Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kazi na Kuonekana kwa Mungu | Dondoo 62

01/08/2020

Watu ulimwenguni kote wanasherehekea kufika kwa siku Yangu, na malaika wanatembea miongoni mwa halaiki. Shetani anapoleta vurugu, malaika, kwa sababu ya huduma yao mbinguni, daima huwasaidia watu Wangu. Wao hawadanganywi na ibilisi kwa sababu ya udhaifu wa binadamu, ila wanapata uzoefu mwingi wa maisha ya mwanadamu yaliyojawa na ukungu unaosababishwa na uvamizi wa nguvu za giza. Watu wote wananyenyekea chini ya jina Langu, na hakuna wakati ambapo mtu huinuka kwa wazi kunipinga Mimi. Kwa sababu ya shughuli za malaika, mwanadamu anakubali jina Langu na wote wako katika mtiririko wa kazi Yangu. Dunia inaanguka! Babeli imelemaa! Dunia ya kidini—itakosa kuharibiwa vipi na mamlaka Yangu duniani? Ni nani bado anathubutu kuniasi na kunipinga? Waandishi? Wakuu wote wa kidini? Viongozi na wenye mamlaka wa duniani? Malaika? Ni nani asiyesherehekea ukamilifu na wingi wa mwili Wangu? Miongoni mwa watu wote, nani asiyeimba sifa Zangu bila kukoma, ni nani asiye na furaha isiyoshindwa? Ninaishi katika nchi ya kiota cha joka kubwa jekundu, ilhali hili halinifanyi Mimi nitetemeke kwa uoga wala kutoroka, kwa maana watu wa nchi hii wote wameanza kulichukia. “Jukumu” la chochote halijawahi kutendwa mbele ya joka hili; badala yake, vitu vyote anaendesha shughuli zake, wakichukua njia inayowafaa zaidi. Je, mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuangamia? Mataifa ya ulimwengu yatakosaje kuanguka? Watu Wangu watakosaje kushangilia? Watakosaje kuimba kwa furaha? Je, hii ni kazi ya mwanadamu? Je, ni tendo la mikono ya mwanadamu? Nilimpa mwanadamu mzizi wa kuwepo kwake, na Nikampa vitu halisi vya dunia, ilhali mwanadamu haridhiki na hali yake ya sasa na anauliza kuingia katika ufalme Wangu. Lakini atawezaje kuingia katika ufalme Wangu kwa urahisi vile, bila kulipa gharama yoyote, na bila nia ya kujitoa kwa kujinyima? Badala ya kulazimisha chochote kutoka kwa mwanadamu, Mimi huweka mahitaji kwake, ili ufalme Wangu duniani ujawe na utukufu. Mwanadamu ameongozwa na Mimi mpaka enzi ya sasa, anaishi katika hali hii, na anaishi katika mwongozo wa mwanga Wangu. Kama haingekuwa hivyo, nani kati ya watu wote duniani angejua matarajio yake? Ni nani ambaye angeelewa mapenzi Yangu? Ninaongeza matoleo Yangu katika mahitaji ya mwanadamu; je, hii haiambatani na sheria za hali asili?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp