Kuonekana Kwa Mwenyezi Mungu na Kazi Yake: Historia ya Kuzaliwa na Kukua kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu (Sehemu 1)

02/05/2020

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alisema, "Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu" (Mathayo 4:17). na Akaahidi, "Nakuja kwa haraka" (Ufunuo 22:7). Kwa muda wa miaka elfu mbili ya kutumaini, na miaka elfu mbili ya kungojea… vizazi vya Wakristo vilikuwa vikisubiri kwa hamu kurudi kwa Bwana Yesu. Wanadamu wote walitamani sana Mwokozi afike na kuwaokoa wanadamu kikamilifu. Wakati tu ambapo ulimwengu ulikuwa katika giza kuu, wakati ambapo nguvu mbaya za Shetani zilikuwa katili na kali zaidi katika upinzani wao dhidi ya Mungu, kulipambazuka huko Mashariki—nchini China. Mnamo 1991, mwaka huo wa ajabu, Mwana wa Adamu mwenye mwili, Mwenyezi Mungu, Alionekana katika makanisa ya nyumbani ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi. Huko Alianza kutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu.

Filamu hii inayoonyesha hali halisi kimsingi inaonyesha historia ya kweli ya jinsi Mwenyezi Mungu alivyoonekana miongoni mwa makanisa ya nyumbani na kuanza kufanya kazi Yake na kutamka maneno Yake. Kwa kuwa wateule wameshiriki maneno haya ya siku hizi ya Mwenyezi Mungu, wamekuja kuelewa ukweli polepole, kupata njia ya utendaji, na kufurahia furaha kamili na uhuru ambao Roho Mtakatifu aliwaletea wanadamu.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp