Filamu ya Kikristo | “Kabla ya Uchaguzi” | Who Does She Vote For? (Swahili Subtitles)

02/10/2020

Zhou Qingyu ni kiongozi wa kanisa ambaye ana ubora mzuri wa tabia, ni hodari na amefanikisha matokeo mazuri katika wajibu wake, na anapendwa na ndugu zake. Uchaguzi wa kanisa wa kila mwaka unapokaribia, ana hakika kwamba atachaguliwa tena. Wakati huo, kiongozi wa kanisa katika mashariki mwa jiji, Yang Jie, anaporipotiwa katika mkutano na kusakwa na CCP. Anatoroka na anapewa wajibu fulani katika kanisa la Zhou Qingyu, na baadaye yeye pia anajiunga na uchaguzi kama mgombea. Baada ya muda mfupi, Zhou Qingyu anagundua kwamba ndugu wote wanataka kusikia ushirika wa Yang Jie na wanamsifu kwa kuwa na uhalisi wa ukweli, na anamwonea wivu. Ili kulinda hadhi na sifa yake mwenyewe, Zhou Qingyu anajionyesha, anajaribu kumtenga Yang Jie, na anajikuta akidhibitiwa na tabia potovu ya kushindania sifa na hadhi. Je, Zhou Qingyu anaondokanaje na vizuizi na utumwa wa kutafuta sifa na hadhi? Na uchaguzi unakapokuja, atawezaje kupiga kura yake? Tazama Kabla ya Uchaguzi ili ujue.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp