Kwa nini Mungu atawaweka wale wanaokataa kumkubali Mwenyezi Mungu katika maafa?

13/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Wale wote ambao Nawapenda wataishi milele kwa hakika, na wale wote wanaosimama dhidi Yangu wataadhibiwa na Mimi milele kwa hakika. Kwani Mimi ni Mungu mwenye wivu, Sitawasamehe kwa urahisi wanadamu kwa kile watakachokuwa wametenda. Nitaiangalia dunia yote, na, Nikitokea Mashariki ya dunia na haki, adhama, ghadhabu, na kuadibu, Nitajionyesha binafsi kwa wanadamu wengi wa tabaka mbalimbali!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26

Ninaamua hatima ya kila mtu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anataka huruma, bali kulingana na ikiwa anao ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili. Sharti mtambue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa pia. Huu ni ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu. …

Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Katika rekodi hii ya hadithi ya Nuhu, mnaona sehemu ya tabia ya Mungu? Kunacho mpaka kwa subira ya Mungu kwa upotovu, uchafu, na vurugu la binadamu. Anapofikia ule mpaka, Hatawahi tena kuwa na subira na badala yake Ataanza usimamizi Wake mpya na mpango mpya, kuanza kufanya kile ambacho lazima Afanye, kufichua matendo Yake na upande ule mwingine wa tabia Yake. Kitendo hiki Chake si cha kuonyesha kwamba lazima Asiwahi kukosewa na binadamu au kwamba Yeye amejaa mamlaka na hasira, na wala si kuonyesha kwamba Anaweza kuangamiza binadamu. Ni kwamba tabia Yake na kiini chake takatifu ambacho hakiwezi tena kuruhusu, hakina tena subira kwa aina hii ya binadamu kuishi mbele Yake, kuishi chini ya utawala Wake. Hivyo ni kusema, wakati wanadamu wote wako dhidi Yake, wakati hakuna mtu yeyote Anayeweza kuokoa katika ulimwengu mzima, Hatakuwa tena na subira kwa binadamu kama hawa, na Ataweza, bila ya utundu wowote, kutekeleza mpango Wake—kuangamiza binadamu wa aina hii. Kitendo kama hicho cha Mungu kinaamuliwa na tabia Yake. Hii ni athari inayohitajika, na athari ambayo kila kiumbe aliyeumbwa chini ya utawala wa Mungu lazima ashuhudie.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Katika awamu za kazi ya Mungu, njia ya wokovu bado inachukua mtindo wa majanga tofauti, na hakuna yeyote ambaye amepotea anaweza kuyaepuka Ni mwisho tu ndio hali ya “kutulia kama mbingu ya tatu: Hapa viumbe vilivyo hai vikubwa na vidogo vinaishi pamoja kwa amani, bila kushiriki katika ‘migogoro ya mdomo na ulimi hata mara moja’” kuwa na uwezo wa kuonekana duniani. Hali moja ya kazi ya Mungu ni kuwashinda wanadamu wote na kuwapata watu waliochaguliwa kupitia kwa maneno Yake. Hali nyingine ni kuwashinda wana wote wa uasi kupitia kwa maafa mbalimbali. Hii ni sehemu moja ya kazi kubwa ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio ufalme ulio hapa duniani ambao Mungu anataka unaweza kutimizwa kwa ukamilifu, na hii ni sehemu ya kazi ya Mungu ambayo ni kama dhahabu nzuri.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 17

Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za maafa” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

Katika hatua hii ya kazi, kwa vile Mungu anataka kufichua matendo Yake yote kotekote katika dunia ili wanadamu wote ambao wamemsaliti watakuja tena kuinama kwa utiifu mbele ya kiti Chake cha enzi, hivi ndani ya hukumu ya Mungu bado kuna huruma na upendo wa Mungu. Mungu hutumia matukio ya sasa kotekote ulimwenguni kutetemesha mioyo ya wanadamu, Akiiamsha kumtafuta Mungu ili waweze kumiminika kwenda Kwake. Hivyo Mungu asema, “Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 10

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp