Imeandikwa pale pale katika Biblia: “Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima(Waebrania 13:8). Kwa hiyo jina la Bwana halibadiliki kamwe! Lakini unasema kwamba wakati Bwana atakapokuja tena katika siku za mwisho atachukua jina jipya na ataitwa Mwenyezi Mungu. Unawezaje kulielezea?

08/06/2019

Jibu:

Biblia inasema, “Yesu Kristo ni yuyo huyo jana, na leo na daima” (Waebrania 13:8). Hii inarejelea ukweli kuwa tabia ya Mungu na kiini Chake ni za milele na hazibadiliki. Haimaanishi kuwa jina Lake halitabadilika. Hebu tuangalie maneno ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria kutobadilika kwa tabia ya Mungu na kiini Chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita? Wewe hujua tu kwamba Mungu habadiliki milele, lakini je, unajua kuwa Mungu ni mpya milele na kamwe si wa zamani? Kama kazi ya Mungu kamwe haikubadilika, basi Angeweza kulea mwanadamu hadi leo? Kama Mungu habadiliki, basi mbona Yeye tayari Amefanya kazi ya nyakati mbili? … maneno haya ‘Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani’ yanarejelea kazi yake, na maneno haya ‘Mungu habadiliki’ kinarejelea kile ambacho Mungu anacho na alicho kiasili. Bila kujali, huwezi kubaini kazi ya miaka elfu sita kwa mtazamo mmoja, ama kwa kuielezea tu kwa maneno ambayo hayabadiliki. Huo ni ujinga wa mwanadamu. Mungu si wazi kama mwanadamu anavyofikiria, na kazi yake haitasimama katika enzi moja. Yehova, kwa mfano, haliwezi daima kusimamia jina la Mungu; Mungu pia hufanya kazi yake kwa kutumia Jina la Yesu, ambayo ni ishara ya vile ambavyo kazi ya Mungu daima husonga kwenda mbele.

Mungu siku zote huwa Mungu, na kamwe Yeye hatakuwa Shetani; Shetani daima ni Shetani, na yeye hawezi kuwa Mungu. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, haki ya Mungu, na adhama ya Mungu kamwe hayatabadilika. Kiini chake na anachomiliki na kile Anacho na alicho kamwe hakitabadilika. Kazi yake, hata hivyo, daima inaendelea mbele, daima inaenda ndani zaidi, kwa kuwa Mungu daima ni mpya na kamwe si wa zamani. Katika kila enzi Mungu huchukua jina jipya, katika kila enzi anafanya kazi mpya, na katika kila enzi Yeye huwaruhusu viumbe Wake kuona mapenzi Yake mapya na tabia Yake mpya(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Tunaweza kuona kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu kuwa Mungu Mwenyewe habadiliki. Hii inarejelea tabia na kiini cha Mungu, sio jina Lake. Ingawa Mungu amefanya kazi tofauti na amechukua majina tofauti katika enzi mbalimbali kupitia mchakato Wake wa kumwokoa mwanadamu, kiini Chake hakiwezi kubadilika kamwe. Mungu Atabaki kuwa Mungu kila wakati. Hivyo, haijalishi iwapo jina Lake ni Yehova au Yesu, kiini Chake hakibadiliki kamwe. Kila wakati ni Mungu yule yule anayefanya kazi. Hata hivyo, wakati huo, Mafarisayo wa Wayahudi hawakujua kuwa jina la Mungu hubadilika pamoja na mabadiliko ya enzi, katika kazi Yake. Waliamini kuwa Yehova pekee ndiye angeweza kuwa Mungu wao, Mwokozi wao kwa sababu katika enzi zilizopita walikuwa wameshikilia kuwa Yehova pekee ndiye Mungu, na kuwa hakuna Mwokozi mwingine ila Yehova. Hivyo basi, Mungu alipobadilisha jina Lake na kuja kufanya kazi ya ukombozi akiwa na jina la “Yesu,” walimkemea na kumpinga Bwana Yesu kwa nguvu. Mwishowe, walimsulubisha msalabani, wakatenda kitendo cha ukatili kabisa, na kupata adhabu ya Mungu. Vivyo hivyo, kwa sababu sasa tuko katika siku za mwisho, tukikana kiini cha Mungu na kwamba hii ni kazi ya Mungu mmoja kwa sababu Amebadilisha kazi Yake na jina Lake, huo utakuwa ni ujinga na kukosa uangalifu kwa wanadamu. Kila jina ambalo Mungu amechukua katika kila enzi lina umuhimu mkubwa, na yote yana wokovu mkuu kwa mwanadamu.

Mungu ni mpya kila wakati, na kamwe hazeeki. Yeye ndiye Mungu anayejumuisha vitu vyote. Majina binafsi ya Mungu hayaweza kuonyesha ukamilifu Wake. Hivyo, kadri enzi zinapoendelea, majina Yake pia yanaendelea kubadilika. Mwenyezi Mungu anasema, “Jina la Yesu lilichukuliwa kuwa la kazi ya ukombozi, hivyo bado Yeye Anaweza kuitwa kwa jina moja wakati Atarudi katika siku za mwisho? Je, bado Yeye Atafanya kazi ya ukombozi? Ni kwa nini Yehova na Yesu ni kitu kimoja, ilhali wanaitwa kwa majina tofauti katika enzi hizi tofauti? Je, si kwa sababu enzi za kazi Yao ni tofauti? Jina moja linawezaje kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake? Kwa njia hii, lazima Mungu aitwe kwa jina tofauti katika enzi tofauti, lazima atumie jina kubadilisha enzi na kuwakilisha hiyo enzi, kwa kuwa hakuna jina moja linaweza kumwakilisha Mungu mwenyewe kikamilifu. Na kila jina linaweza tu kuwakilisha kipengele cha wakati cha tabia ya Mungu katika enzi fulani; yote linahitaji kufanya ni kuwakilisha kazi Yake. Kwa hivyo, Mungu Anaweza kuchagua jina lolote ambalo linafaa tabia yake kuwakilisha enzi nzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). “Je, Jina la Yesu—‘Mungu pamoja nasi,’—linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na yanazidi uwezo wa mwanadamu kumjua Yeye. Lugha ya mwanadamu haina uwezo wa kumfafanua Mungu kwa ukamilifu. … Neno au jina moja maalum halina uwezo wa kumwakilisha Mungu kwa ukamilifu wake. Kwa hivyo, je, Mungu Anaweza kuchukua jina moja lisilobadilika? Mungu ni mkuu sana na mtakatifu sana, kwa hivyo mbona wewe huwezi kumruhusu Yeye abadili jina Lake katika kila enzi mpya? Kwa hivyo, katika kila enzi ambayo Mungu binafsi hufanya kazi yake mwenyewe, Yeye hutumia jina ambalo linafaa enzi hiyo ili kujumlisha kazi ambayo anaifanya. Yeye hutumia hili jina haswa, ambalo linamiliki umuhimu wa wakati, kuwakilisha tabia yake katika enzi hiyo. Mungu hutumia lugha ya mwanadamu kuelezea tabia yake mwenyewe(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)). Mungu ni mwenye hekima, Mtawala mwenyezi. Yeye ni mkuu, mkarimu, na Anajumlisha yote. Jina moja pekee haliwezi kuwakilisha yote Mungu Alicho. Juu ya hayo, katika kila enzi Mungu amefanya tu sehemu ya kazi Yake, na Amefichua tu sehemu ya tabia Yake. Hajaonyesha yote Aliyo nayo na Alicho. Hivyo, katika kila hatua ya kazi Yake Yeye hutumia jina fulani ambalo lina umuhimu katika enzi hiyo ili kuonyesha kazi Yake katika enzi hiyo, na tabia Anayoonyesha. Hii ni kanuni ya kazi ya Mungu, na ndiyo sababu kuu ya kubadilisha jina Lake.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Jina la Mungu kila enzi haliwezi kuonyesha ukamilifu Wake, basi jina Lake lina umuhimu gani katika kila enzi? Swali hili ni la muhimu sana. Sasa, Mwenyezi Mungu ametupa jibu la swali hili. Mwenyezi Mungu anasema, “‘Yehova’ ni jina Nililolichukua wakati wa kazi Yangu kule Uyahudi, nalo linamaanisha Mungu wa Wayahudi (Wateule wa Mungu) Anayeweza kumhurumia mwanadamu, kumlaani mwanadamu, na kuyaongoza maisha ya mwanadamu. Linamaanisha Mungu anayemiliki nguvu kuu na Amejawa na hekima. ‘Yesu’ ni Imanueli, nalo linamaanisha sadaka ya dhambi iliyojawa na upendo, Amejawa na huruma, naye Anamkomboa mwanadamu. Alifanya kazi ya Enzi ya Neema, naye Anawakilisha Enzi ya Neema, na Anaweza tu kuwakilisha sehemu moja ya mpango wa usimamizi. Yaani, Yehova pekee ndiye Mungu wa watu wateule wa Uyahudi, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, Mungu wa Musa, na Mungu wa Wayahudi wote. Na hivyo, katika enzi ya sasa, Waisraeli wote, isipokuwa Wayahudi, wanamwabudu Yehova. Wanamtolea kafara kwa madhabahu, na kumtumikia wakiwa wamevalia mavazi ya kikuhani katika hekalu. Wanachotumainia ni kuonekana tena kwa Yehova. Yesu pekee ndiye Mkombozi wa wanadamu. Yeye ni sadaka ya dhambi ambayo ilimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi. Yaani, jina la Yesu lilitoka katika Enzi ya Neema, nalo lilikuwepo kwa ajili ya kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema. Jina la Yesu lilikuwepo ili kuwawezesha watu wa Enzi ya Neema kuzaliwa upya na kuokolewa, nalo ni jina mahsusi la wokovu wa binadamu wote. Kwa hiyo jina Yesu linawakilisha kazi ya ukombozi, nalo linaashiria Enzi ya Neema. Jina Yehova ni jina mahsusi la Wayahudi walioishi chini ya sheria. Katika kila enzi na kila hatua ya kazi, jina Langu haliko bila msingi, lakini lina umuhimu wakilishi: Kila jina linawakilisha enzi moja. ‘Yehova’ linawakilisha Enzi ya Sheria, nalo ni jina la heshima kwa Mungu aliyeabudiwa na Wayahudi. ‘Yesu’ linawakilisha Enzi ya Neema, nalo ni jina la Mungu wa wale wote waliokombolewa katika Enzi ya Neema. Iwapo mwanadamu bado anatamani kuwasili kwa Yesu Mwokozi katika siku za mwisho, na bado anamtarajia Afike katika mfano aliochukua kule Uyahudi, basi mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita ungekoma katika Enzi ya Ukombozi, nao usingeweza kuendelea zaidi. Siku za mwisho, hata zaidi, zisingeweza kufika, nayo enzi isingekomeshwa. Hiyo ni kwa sababu Yesu Mwokozi ni kwa ajili ya ukombozi na wokovu wa wanadamu peke yake. Nililichukua jina la Yesu kwa sababu ya watenda dhambi wote katika Enzi ya Neema, nalo si jina ambalo kwalo Nitawaangamiza wanadamu wote(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Kutoka kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, tumeelewa maana ya majina ya Mungu ambayo amechukua katika kila enzi. Katika Enzi ya Sheria, jina Lake lilikuwa Yehova, na jina hilo lilidhihirisha kile Alichoonyesha mwanadamu katika enzi hiyo: tabia ya adhama, hasira, laana, na huruma. Kisha, Mungu alianza kazi ya Enzi ya Sheria akiwa na jina la Yehova. Alipeana sheria na amri Zake na kuongoza rasmi mwanadamu mchanga katika maisha yake duniani. Aliwahitaji watu kufuata sheria kikamilifu na kujifunza kumwabudu Yeye, kumheshimu kama mkuu. Baraka na neema zilimfuata yeyote aliyetii sheria. Yeyote aliyevunja sheria alipigwa mawe hadi kufa, au kuchomwa na mioto ya mbinguni. Hiyo ndiyo maana Wayahudi walioishi chini ya sheria waliitii kwa ukamilifu, na walishikilia jina la Yehova kuwa takatifu. Waliishi chini ya jina la Yehova kwa miaka elfu kadhaa, hadi Enzi ya Sheria ikaisha. Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, kwa sababu wanadamu walikuwa wamezidi kuwa wapotovu zaidi na walikuwa wanatenda dhambi zaidi, hakukuwa na njia ya watu kuendelea kutii sheria. Kila mtu alikuwa katika hatari ya kila wakati ya kuadhibiwa kwa sababu ya kuvunja sheria, na ndio maana Mungu Alifanya kazi Yake ya ukombozi chini ya jina la Yesu. Alifungua Enzi ya Neema na kumaliza Enzi ya Sheria, akionyesha tabia ya Mungu ya upendo na huruma. Alimpa pia mwanadamu neema Yake ya ukarimu, na mwishowe alisulubiwa kwa ajili ya mwanadamu, hivyo kutokomboa kutoka kwa dhambi zetu. Kuanzia hapo, tumeanza kuomba kwa jina la Yesu na kulicha jina Lake kama takatifu, kufurahia msamaha wa dhambi zetu na utajiri wa neema Yake. Jina la “Yesu” lipo ndiposa watu wa Enzi ya Neema waweze kuzaliwa upya na kupata wokovu. Maana yake ni kuwa sadaka ya dhambi ya huruma na upendo kwa ukombozi wa mwanadamu. Jina “Yesu” linawakilisha kazi ya Mungu ya ukombozi, na linawakilisha pia tabia Yake ya huruma na upendo. Tunaweza kuona kutoka kwa hatua hizi mbili za kazi ambayo Mungu amekamilisha tayari kuwa jina Analochukua katika kila enzi lina umuhimu wake mahsusi. Kila jina linawakilisha kazi ya Mungu katika enzi hiyo na tabia Anayoonyesha katika enzi hiyo. Katika Enzi ya Neema, Bwana alipokuja, ikiwa hakuwa anaitwa Yesu, lakini aliitwa Yehova, basi kazi ya Mungu ingesimama katika Enzi ya Sheria, wanadamu wapotovu hawangewahi kupata ukombozi wa Mungu. Mwishowe, mwanadamu angelaaniwa na kuadhibiwa kwa kuvunja sheria, na wakati Mungu atapokuja katika siku za mwisho, kama Angekuwa bado anaitwa Yesu, wanadamu wapotovu wangepata tu ukombozi wa dhambi zao, lakini hawangewahi kamwe kutakaswa na kuokolewa ili kuingia katika ufalme wa Mungu. Hii ni kwa sababu tunasamehewa dhambi zetu kwa kumwamini Bwana Yesu, lakini asili yetu ya ndani yenye dhambi bado inaishi. Bado tunaendelea kutenda dhambi mara nyingi, kwa hivyo bado hatujapatwa na Mungu kabisa. Hivyo, ili kuokoa mwanadamu kabisa kutoka kwa dhambi, Mungu sasa anafanya hatua nyingine ya kazi yake ya kutakasa na kuokoa mwanadamu, kwa msingi wa kazi ya Bwana Yesu. Jina la Mungu ni lazima libadilike ipasavyo tena na kuwa Mwenyezi Mungu. Kuhusu Mungu kuitwa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, hili hakika lilitabiriwa zamani sana. Hebu tusome Ufunuo 1:8: “Mimi ndiye Alfa na Omega, Mwanzo na tena mwisho, Akasema Bwana, ambaye yuko, na ambaye alikuweko, na ambaye atakuja, Mwenyezi.” Na Ufunuo 11:16-17: “Na wao wazee ishirini na wanne, ambao waliketi katika viti vyao mbele ya Mungu, walianguka chini kifudifudi, na kumwabudu Mungu, wakisema, Tunakupa shukrani, Ee BWANA Mungu Mwenyezi, ambaye uko, na ulikuwa, utakuwa, kwa kuwa umeichukua nguvu yako kuu, na umetawala.” Hili lilitabiriwa pia katika Ufunuo 4:8, 16:7, 19:6 na vifungu vingine vingi katika Biblia. Jina jipya la Mungu katika siku za mwisho ni mwenye Uwezo, yaani, Mwenyezi Mungu.

Mungu ni Mungu mwenye hekima, na kila kitu Anachofanya kina umuhimu. Jina la Mwenyezi Mungu linawakilisha kazi yake kwa ukamilifu na tabia Anayoonyesha katika siku za mwisho. Bila Mungu kutufunulia mafumbo haya yeye binafsi, haijalishi ni miaka ngapi tutatumia kusoma Biblia, hatuwezi kujua mambo haya. Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu pamoja.

Mwenyezi Mungu anasema, “Kazi ya Mungu kokote katika usimamizi wake ni wazi kabisa: Enzi ya Neema ni Enzi ya Neema, na siku za mwisho ni siku za mwisho. Kuna tofauti baina ya kila enzi, kwa kuwa katika kila enzi Mungu Anafanya kazi ambayo inawakilisha enzi hiyo. Ili kazi ya siku za mwisho iweze kufanywa, lazima kuwe na kuungua, hukumu, kuadibu, ghadhabu, na uharibifu wa kuleta enzi kwenye kikomo. Siku za mwisho zinaashiria enzi ya mwisho. Wakati wa enzi ya mwisho, je, Mungu si Ataleta enzi kwenye kikomo? Na ni kwa njia tu ya kuadibu na hukumu ndio inaweza kuleta enzi kwenye kikomo. Ni kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kuitamatisha enzi hiyo. Madhumuni ya Yesu yalikuwa kwamba mwanadamu aweze kuendelea kuwepo, kuishi, na kuweza kuwepo kwa njia bora zaidi. Alimwokoa mwanadamu kutoka kwa dhambi ili mwanadamu akome upotovu wa kudumu na kamwe asiishi katika Kuzimu na jehanamu, na kwa kumwokoa mwanadamu kutoka kwa Kuzimu na jehanamu, Yesu alimwezesha mwanadamu kuendelea kuishi. Sasa, siku za mwisho zimewadia. Mungu atamwangamiza mwanadamu, Atamharibu mwanadamu kabisa, ambayo ina maana kuwa Atageuza uasi wa binadamu. Kwa hivyo, huruma ya Mungu na tabia yake ya hapo zamani ya kupenda haitakuwa na uwezo wa kuhitimisha enzi hiyo, na haitakuwa na uwezo wa kukamilisha usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita. Kila enzi inaonyesha uwakilishi maalum wa tabia ya Mungu, na kila enzi ina kazi ambayo inafaa kufanywa na Mungu. Kwa hivyo, kazi iliyofanywa na Mungu mwenyewe kwa kila enzi ina dhihirisho la tabia Yake ya ukweli, na jina Lake na kazi anaofanya hubadilika na enzi—zote ni mpya. … Kwa hivyo, wakati wa Enzi ya Sheria Yehova ndilo lilikuwa jina la Mungu, na katika Enzi ya Neema jina la Yesu lilimwakilisha Mungu. Katika siku za mwisho, jina lake ni Mwenyezi Mungu—mwenye uweza, na yeye hutumia nguvu zake kumwongoza mwanadamu, kumshinda mwanadamu, kumtwaa mwanadamu, na mwishowe, kuhitimisha enzi hiyo(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)).

Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linachoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”).

Katika siku za mwisho, Mungu anafanya kazi Yake ya hukumu ya Enzi ya Ufalme chini ya jina la Mwenyezi Mungu. Amefunua asili potovu ya mwanadamu na kuhukumu ukosefu wetu wa haki kupitia maneno Yake ili tujue asili yetu na kiini chetu kupitia kusoma maneno haya, tuone ukweli wa jinsi Shetani ametupotosha kwa undani, tuelewe kiini cha upotovu wetu, na tujue haki ya Mungu, na tabia Yake ambayo haivumilii makosa ya mwanadamu. Anatuonyesha pia njia na mwelekeo ili tubadilishe tabia zetu ili tuache maovu, tufuate ukweli, na tupate badiliko la tabia na kuokolewa na Mungu. Mungu amekuja kufanya kazi ya kuhukumu na kutakasa mwanadamu, kutugawanya kulingana na aina zetu, na kutuza mazuri na kuadhibu uovu, ili kuokoa kabisa wanadamu wapotovu kutoka kwa utawala wa Shetani na kuleta mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita kwenye kikomo. Mungu ameonekana kwa mwanadamu katika siku za mwisho akiwa na tabia Yake ya haki, uadhama, na hasira ambayo haitavumilia makosa. Ameonyesha kwa uwazi tabia Yake ya asili, na kile Anacho na Alicho kwa kila mmoja. Amekuja kuhukumu na kutakasa uovu wote na ukosefu wa haki wa mwanadamu, ili atuokoe kwa ukamilifu kutoka kwa dhambi na kurejesha utakatifu wa asili wa binadamu. Anataka watu wote waone hekima Yake katika kuumba mbingu, nchi, na vitu vyote, lakini hata zaidi hekima ya kazi Yake ya utendaji kwa mwanadamu. Hakuumba tu vitu vyote, bali Anatawala pia vitu vyote. Hakuweza tu kuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, lakini Anaweza pia kutufanya kuwa wasio na makosa, kutubadilisha, na kututakasa. Yeye ndiye wa Kwanza, na wa Mwisho. Hakuna mtu anayeweza kuelewa ajabu Yake au matendo Yake. Hivyo, kuita Mungu kwa jina Lake la Mwenyezi Mungu kunafaa zaidi. Kazi ya Roho Mtakatifu sasa ni kudumisha tu kazi iliyofanywa chini ya jina la Mwenyezi Mungu. Yeyote aombaye jina la Mwenyezi Mungu na kuabudu Mwenyezi Mungu kwa kweli anaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu, na kufurahia utajiri wa riziki ya maisha na unyunyiziaji unaopeanwa na Mungu, la sivyo wataingia gizani na kupoteza njia yao. Kwa sasa, makanisa ambayo bado yamekwama kwenye Enzi ya Neema yanapitia ukiwa. Waumini wamezembea katika imani yao, wahuburi hawana kitu cha kuhubiri, na watu hawaguswi wanapomuomba Mungu. Aidha, watu wengi zaidi wameingia katika majaribu ya ulimwengu. Sababu kuu ya hili ni kuwa hawajakubali jina la Mwenyezi Mungu, na hawajafuatilia kazi mpya ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp