Kwa nini ulimwengu wa kidini daima umemkana Kristo, kumkataa na kumhukumu Yeye, na hivyo kupitia laana za Mungu?

24/09/2018

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Sikizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mwenye nyumba fulani, aliyepanda shamba la zabibu, na akalizingira kwa ua, na akachimba kishinikizo cha zabibu ndani yake, na akajenga mnara, na akalipangisha kwa wakulima, na akasafiri kwenda nchi ya mbali: Na wakati wa matunda ulipokaribia, aliwatuma watumwa wake kwa wakulima, ili waweze kupokea matunda yake. Na wakulima wakawachukua watumwa wake, wakampiga mmoja, na kumuua mwingine, na kumpiga mwingine kwa mawe. Tena, akawatuma watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza: na wakawafanyia vivyo hivyo. Lakini mwishowe kabisa alimtuma mwanawe kwao, akisema, Watamheshimu mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona mwana huyo, walisema miongoni mwao, Huyu ndiye mrithi; njooni, tumuue, na tutwae urithi wake. Na wakamshika, wakamtupa nje ya shamba la zabibu, na wakamchinja” (Mathayo 21:33-39).

“Kisha makuhani wakuu na Mafarisayo walikonga baraza, na wakasema, Tufanye nini? Kwani mtu huyu anatenda miujiza mingi. Tukimwacha hivi peke yake, watu wote watamsadiki: nao Warumi watafika na kuichukua nafasi yetu na taifa letu” (Yohana 11:47-48).

“Hivyo kuanzia siku hiyo walishauriana pamoja ili wamuue” (Yohana 11:53).

Maneno Husika ya Mungu:

Jinsi inavyovutia! Kwa nini kupata mwili kwa Mungu daima kumekataliwa na kushutumiwa na watu? Kwa nini watu hawawi na ufahamu wowote wa kupata mwili kwa Mungu kamwe? Inawezekana kuwa Mungu amekuja wakati mbaya? Inawezekana kuwa Mungu amekuja mahali pabaya? Inawezekana kwamba hili hutokea kwa sababu Mungu ametenda peke yake, bila “sahihi” ya mwanadamu? Inawezekana ni kwa sababu Mungu alifanya maamuzi Yake Mwenyewe bila ruhusa ya mwanadamu? … Watu walikula kile Alichokitoa mdomoni Mwake, walikunywa damu Yake, walifurahia neema Aliyowapatia, lakini bado walimpinga, maana hawakujua nani aliwapa uhai walionao. Hatimaye, walimsulubisha msalabani, lakini bado Hakutoa hata sauti. Hata leo, bado Anabakia kimya. Watu wanakula mwili wake, wanakula chakula Anachowatengenezea, wanapita njia ambayo Ameifungua kwa ajili yao, na wanakunywa damu Yake, lakini bado wanakusudia kumkataa, kimsingi wanamchukulia Mungu ambaye Amewapatia maisha yao kama adui, na badala yake wanawachukulia wale ambao ni watumwa kama wao kama Anavyofanya Baba wa mbinguni. Katika hili, je, hawampingi kwa makusudi? Yesu aliwezaje kufa msalabani? Je, mnajua? Je, Hakusalitiwa na Yuda, ambaye alikuwa karibu kabisa Naye, na akamla, akamnywa, na akamfurahia? Je, sababu ya usaliti wa Yuda haikuwa ni kwa sababu Yesu hakuwa kitu chochote isipokuwa mwalimu mdogo wa kawaida? Ikiwa watu walikuwa wameona kwamba Yesu alikuwa si wa kawaida kabisa, na Ambaye Alitoka mbinguni, wangewezaje kumsulubisha msalabani Akiwa hai kwa masaa ishirini na nne, hadi Alipoishiwa na pumzi yote katika mwili wake? Nani awezaye kumjua Mungu? Watu hawafanyi chochote isipokuwa kumfurahia Mungu kwa tamaa isiyotosheka, lakini hawajawahi kumjua. Walipewa inchi na wamechukua maili, na wanamfanya Yesu kutii kabisa amri zao, na maelekezo yao. Ni nani ambaye ameonyesha huruma kwa huyu Mwana wa Adamu, Ambaye hana mahali pa kuweka kichwa Chake? Ni nani ambaye amewahi kufikiria kushikana mikono Naye kukamilisha agizo la Mungu Baba? Ni nani amewahi kumuwaza? Ni nani mbaye amewahi kuyajali matatizo Yake? Bila upendo hata kidogo, mwanadamu anamvuta nyuma na mbele; mwanadamu hajui nuru na uhai wake unatoka wapi, na hafanyi chochote isipokuwa kupanga kwa siri jinsi ya kumsulubisha tena Yesu wa miaka elfu mbili iliyopita, nani ambaye amepitia uzoefu wa maumivu miongoni mwa wanadamu. Je, Yesu anawatia watu moyo kuwa na chuki ya namna hiyo? Je, yote Aliyoyafanya yamesahaulika zamani? Chuki ambayo ilichanganyika kwa maelfu ya miaka itaibuka tena juu. Nyinyi vifaranga wa Wayahudi! Ni lini Yesu amekuwa adui yenu, hadi mmchukie kiasi hicho? Amefanya mengi na kuzungumza mengi—je hakuna chochote chenye manufaa kwenu? Ameyatoa maisha Yake kwenu bila kuomba kurudishiwa kitu chochote, Amejitoa mzima kwenu—kweli bado mnataka kumla Akiwa mzima? … Hakuna mahali ambapo huwezi kuwakuta “Wayahudi,” na leo bado wanafanya kazi ile ile, bado wanafanya kazi ile ile ya kumpinga Mungu, na bado wanaamini kwamba wanamwinua Mungu juu? Inawezekanaje macho ya mwanadamu yamjue Mungu? Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutoka katika Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua? Ukweli upo wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli ipo wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuwa miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Inawezekanaje mwanadamu kuvumilia uwepo wa Mungu? Anawezaje kuvumilia kuruhusu mwanga kuondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (10)

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[1] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba si chochote zaidi ya nzi katika kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kutegemea nguruwe na mbwa wa wazazi wao. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno.[2] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu anajua kidogo kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujazwa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza kazi yao tena ya utesaji, wakiendeleza kazi yao yenye umri wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)

Tanbihi:

1. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

2. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp