Christian Testimony Video | Ulinzi wa Mungu (Swahili Subtitles)

05/08/2020

Katika Ulinzi wa Mungu, kwa kuwa mhusika mkuu ana ubora fulani wa tabia na anashuhudia matokeo kiasi katika wajibu wake, anaanza kuwa mwenye majivuno, na kuwa mwenye kiburi na makuu zaidi, na kumdharau kila mtu mwingine. Yeye hufanya chochote anachotaka na husababisha usumbufu kwa kazi ya kanisa. Anapogolewa na kushughulikiwa kwa njia ambayo inaacha kumbukumbu isiyofutika moyoni mwake, na kupitia ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu, anapata ufahamu kiasi juu ya asili yake mwenyewe ya kiburi na anakuja kufahamu kuwa tabia ya haki ya Mungu haitavumilia kosa lolote. Anamcha Mungu kiasi na kuanza kulenga kutafuta ukweli na kutenda kulingana na kanuni katika wajibu wake. Anakuja kuhisi kwa kweli kwamba ni kupitia tu hukumu na kuadibu kwa Mungu ndiyo tabia potovu inaweza kutakaswa na kubadilishwa, na kwamba kupogolewa, kushughulikiwa, kuhukumiwa, na kuadibiwa ni upendo na ulinzi mkuu zaidi wa Mungu kwa wanadamu.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp