Wimbo wa Injili | Hisia za Dhati za Muumba Kuelekea Binadamu (Music Video) | Sauti za Sifa 2026
14/01/2026
Kifungu kifuatacho kilirekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: "Kisha Yehova akasema, Umekitunza sana kibuyu, ambacho hujakifanyia kazi, wala kukikuza; ambacho kilimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami, je, sipaswi kulitunza Ninawi, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini humo ambao hawawezi kupambanua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo mingi?" Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu, kutoka katika mazungumzo kati ya Mungu na Yona. Ingawa mazungumzo haya ni mafupi, yamejaa kutotaka kwa Muumba kumwacha mwanadamu na utunzaji Wake kwa binadamu. Maneno haya yanaonyesha mtazamo na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kwa viumbe Wake aliowaumba. Maneno haya pia ni Mungu akieleza nia Zake za kweli kwa binadamu, kwa njia iliyo dhahiri ambayo binadamu husikia kwa nadra sana.
1
Muumba yuko miongoni mwa binadamu wakati wote, siku zote Anazungumza na binadamu na vitu vyote, na Anatekeleza matendo mapya kila siku. Kiini Chake na tabia Yake vimeonyeshwa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafunuliwa kabisa katika matendo Yake; Anaandamana na mwanadamu na kumtazama wakati wote. Yeye anatumia maneno Yake asiyotamka kuwaambia wanadamu na vitu vyote kwa utulivu: "Mimi niko mbinguni, na Mimi nimo miongoni mwa vitu vyote. Ninaangalia, Ninasubiri; Niko kando yako…."
2
Mikono Yake ni yenye joto na nguvu; nyayo Zake ni nyepesi; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake hupita na kugeuka, likiwakumbatia wanadamu wote; uso Wake ni mzuri na mpole. Hajawahi kuondoka, hajawahi kutoweka. Usiku na mchana, Yeye yuko na mwanadamu siku zote, Asiyeondoka upande wao kamwe. Utunzaji Wake wa kujitolea na mapenzi Yake ya kipekee kwa binadamu, pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu, yalionyeshwa kidogo kidogo Alipouokoa mji wa Ninawi. Hasa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona yalifunua kikamilifu upole wa Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Alimuumba. Kupitia katika maneno hayo, unaweza kufahamu kwa kina hisia za dhati za Mungu kwa binadamu …
kutoka katika Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video