Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 392

29/08/2020

Katika nyakati zilizopita, watu wengi walifuatilia kwa jitihada na fikira za mwanadamu na kwa ajili ya matumaini ya mwanadamu. Mambo haya hayatajadiliwa sasa. La muhimu ni kupata njia ya kutenda ambayo itawezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele ya Mungu na hatimaye kuvunja pingu za ushawishi wa Shetani, ili mpate kuwa wakubalika wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha duniani matakwa ya Mungu kwenu. Ni haya tu yanayoweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Wengi wanaamini katika Mungu, ila hawajui ni kitu gani Anachotamani Mungu wala ni nini anachotamani Shetani. Wao wanaamini kipumbavu na kuwafuata watu wengine kama vipofu, na kwa hivyo hawajakuwa kamwe na maisha ya kawaida ya Kikristo; hawana uhusiano wa kawaida wa binafsi na watu wengine, sembuse uhusiano wa kawaida ambao mwanadamu anao na Mungu. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba matatizo na makosa ya mtu, na mambo mengine ambayo yanaweza kuzuia mapenzi ya Mungu ni mengi. Hili linatosha kuthibitisha kwamba mwanadamu hajajiandaa kikamilifu kufuata njia iliyo sahihi wala kuwa na uzoefu wa maisha halisi. Kujiandaa kufuata njia iliyo sahihi ni nini? Kujiandaa kufuata njia iliyo sahihi ina maana kwamba unaweza kunyamazisha moyo wako mbele za Mungu wakati wote na wasiliana kwa karibu na Mungu, hatua kwa hatua ukipata kujua ni nini kinachokosa ndani ya mwanadamu na polepole kupata kumfahamu Mungu zaidi. Kwa njia hii, utakuwa kila siku utapata maono mapya na kupata nuru kiroho; hamu yako inakua, na wewe kutafuta kuingia katika ukweli. Kila siku kuna mwanga mpya na ufahamu mpya. Kupitia njia hii, wewe hatua kwa hatua unavunja ushawishi wa Shetani na kuwa huru, na maisha yako yanakua kwa kiasi kikubwa. Mtu kama huyu ameweka mikakati ya kufuata mwenendo sawa. Tathmini uzoefu wako mwenyewe halisi na kuchunguza njia uliyoichukua katika imani yako kwa Mungu dhidi ya yaliyotajwa hapo juu. Wewe ni yule ambaye amepangwa kufuata mwenendo sawa? Ni katika masuala gani ambapo umejiweka huru kutokana na pingu za shetani na kutokana na ushawishi wa Shetani? Kama bado hujajiandaa kufuata njia iliyo sahihi, uhusiano wako na Shetani bado haujaisha. Kwa jinsi hiyo, ukimbiziaji huu wa upendo kwa Mungu inaweza kusababisha upendo ambao ni sahihi, wa kujitolea, na safi? Unasema kwamba upendo wako kwa Mungu ni wa dhati na imara, bali hujajinasua kutoka kwa pingu za Shetani. Je, wewe si unajaribu kumpumbaza Mungu? Ukitaka kuufikia upendo safi kwa Mungu, kuwa wa Mungu kikamilifu, na kuwa mhesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme, basi lazima kwanza ujiandae kufuata njia iliyo sahihi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp