Wimbo wa Injili | Mungu Amhukumu na Kumkamilisha Mwanadamu kwa Maneno Yake Katika Siku za Mwisho

29/06/2020

Mungu katika mwili wa siku za mwisho

Amekuja hasa kwa ajili ya kuzungumza maneno Yake,

ili kuelezea yale yote ambayo ni ya lazima katika maisha ya mwanadamu,

kuonyesha yale ambayo mwanadamu anapaswa kuingia kwayo,

kumwonesha mwanadamu matendo ya Mungu,

na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu,

na kumwonesha mwanadamu hekima, uweza na uajabu wa Mungu.

Kupitia njia nyingi ambazo Mungu Anazungumza,

mwanadamu anatazama ukuu wa Mungu, aidha,

unyenyekevu na usiri wa Mungu.

Mwanadamu anatazama kwamba Mungu ni mkuu,

lakini ni mnyenyekevu na msiri, na Anaweza kuwa mdogo kuliko vitu vyote.

Baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa Roho,

baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa moja kwa moja kutoka kwa mtazamo wa mwanadamu,

na baadhi ya maneno Yake yanazungumzwa kutoka kwa mtazamo wa nafsi ya tatu.

Katika hili inaweza kuonekana kwamba

namna ya kazi ya Mungu inatofautiana kwa kiasi kikubwa

na ni kwa njia ya maneno ndipo Anamruhusu mwanadamu kuiona.

Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii

ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu,

kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika,

uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi,

mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu.

Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu.

Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno

na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu.

Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu,

kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu,

Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu,

kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu,

ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu,

na aje kuelewa tabia ya Mungu,

ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.

Wakati wa siku za mwisho, kimsingi Mungu Anakusudia kukamilisha

hatua ya kazi ambayo kwayo Neno Anaonekana katika mwili,

na hii ni sehemu moja ya mpango wa usimamizi wa Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp