Wimbo wa Sifa | Mwenyezi Mungu, Anayependeza Zaidi (Muziki wa Akapela)

21/07/2020

Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo, Anayependeza zaidi!

Umeshuka kutoka mbinguni hadi duniani, ukiwa katika mwili.

Unaishi pamoja na mwanadamu, na hakuna aliyewahi kukujua.

Mnyenyekevu na Uliyejificha, Unanena maneno Yako,

ukileta njia ya uzima wa milele.

Unapitia shida na fedheha, yote kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu.

Unayaeleza maisha Yako kwa mwanadamu waziwazi,

nasi twaona jinsi unavyopendeza.

Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo, Anayependeza zaidi!

Duniani, Wewe ndiwe Upendezaye zaidi, tutakupenda milele.

Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo, Anayependeka sana!

Moyo Wako na upendo Wako unazidi wa yeyote duniani.

Unahukumu na kuwaadibu wanadamu,

unawajaribu na kuwasafisha kwa njia za kila aina.

Kazi na maneno Yako yote ni ili kutakasa na kuokoa wanadamu.

Unatupa ukweli wote na unayaeleza mapenzi Yako waziwazi.

Hukumu Yako na upendo Wako umeshinda mioyo yetu kabisa.

Mwenyezi Mungu, Mwenye kupendeka sana!

Duniani, Wewe unapendeka sana, tutakupenda milele.

Mwenyezi Mungu, Mwenye kupendeka sana!

Mwenyezi Mungu, Mwenye kupendeka sana!

Mwenyezi Mungu, Mungu wa vitendo, anayependeka sana!

Kupitia hukumu Yako, upotovu wetu unatakaswa.

Tunathamini hekima na uweza Wako,

na tunajua haki na utakatifu Wako.

Tunapitia upendo Wako na ni wa kweli zaidi na halisi.

Unalipia gharama kubwa sana ili kutuokoa.

Wewe ni mzuri kwa njia nyingi sana,

tutakosaje kuchukia kujitenga na Wewe?

Mwenyezi Mungu, Mwenye kupendeka sana!

Duniani, Wewe unapendeka sana, tutakupenda milele.

Mwenyezi Mungu, Mwenye kupendeka sana!

Duniani, Wewe unapendeka sana, tutakupenda milele.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp