Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Mungu Anatafuta Moyo Wako na Roho Yako” | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Binadamu, wakiwa wamepotoka kutoka kwa ugavi wa uzima wa Mwenye Uweza, hawajui kusudi la kuwepo, lakini wanaogopa kifo hata hivyo. Hawana msaada au tegemeo, lakini bado hawako tayari kufumba macho yao, na wanajikaza kuitegemeza miili yao, isiyo na hisia yoyote ya kiroho, na kujikokota kuishi maisha duni duniani humu. Wewe unaishi hivyo, bila tumaini, kama wafanyavyo wengine, bila lengo. Ni Yule Mtakatifu wa ngano pekee ndiye Atakayewaokoa watu ambao, wakiwa wanaomboleza katikati ya mateso yao, wanangoja kwa hamu kubwa kuja Kwake. Imani kama hiyo imebaki bila kutimizwa kwa muda mrefu ndani ya wale wasio na fahamu. Hata hivyo, bado wanaitamani sana.

2

Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana; wakati huo huo, Anawachukia watu hawa wasio na fahamu zozote kabisa, kwani inabidi Asubiri kwa muda mrefu sana kabla ya kupokea jibu kutoka kwa watu. Anataka kutafuta, kutafuta moyo wako na roho yako, na kukuletea maji na chakula, ili uzinduke na usiwe na kiu au njaa tena. Unapochoka na unapohisi kiasi fulani cha ukiwa wa dunia hii, usijihisi umepotea, usilie. Mwenyezi Mungu, Mwangalizi, atakumbatia kuja kwako wakati wowote. Anakesha kando yako. Anakusubiri urejee, akisubiri siku utakayorejesha kumbukumbu yako ghafla: utakapotambua kwamba ulitoka kwa Mungu, na kwamba, wakati fulani usiojulikana ulipoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ulilala usingizi njiani, na wakati fulani usiojulikana ulikuwa na "baba"; unapotambua, zaidi ya hayo, kwamba Mwenye Uweza amekuwa akikesha daima, Akisubiri hapo kwa muda mrefu sana, sana kwa ajili ya kurudi kwako. Amekuwa akitamani kwa hamu kubwa, akisubiri itikio lisilo na jibu. Kukesha Kwake ni kwa thamani isiyokadirika, na ni kwa ajili ya moyo wa mwanadamu na roho ya mwanadamu. Pengine kukesha Kwake hakuna kikomo, au pengine kumefika mwisho. Lakini unapaswa kujua hasa ulipo moyo wako na ilipo roho yako sasa hivi.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp