Christian Movie Based on a True Story | “Makovu ya Kudumu” | 28 Years of Persecution by the CCP

21/10/2020

Li Chenxi amehudhuria mikutano na kusoma Biblia pamoja na wazazi wake tangu alipokuwa mchanga. Mnamo 1988 akiwa mwenye umri wa miaka 13 tu, anakamatwa anapokuwa akihudhuria mkutano, kisha anafungiwa katika chumba kidogo na cha giza kwa siku tatu. Kuanzia wakati huo, CCP haiachi kamwe kumtesa. Anakamatwa tena na polisi akiwa mwenye umri wa miaka 17 kwa kuwatumia ndugu wengine waliokuwa kanisani vitabu vya maneno ya Mungu. Ili kujaribu kumlazimisha afichue vilikotoka vitabu hivyo, polisi wanampiga babake kikatili mbele yake na kumtembeza mitaani akiwa amepachikwa jina “mfungwa wa kisiasa.” Mnamo 1996, polisi wanakuja kumkamata tena Li Chenxi. Hana chaguo lingine ila kuukimbia mji wake na kuanza maisha ya mkimbizi. Mashambulio na vitisho vya mara kwa mara vya polisi wa CCP vinaiacha familia yake yote ikiishi siku zote katika hali ya hofu kuu. Kwa sababu ya mamake kushindwa kuvumilia mfadhaiko na hofu ya muda mrefu, anarukwa na akili, na baba yake, ambaye tayari alikuwa na matatizo ya afya, anaona hali yake ikianza kuwa mbaya hata zaidi kwa sababu ya kupigwa vikali na polisi. Familia iliyokuwa na furaha wakati mmoja inavunjwa. Anapokuwa akikimbia, Li Chenxi anajiunga na kina ndugu katika kueneza injili kote nchini. Wanateseka chini ya utawala mbaya wa CCP, wanakandamizwa na kukamatwa mara nyingi. Ndugu wengine wanakamatwa na kisha kuteswa vikali. Wengine wanapigwa hadi kufa na wengine wanahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 10. Mwishoni mwa mwaka wa 2012, Li Chenxi anakamatwa tena anapokuwa akishiriki injili na anapitia miezi minne mirefu ya mahojiano, majaribio ya kumlazimisha akiri na utiaji kasumba.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp