Wimbo wa Kikristo | Mungu Asikitikia Mustakabali wa Binadamu

27/08/2020

Katika upana mkubwa wa dunia hii, mabadiliko yasiyohesabika yamefanyika,

bahari kujaa hadi kuziba mashamba, mashamba kufurika hadi baharini, tena na tena.

Isipokuwa Yule ambaye anatawala kila kitu katika ulimwengu,

Hakuna anayeweza kuongoza na kuelekeza jamii hii ya wanadamu.

Hakuna yeyote hodari kufanya kazi

au kufanya maandalizi kwa ajili ya jamii hii ya binadamu,

sembuse yule anayeweza kuiongoza jamii hii ya wanadamu

hadi hatima ya mwanga

na kuikomboa kutokana na udhalimu wa duniani.

Mungu hulalamikia wakati ujao wa wanadamu,

huhuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu

na anaumizwa kwamba binadamu wanatembea,

hatua baada ya nyingine hadi kuoza na katika njia ambayo hawawezi kurudi.

Wanadamu ambao wameuvunja moyo wa Mungu

na wakamkana kumfuata yule mwovu:

je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaza

kuhusu mwelekeo ambao wanadamu wa aina hii huenda wanafuata?

Ni kwa sababu hii haswa kwamba hakuna anayehisi hasira ya Mungu,

hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu

au kujaribu kuja karibu na Mungu na isitoshe,

hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu.

Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu,

binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mwenyewe,

anazidi kwenda mbali na Mungu,

kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli Wake,

akiona heri kujiuza kwa Shetani, adui wa Mungu.

Na ni nani amefikiri—iwapo mwanadamu ataendelea kuwa mkaidi—

jinsi Mungu atakavyowatendea wanadamu hawa ambao wamempuuza bila kusita?

Hakuna anayejua kwamba maana ya ukumbusho wa mara kwa mara na kusihi kwa Mungu

ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake

maafa yasiyokuwa ya kawaida ambayo ameandaa,

Yeye anayo katika mikono yake maafa yasiyokuwa ya kawaida ambayo ameandaa,

maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili.

Maafa haya siyo tu adhabu ya mwili bali pia ya roho.

Unafaa kujua hili: Mpango wa Mungu utakaposhindikana

na wakati makumbusho Yake na kusihi Kwake hakutapata majibu yoyote,

atatoa hasira ya aina gani?

Atatoa hasira ya aina gani?

Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali

au hata kusikika na viumbe vyovyote.

Na hivyo Nasema, majanga haya hayana mengine ya kulinganishwa nalo awali

na kamwe hayatawahi kurudiwa.

Hii ni kwa sababu ni mpango wa Mungu kuumba wanadamu mara hii moja tu

na kuwaokoa wanadamu mara hii moja tu.

Hii ndiyo mara ya kwanza na pia ni ya mwisho.

Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa

nia za bidii na hamu ya ari ambazo kwazo

Mungu huokoa wanadamu wakati huu.

Hakuna anayeweza kuelewa

nia za bidii na hamu ya ari ambazo kwazo

Mungu huokoa wanadamu wakati huu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp