Kipengele kimoja cha kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi kilikuwa ni kutusamehe na kutuondolea dhambi zetu, wakati kile kipengele kingine kilikuwa ni kutupa amani na furaha na neema nyingi. Hili linatuwezesha kuona kwamba Mungu ni Mungu mwenye huruma na mwenye upendo. Lakini unashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu hufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, kwamba Yeye huonyesha ukweli na humhukumu na kumwadibu mwanadamu, humpogoa na kumshuhgulikia mwanadamu, humfichua mwanadamu na kuziondosha kila aina ya watu waovu, pepo wabaya na wapinga Kristo, jambo linalowaruhusu watu kuona kwamba tabia ya haki ya Mungu haivumilii kosa lolote. Kwa nini tabia iliyofichuliwa katika kazi ya Bwana Yesu ni tofauti kabisa na tabia iliyofichuliwa katika kazi ya Mwenyezi Mungu? Ni vipi hasa tunafaa kuielewa tabia ya Mungu?

08/06/2019

Jibu:

Tangu Bwana Yesu alipofanya kazi Yake ya ukombozi katika Enzi ya Neema, tumeona kwamba Yeye ni mwingi wa stahamala na uvumilivu, mwingi wa upendo na huruma. Ilimradi tumwamini Bwana Yesu, dhambi zetu zitasamehewa na tutaweza kufurahia neema ya Mungu. Kutokana na hilo, tumepambanua kwamba Mungu ni Mungu mwenye upendo na mwenye rehema, kwamba Yeye ni mwenye huruma kwa mwanadamu na humsamehe mwanadamu dhambi zake zote milele, na kwamba siku zote Mungu hututendea kama mama anavyowatendea watoto wake, kwa kujali sana, asionyeshe hasira kamwe. Kwa hivyo, watu wengi huchanganyikiwa wanapomwona Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho akionyesha ukweli na kumhukumu mwanadamu kwa lugha kali ambayo hufichua waziwazi upotovu wa mwanadamu bila huruma yoyote; hawaelewi Anapowahukumu na kuwalaani watu waovu, wapinga Kristo na Mafarisayo. Wanahisi kwamba Mungu hapaswi kutumia lugha kali kama hiyo kumhukumu mwanadamu. Ukweli kwamba tuna uwezo wa kuhodhi aina hizi za mawazo ni kutokana na kukosa maarifa kuhusu tabia ya asili ya Mungu kabisa. Tabia yoyote ambayo Mungu hufichua katika kila enzi daima hutegemea mahitaji ya kazi Yake ya kuiokoa jamii ya wanadamu, na pia huamuliwa na mahitaji ya binadamu waliopotoka. Yote ni kwa ajili ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu. Ikiwa tunataka kuelewa kipengele hiki cha ukweli na kupata maarifa ya kweli kuhusu tabia ya Mungu, basi hebu tusome vifungu vichache kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu akasema, “Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi).

Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Wokovu uliopewa leo unatokea wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu ya Kumletea Mwanadamu Wokovu).

Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitatengashwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wao mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa enzi, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kutompitisha mwanadamu katika hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki: basi usimamizi wa Mungu ungetamatishwa lini? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kumtenganisha mwanadamu kulingana na aina yake na kumleta mwanadamu katika ufalme mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Baada ya kusoma maneno haya kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tunaweza kuona nini kuhusu tabia ya Mungu iliyofichuliwa katika Enzi ya Neema? Je, Mungu hufichua tabia ipi katika Enzi ya Ufalme? Je, tabia za Mungu kama zilivyofichuliwa katika Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme ni sawa? Katika Enzi ya Neema ndipo Mungu alifanya kazi Yake ya ukombozi, ambapo Alifichua huruma na upendo Wake, ustahimilivu na uvumilivu Wake, pamoja na msamaha Wake na ghofira Yake. Ilikuwa tu kwa njia hii ambapo wanadamu walipata sifa za kustahili kuja mbele za Mungu na kuomba, kukiri dhambi zao na kumsihi Mungu. Baada ya kupata msamaha wa Mungu, waliweza kufurahia neema na baraka za Mungu. Mwishoni mwa kipindi cha Enzi ya Sheria, licha ya wanadamu kujua dhambi ilikuwa nini na kujua kwamba sheria za Yehova Mungu hazingevumilia kosa lolote kutoka kwa wanadamu, hata hivyo wanadamu mara nyingi walitenda kinyume cha sheria hizi na kumkosea Mungu. Kwa mujibu wa kile ambacho sheria na amri zilihitaji kutoka kwa wanadamu, wote walipaswa kuuawa kulingana na sheria. Ndiyo maana Mungu alikuwa mwili na akasulubiwa kwa ajili ya wanadamu katika Enzi ya Neema; Yeye mwenyewe alizibeba dhambi za binadamu, Akiwaondolea na kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Bwana Yesu aliwatendea wafuasi Wake kama ambavyo mama na baba wangewatendea wana na binti zao wenyewe: kwa uangalifu mkubwa na kutotaka kumtelekeza mtu yeyote aliyemwamini au kumfuata. Bwana Yesu kufichua rehema, upendo, msamaha, na kuondoa dhambi Kwake ilikuwa ili tuweze kuona jinsi upendo wa Mungu ulivyo wa kweli kwetu, jinsi ambavyo moyo wa Mungu ulivyo na huruma na ulivyo mkarimu, na jinsi Alivyo na huruma kwa udhaifu wetu. Upendo Wake ulibadili mioyo yetu. Ni kwa njia hiyo pekee ndiyo tukawa tayari kumkubali Mungu, kuja mbele Zake kutubu dhambi zetu, na kupata ukombozi wa Mungu. Je, si sote tumehisi huruma na upendo huu kutoka kwa Mungu? Sasa kwa kuwa siku za mwisho zimefika, wanadamu tayari wanajua kuhusu kuwepo kwa Mungu na wamefurahi sana neema kubwa ya Mungu. Wote wanaweza kuwa na hakika kwamba Mungu anawakomboa na kuwaokoa wanadamu. Wakati huu watu wanaweza kukubali ukweli fulani—wakati umefika wa Mungu kufanya kazi Yake ya hukumu ili mwanadamu aweze kusafishwa na kuokolewa kikamilifu. Kwa kuwa wanadamu wa siku za mwisho wametiwa doa kabisa na upotovu wa Shetani, wao ni wenye kiburi sana na wapotovu, wenye ubinafsi na wenye kustahili kudharauliwa, na waovu na wenye tamaa sana. Watafanya lolote wawezalo kwa ajili ya sifa, hadhi, na mali. Wamepoteza dhamiri na mantiki yote, hawana ubinadamu hata kidogo, na hata ingawa wanamwamini Bwana na wamesamehewa dhambi zao, asili yao ya dhambi na tabia ya kishetani bado vinasalia. Hii ndiyo sababu wanadamu wote hawawezi kujinasua katika kuishi katika dhambi. Ili kuwaokoa binadamu kabisa kutokana na maovu ya dhambi, Mungu amekuwa mwili kama Mwana wa Adamu katika siku za mwisho kwa mujibu wa mahitaji ya wanadamu wapotovu; Ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Mungu ametekeleza hatua ya kazi ya hukumu na kuadibu, na wakati ambapo Atatoa ukweli ili kumhukumu mwanadamu, maneno Yake yatakuwa makali kidogo na yatachoma sana moyoni, kama tu upanga mkali ukatao kuwili, Akifichua kikamilifu tabia Yake ya haki, heshima na yenye hasira. Hasa ni kwa sababu ya hukumu na kuadibu kwa Mungu ndiyo tunaweza kuona kwamba haki na utakatifu Wake hautavumilia makosa ya wanadamu, na wakati huo pekee ndipo tutajiangusha chini na hatutakuwa na mahali popote pa kujificha. Kisha tunatambua kwamba tumepotoshwa sana na tumejawa kabisa na tabia ya Shetani, kwamba tumekosa kabisa uchaji na utiifu kwa Mungu, tunachofanya tu ni kuasi na kwenda kinyume Chake, na kwamba hatustahili kuwa mbele za Mungu. Ni kwa njia hii tu ndipo tunafanikisha toba ya kweli na tunakuja kujua mfano wa kweli wa binadamu ni upi, na jinsi mtu anavyopaswa kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, tunaweza kuelewa ukweli mwingi, kukuza moyo wa uchaji na utiifu kwa Mungu, kujua umuhimu wa kufuatilia ukweli na vile vile umuhimu wa msingi wa kumjua na kumpenda Mungu; je, si hii ni toba ya kweli? Je, si haya ni mabadiliko halisi? Bila hukumu na kuadibu kwa Mungu, wanadamu kama hawa waliopotoka sana wasingekuwa na njia yoyote ya kutakaswa na kupata wokovu.

Tunaona sasa kwamba matokeo ya Mungu kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu yanaweza kupatikana tu kwa njia ya hukumu na kuadibu Kwake. Huu ni ukweli. Ikiwa mambo yangeendelea kulingana na vile tunavyofikiria, Mungu katika siku za mwisho Angeifichua tabia ile ile ya upendo na rehema kama ya Bwana Yesu—je, hiyo ingefanikisha matokeo ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu? Mungu asingetekeleza kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho basi kamwe tusingeelewa kikamilifu tabia ya Mungu ambayo inategemea haki Yake. Kisha tusingeweza kupokea ukweli, kufikia utakaso au wokovu, au kukamilishwa. Aidha, kusingekuwa na njia ya kuwafunua na kuwaondoa wale makafiri ambao hawaufuatilii ukweli au wale wapinga Kristo ambao wanauchukia ukweli na ni maadui wa Mungu. Hukumu ya haki ya Mungu pekee ndiyo inayoweza kumfunua mtu kabisa na kumwainisha kila mtu kulingana na aina yake. Hii pekee ndiyo inaweza kumaliza kikamilifu kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Kupitia kulisoma neno la Mwenyezi Mungu tunaweza kujua kwamba tabia ambayo Mungu huonyesha katika kila hatua huamuliwa kulingana na mahitaji ya kazi ya kuwaokoa wanadamu. Kwa hiyo, hatuwezi kuiwekea mipaka tabia ya Mungu na ukamilifu Wake kulingana na tabia anayofichua katika enzi yoyote moja. Ni kwa sababu Mafarisayo waliliwekea mipaka jina la Mungu na kuzishika kanuni kiasi kwamba walimkataa na kumhukumu Bwana Yesu, ikisababisha wao kuadhibiwa na kulaaniwa na Mungu. Lazima tuijue tabia ya Mungu kwa kuja kuzielewa hatua Zake tatu za kazi. Hii ndiyo njia pekee iliyo sahihi ya kufanya hivyo, na hii inapatana na mapenzi ya Mungu. Ikiwa tungefikia uamuzi kuwa Mungu ni mwenye upendo na mwenye rehema kwa msingi tu wa tabia iliyofunuliwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, hii yangewezaje kuwa maarifa ya kweli kumhusu Mungu? Hiyo ingekuwa njia pumbavu na ya kijinga ya kumjua Mungu. Mafarisayo wote waliielewa Biblia, lakini kwa nini hawamkujua Mungu? Ilikuwa kwa sababu walimfafanua Mungu kwa kutegemea tu hatua moja ya kazi Yake, kwa hivyo Bwana Yesu alipokuja kuitekeleza kazi Yake walimsulubisha msalabani. Hii inaonyesha jinsi ilivyo rahisi kumwekea Mungu mipaka na kumpinga ikiwa hatumjui.

Kimetoholewa Kutoka Katika Majibu ya Mswada wa Filamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp