Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho | Dondoo 239

09/11/2020

Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong’aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu. Wakati ambapo mbingu mpya inashuka duniani na nchi mpya kuenea juu ya anga ndio pia wakati hasa ambao Ninafanya kazi kirasmi miongoni mwa binadamu. Ni nani kati ya wanadamu anayenijua Mimi? Ni nani aliyeona wakati wa kuwasili Kwangu? Ni nani ameona kwamba Mimi sina jina tu, bali zaidi ya jina Nina dutu? Mimi huyasongeza mawingu meupe kwa mkono wangu na kwa karibu Naichunguza anga; katika anga, hakuna kitu kisichopangwa kwa mkono wangu, na chini ya anga, hakuna mwanadamu asiyechangia juhudi yake ndogo kwa ukamilishaji wa shughuli Yangu kuu. Mimi Simwekei mwanadamu madai mazito duniani, kwa maana Mimi daima Nimekuwa Mungu wa vitendo, na kwa sababu Mimi ni Mwenyezi Aliyeumba mwanadamu na Anayejua mwanadamu vizuri. Watu wote wako machoni pa Mwenyezi. Hata wale walio katika pembe zote mwisho wa dunia watawezaje kuepuka uchunguzi wa Roho Yangu? Ingawa mwanadamu anajua Roho Wangu, yeye pia huichukiza Roho Wangu. Maneno Yangu yanaweka wazi uso mbaya wa wanadamu wote, na kuweka wazi mawazo ya ndani kabisa ya watu wote, na kusababisha wote duniani kufanywa wazi na mwanga Wangu na kuanguka chini ndani ya uchunguzi Wangu. Ijapokuwa mwanadamu anaanguka chini, moyo wake hauthubutu kwenda mbali Nami. Miongoni mwa viumbe, ni nani asiyekuja kunipenda kwa sababu ya matendo Yangu? Ni nani asiyekuwa na hamu kwa ajili ya kuyasikia maneno Yangu? Ni nani asiyezaliwa ndani mwake na hisia za ibada kwa sababu ya upendo Wangu? Ni kwa sababu tu ya ufisadi wa Shetani ndio maana mwanadamu anashindwa kuufikia ulimwengu kama Ninavyomhitaji kufika. Hata viwango vya chini kabisa ambavyo Mimi Namhitaji kufika huzalisha mashaka ndani yake, bila kutaja chochote cha leo, enzi ambayo Shetani anaendesha ghasia na ni mdhalimu mkuu, au wakati ambapo mwanadamu amekanyagwa sana na Shetani mpaka mwili wake mzima umejaa uchafu. Ni lini ambapo kutojali kwa mwanadamu kuhusu moyo Wangu kwa sababu ya upotovu wake hakujanisababishia Mimi huzuni? Je, inawezekana kwamba Mimi namwonea Shetani huruma? Je, inawezekana kwamba Mimi Nimekosea katika upendo wangu? Wakati mwandamu ananikaidi, Moyo wangu unaomboleza kwa siri; wakati mwanadamu ananipinga, Ninamwadibu; wakati Ninamwokoa mwandamu na kumfufua kutoka wafu, Mimi Humlisha kwa uangalifu ulio bora zaidi; wakati mwanadamu ananitii, Moyo Wangu unatulia tuli na mara moja Ninahisi mabadiliko makubwa katika mambo yote mbinguni na duniani; wakati mwanadamu ananisifu, itawezekanaje Nisiwe na furaha? Wakati mwanadamu ananishuhudia na kupatwa na Mimi, itawezekanaje Nisitukuzwe? Inawezekana kwamba kila anachofanya mwanadamu hakiongozwi na kutolewa na Mimi? Wakati ambapo Sitoi mwelekeo, wanadamu wanazembea na kuwa wanyamavu, na, nyuma Yangu, wao wanashiriki katika zile shughuli chafu “zenye kusifika.” Je, unafikiri kwamba mwili Ninaouvaa, haufahamu chochote kuhusu matendo yako, tabia zako, na maneno yako? Nimestahimili mvua na upepo kwa miaka mingi, na vile vile Nimepitia machungu ya ulimwengu wa binadamu, lakini ukitafakari kwa karibu, hakuna kiasi cha mateso kinachoweza kumfanya mwanadamu aliye katika nyama za mwili kupoteza matumaini ndani Yangu, kama vile hakuna utamu wowote unaoweza kumfanya mwanadamu wa mwili awe bila hisia, mwenye kuvunjika moyo au mwenye kunipuuza Mimi. Je, upendo wa mwanadamu Kwangu una mipaka kwa hali ya kutokuwa na maumivu au kutokuwa na utamu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 9

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp