Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

12/06/2019

Maneno Husika ya Mungu:

Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri kwa na namna hii: Naweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu anasema ni vizuri na kunipa hongera, hivyo inahesabika kama kuelewa neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza nia ya neno la Mungu na kile ambacho yatafanikisha hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo ya madoido ya maandishi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyoweza kueleza maandishi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu—ni bure!

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Mmekengeuka katika kufanya kwenu muhtasari wa ukweli; baada ya kufanya muhtasari wote huu, matokeo yamekuwa tu sheria. Kutoa kwenu “muhtasari kuhusu ukweli” hakufanywi ili watu wapate maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunawafanya watu wawe weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka katika ukweli. Wao huonekana kuelewa lengo la kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno na mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli; si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na kisha unamiliki kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini ni nini kinachofanyika unapomaliza kunena? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu, wala hawajifahamu. Mwishowe, yote ambayo watakuwa wamepata ni virai na kanuni, na wanaweza kuzungumza juu ya mambo hayo machache pekee. Mungu angefanya jambo jipya, je, ungeweza kulinganisha mafundisho yote unayojua na hilo? Hayo mambo yako ni kanuni tu na wewe unawafanya watu wajifunze theolojia tu, kutowaruhusu kupitia neno la Mungu au ukweli. Kwa hivyo, vitabu hivyo ambavyo mnakusanya vinaweza kuwaleta wengine katika theolojia na maarifa tu, katika virai vipya na katika kanuni na mila mpya. Haviwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu au kuwaruhusu kuuelewa ukweli au mapenzi ya Mungu. Unafikiria kwamba kwa kuuliza maswali hayo moja baada ya lingine, ambayo kisha unayajibu na ambayo unayaandikia maelezo, tabia ya aina hiyo itawafanya ndugu zako kuyaelewa. Unafikiri kwamba mbali na kuwa rahisi kukumbuka, masuala haya ni wazi mara moja, na kwamba hii ni njia nzuri sana ya kufanya vitu. Lakini kile wanachokielewa siyo maana halisi iliyokusudiwa ya ukweli na hakilingani na uhalisi—ni maneno na mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Kufanya hivi ni kuwaongoza watu kuelewa na kuwa weledi wa maarifa. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, huko si kuwa sawa tu na Paulo?

Kimetoholewa kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu. Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Mkitenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa la utendaji kwenu; usipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwako ni hekaya ya mbinguni ya tatu tu. …

… Kuelewa neno la Mungu kwa kweli hutokea unapoweka ukweli katika vitendo, na ni lazima uelewe kwamba “ni kwa kutenda ukweli tu ndipo unaweza kueleweka.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema kwamba unalielewa. Wengine husema kwamba njia ya pekee ya kutenda ukweli ni kuuelewa kwanza, lakini hii ni sahihi kwa kiwango fulani tu, na hakika si sahihi kikamilifu. Kabla uwe na maarifa ya ukweli fulani, hujapitia ukweli huo. Kuhisi kwamba unaelewa kitu unachosikia katika mahubiri si kuelewa kwa kweli—huku ni kuwa na maneno halisi ya ukweli tu, na si sawa na kuelewa maana ya kweli ndani yake. Kuwa tu na maarifa ya juujuu ya ukweli hakumaanishi kwamba kweli unauelewa ama una maarifa yoyote kuuhusu; maana ya kweli ya ukweli hutokana na kuupitia. Kwa hiyo, ni wakati tu unapopitia ukweli ndiyo unaweza kuuelewa, na ni hapo tu ndiyo unaweza kufahamu sehemu zake zilizofichika. Kukuza uzoefu wako ndiyo njia ya pekee ya kuelewa vidokezo, na kuelewa asili ya ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa vitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Hawa ni watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na hawaelewi mambo ya kiroho. Haijalishi aina ya maarifa unayoonyesha, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikira.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Chochote ambacho hakijatoka kwa uzoefu wako mwenyewe, iwe umejifunza kutoka kwa vitabu au kutoka kwa uzoefu wa watu wengine, kinakuwa mafundisho kwako. Unapokipitia, na unafikia matokeo kutoka kwa uzoefu wako, basi utapata ufahamu wa kweli, na maneno unayoyasema unapotoa ushirika yatakuwa halisi; ni hapo tu ndipo kinakuwa uhalisi wa kweli. Angalia jinsi wasioamini wanavyotafiti nadharia fulani: Wanatafiti kutoka kwa kile kilichoandikwa tu, wanatafiti mafundisho na kuyapima na kisha kufikia mahitimisho yao. Hasa wanateolojia na wachungaji, na vile vile wasomi na watafiti wa teolojia, baada ya kusoma fungu la maneno ya Mungu, hawatafuti ukweli au kutafuta ufahamu wa kweli wa Mungu kutoka kwa uzoefu wa utendaji. Badala yake, wanachunguza na kupima nadharia mbalimbali na hatimaye kufikia mahitimisho fulani. Kwa hiyo, mahitimisho ambayo wanafikia ni halisi au ya mafundisho ya dini? Yote ni mafundisho? Hii ni kwa sababu walifikia mahitimisho haya kwa msingi wa utafiti wa maandishi maalum na majadiliano, na sio kwa msingi wa uzoefu wao wenyewe. Mahitimisho yaliyofikiwa kutoka kwa utafiti wa maandishi halisi na kutoka kwa kutafiti vitu vilivyorekodiwa katika Biblia, yameunda nadharia ya aina moja, inayoitwa nadharia ya teolojia. Hakuna ufahamu kutoka kwa uzoefu katika hili, na hakuna nuru ya Roho Mtakatifu. Ufahamu wa kina kutoka kwa nuru ya Roho Mtakatifu unazidi ule unaotoka kwa maana ya juu juu ya maneno; hauwezi kuelezwa kwa lugha yoyote ya juu juu. Roho Mtakatifu atakupa nuru na mwangaza wakati tu utakapotafuta ukweli baada ya kuingia katika uzoefu. Vitu ambavyo Roho Mtakatifu huvipa nuru na kuviangaza kwa ajili yako ni vitu ambavyo ni halisi zaidi na vitu ambavyo ni vya ukweli zaidi kwako, na hivi ndivyo vitu ambavyo huwezi kuvipata kutoka katika Biblia bila kujali jinsi unavyoichunguza kwa bidii. Kwa hiyo leo, Mungu anatutaka tupitie neno la Mungu. Kama, katika uzoefu wetu wa neno la Mungu, Roho Mtakatifu anatupa nuru, basi tunaweza kufikia ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu. Ufahamu huu wa kweli hauwezi kufikiwa bila kujali jinsi unavyochunguza maana halisi ya maneno ya Mungu kwa bidii; hili ni jambo ambalo haliwezi kufikiwa na fikira za binadamu, na kitu ambacho huwezi kukiwazia, bila kujali unavyojaribu kwa bidii jinsi gani. Kwa hiyo, ni ukweli unaopokewa kutoka kwa uongozi, nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu pekee ndio ufahamu wa kweli wa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Tofauti kati ya maneno ya mafundisho na ukweli ni ipi hasa? Ukweli ni vitu halisi vya neno la Mungu; unawakilisha mapenzi ya Mungu. Maneno ya mafundisho ni ya kikundi cha vitu vya juu juu, na yanawakilisha mawazo na fikira za binadamu. Hayalingani na ukweli. Vitu halisi vya ukweli ni vya utendaji sana; ni vyenye maadili na vya kuridhisha hasa. Punde mtu anapoelewa kitu halisi, moyo wake unachangamka na kuachiliwa huru—hakabiliwi tena na shutuma za kanuni. Kwa upande mwingine, maneno ya mafundisho ni matupu na yasiyo ya kweli. Ni kanuni na mambo ya desturi tu, na huwafanya watu hasa wenye kuweza kuzuiwa na kutohisi huru. Aidha, bila kujali ni maneno mangapi ya mafundisho ambayo mtu anajua, hayawezi kuleta mabadiliko katika tabia yake ya maisha. Yana faida ndogo ya msingi kwa watu. Kwa hiyo, maneno ya mafundisho hayawezi kabisa kulingana na ukweli. Ukweli unaweza kuwa uzima wa mtu. Punde mtu anapokubali ukweli utaleta mabadiliko ya tabia ya maisha. Kuelewa kiwango kikubwa cha mafundisho kunaweza tu kumletea mtu majivuno, majigambo, kiburi na kumfanya akose busara. Ni wakati tu ambapo mtu ana ukweli kama uzima wake ndiyo utendaji wake unakuwa halisi. Bila kujali ni maneno mangapi ya mafundisho mtu anaelewa, hatakuwa na uhalisi. Anapokabiliwa na suala bado hatajua cha kutenda. Wale wote ambao wanakamilishwa na Mungu ni watu walio na ukweli, wakati wale wote ambao hawajapitia kukamilishwa na Mungu ni watu wa maneno ya mafundisho. Wale walio na ukweli wanafaa kwa matumizi na Mungu. Kazi yao huzaa matunda, na wanaweza kweli kuwaleta wengine mbele za Mungu. Wale wanaolenga maneno ya mafundisho hawapati matokeo ya kweli kutoka kwa kazi yao. Hawawezi kuwapa watu riziki ya uzoefu na ufahamu wa kweli, sembuse kutumia ukweli kutatua masuala. Hii ndiyo maana hawawezi kuwaleta wengine mbele za Mungu. Mtu ambaye ana ukweli hawahepi watu wanaotafuta ukweli, na anaweza kutatua shida zote za utendaji ambazo watu wako nazo katika imani yao. Wale ambao wanasisitiza maneno ya mafundisho wanaogopa watu kutafuta ukweli kwa sababu hawana vitu vya kweli ndani yao, na mafundisho wanayozungumzia hayawezi kutatua shida za kweli. Kwa hiyo, hawathubutu kuwaagiza wengine waulize maswali, na bila shaka hawawezi hata zaidi kutatua taabu za utendaji. Wale walio na ukweli wanathubutu kukabili uhalisi; wale wanaolenga maneno ya mafundisho hawathubutu kukabili uhalisi, badala yake, wanauepuka. Hizo ndizo kanuni za kutambua kati ya ukweli na maneno ya mafundisho.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp