kati yenu ni mzuri ama mbaya—alimradi anasema kitu kilicho sahihi na kinacholingana na ukweli, na chenye manufaa kwa kazi ya familia ya Mungu, basi unaweza kukisikiza, ukichukue na kukikubali, na usiathiriwe na mambo mengine yoyote. Hiki ndicho kipengele cha kwanza cha sifa hiyo bainifu. Kwanza unaweza kukubali ukweli, na pia vitu ambavyo ni sahihi na vinalingana na ukweli. Kingine ni kuweza kutafuta ukweli wakati wowote unapokumbana na shida. Huwezi tu kukubali ukweli; lazima uweze kuutafuta. Kwa mfano, ukikumbana na shida mpya ambayo hakuna mtu anaweza kuielewa, unaweza kutafuta ukweli, uone ni nini unachopaswa kutenda ama kufanya ili kufanya jambo hilo lilingane na kanuni za ukweli, na kinatosheleza mahitaji ya Mungu. Kipengele kingine ni kupata uwezo wa kufikiria mapenzi ya Mungu. Unapaswaje kufikiria mapenzi Yake? Hili linategemea ni wajibu upi unatimiza na ni mahitaji yapi ambayo Mungu anayo kwako katika wajibu wako. Lazima uelewe kanuni hii. Tekeleza wajibu wako kulingana na kile ambacho Mungu anahitaji, na kitekeleze ili kumridhisha Mungu. Lazima pia uelewe mapenzi ya Mungu, na matokeo yanayofaa ya wajibu yako ni yapi, na lazima uweze kutenda kwa uwajibikaji na uaminifu. Yote haya ni njia ya kufikiria mapenzi ya Mungu. Kama hujui jinsi ya kufikiria mapenzi ya Mungu katika jambo unalotenda, lazima ufanye utafutaji fulani ili kukamilisha hilo, na kumridhisha Yeye. Ikiwa mnaweza kuweka kanuni hizi tatu katika vitendo, mpime njia ambayo kwa kweli mnaishi kulingana nazo, na kupata njia ya kutenda, basi mtakuwa mnayashughulikia mambo kwa njia yenye maadili. Bila kujali unalokabiliana nalo na bila kujali ni shida gani unazoshughulikia, lazima utafute ni kanuni gani unazopaswa kutenda kulingana nazo, ni maelezo gani yanayohusisha kila moja ya hizi, na jinsi zinavyopaswa kutendwa ili usiwe unakiuka hizi kanuni. Mara utakapokuwa na ufahamu dhahiri wa vitu hivi, utaweza kutenda ukweli kwa urahisi.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kuweka Ukweli Katika Vitendo Tu Ndipo Unaweza Kutupa Minyororo ya Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp