Kwa nini serikali ya Kikomunisti ya China hutesa kwa ukali, kukandamiza na kuchukulia hatua Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu?
Udhihirisho wa joka kuu jekundu ni upinzani Kwangu, ukosefu wa ufahamu na utambuzi wa maana ya maneno Yangu, mateso ya mara kwa mara Kwangu, na kutafuta kutumia njama ili kuzuia usimamizi Wangu. … Joka kuu jekundu Ninayezungumzia si joka kuu jekundu lolote fulani; badala yake ni pepo mbaya anayenipinga Mimi, ambaye kwaye “joka kuu jekundu” ni kisawe.
Kwa nini ulimwengu wa kidini daima umemkana Kristo, kumkataa na kumhukumu Yeye, na hivyo kupitia laana za Mungu?
Jinsi inavyovutia! Kwa nini kupata mwili kwa Mungu daima kumekataliwa na kushutumiwa na watu? Kwa nini watu hawawi na ufahamu wowote wa kupata mwili kwa Mungu kamwe? Inawezekana kuwa Mungu amekuja wakati mbaya? Inawezekana kuwa Mungu amekuja mahali pabaya? Inawezekana kwamba hili hutokea kwa sababu Mungu ametenda peke yake, bila “sahihi” ya mwanadamu? Inawezekana ni kwa sababu Mungu alifanya maamuzi Yake Mwenyewe bila ruhusa ya mwanadamu? …