Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kuingia Katika Uzima | Dondoo 403

16/10/2020

Tukisonga mbele, kuzungumzia neno la Mungu ni kanuni ambayo unaongelea. Mnapokuja pamoja, mnafaa kushiriki kuhusu neno la Mungu na kulitumia kama mada yenu; zungumzieni kuhusu kile mnachojua kuhusu neno la Mungu, namna mnavyoitia katika vitendo neno Lake, na namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi. Ukishiriki kuhusu neno la Mungu, Roho Mtakatifu atakuangaza. Binadamu pia lazima ashirikiane kama huu utakuwa ndio ulimwengu wa neno la Mungu. Kama hutaingia ndani ya hili, Mungu hawezi kufanya kazi Yake. Kama hutazungumzia neno Lake, Hawezi kukuangaza. Unapopata nafasi, zungumzia neno la Mungu. Usizungumze tu bila mpango! Acha maisha yako yakajazwe na neno la Mungu; kisha utakuwa muumini mwenye kumcha Mungu. Hata kama ushirika wako ni hafifu, hiyo ni sawa. Bila ya hali hiyo ya juujuu, hakuwezi kuwa na kina. Kunao mchakato ambao lazima upitiwe. Kupitia kwa mazoezi yako, unapata utambuzi wa kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na namna unavyoweza kula na kunywa neno la Mungu kwa njia bora. Baada ya kipindi cha uchunguzi kama huo, utaingia katika uhalisia wa neno la Mungu. Ni kama tu utakuwa na uamuzi wa kushirikiana ndipo utakapopokea kazi ya Roho Mtakatifu.

Kunayo mielekeo miwili ya kanuni za kula na kunywa neno la Mungu: Mmoja unahusiana na maarifa, na mwingine ni kuingia. Ni maneno yapi unayofaa kujua? Unafaa kujua maneno yanayohusiana na maono (hivyo ni kusema, ni enzi gani Mungu amekwisha ingia ndani yake, ni nini ambacho Mungu Angependa wewe kutimiza sasa, kupata mwili ni nini, na kadhalika. Haya yote yana uhusiano na maono). Ni njia gani ambamo binadamu anafaa kuingia? Hii inarejelea maneno ya Mungu ambayo binadamu anafaa kufanyia mazoezi na kuingia ndani. Hii ndiyo mielekeo miwili ya kula na kunywa neno la Mungu. Kuanzia sasa, kula na unywe neno la Mungu kwa njia hii. Kama unao uelewa kamili wa maneno yanayohusu maono, basi hakuna haja ya kusoma zaidi. Kilicho na umuhimu mkubwa ni kula na kunywa zaidi ya maneno kuhusu kuingia, kama vile kuelekeza moyo wako kwa Mungu, namna ya kutuliza moyo wako mbele ya Mungu, na namna ya kunyima mwili. Haya ndiyo unayofaa kufanyia mazoezi. Bila ya kujua namna ya kula na kunywa neno la Mungu, ushirika wa kweli hauwezekani. Punde utakapojua namna ya kula na kunywa neno Lake, na umeng’amua kilicho muhimu, ushirika utakuwa huru. Masuala yawayo yote yaulizwapo, unaweza kushiriki kuyahusu na kung’amua uhalisia. Kushiriki kuhusu neno la Mungu bila ya uhalisia kunamaanisha huwezi kung’amua kilicho muhimu, na hii inamaanisha kwamba hujui kula na kunywa neno Lake. Wengine huhisi uchovu wakati wanaposoma neno la Mungu. Hali kama hiyo si kawaida. Kwa hakika, kilicho kawaida ni kutochoka wakati unasoma neno la Mungu, siku zote kuwa na kiu ya neno la Mungu, na kila wakati kufikiria kuwa neno la Mungu ni zuri. Hivi ndivyo mtu ambaye kweli ameingia anakula na kunywa neno la Mungu. Unapohisi kwamba neno la Mungu ni la kimatendo kweli na ndilo hasa lile binadamu anafaa kuingia ndani; unapohisi kwamba neno Lake ni lenye manufaa na faida kubwa kwa binadamu, na huo ndio ujazo wa uzima wa binadamu, unapokea hisia hii kutoka kwa Roho Mtakatifu, kupitia kwa wewe kuguswa na Roho Mtakatifu. Hii inathibitisha kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako na kwamba Mungu hajakugeukia. Kuona kwamba Mungu siku zote anaongea, baadhi huwa na uchovu wa maneno Yake na kufikiria kwamba hakuna tofauti yoyote kama watasoma maneno Yake au hawatasoma. Hiyo si hali ya kawaida. Mioyo yao haina kiu ya kuingia katika uhalisi, na binadamu kama hao hawana kiu ya kufanywa watimilifu wala kutilia umuhimu kwa kufanywa watimilifu. Kila unapopata huna kiu ya neno la Mungu, yaonyesha kwamba hali yako si ya kawaida. Siku za kale, kama Mungu alikugeukia au la iliamuliwa na kama wewe ulikuwa na amani ndani yako na ulipitia furaha. Sasa kilicho muhimu ni kama una kiu ya neno la Mungu, kama neno Lake ndio uhalisi wako, kama wewe ni mwaminifu, kama unaweza kufanya kile unachoweza kwa ajili ya Mungu. Kwa maneno mengine, binadamu huhukumiwa na uhalisia wa neno la Mungu. Mungu huelekeza neno Lake kwa watu wote. Kama uko radhi kulisoma, Atakupa nuru, lakini kama huko radhi, Hatakupa nuru. Mungu hupa nuru wale walio na njaa na kiu ya haki, na wale wanaomtafuta Yeye. Baadhi husema kwamba Mungu hakuwapa nuru hata baada ya wao kusoma neno Lake. Maneno haya yalisomwa vipi? Ukisoma neno Lake kama kutazama maua mgongoni mwa farasi na hukutilia umuhimu katika uhalisia, Mungu angekupa nuru vipi? Ni vipi ambavyo mtu asiyethamini neno la Mungu atakavyofanywa kuwa mtimilifu na Yeye? Kama huthamini neno la Mungu, basi hutakuwa na ukweli wala uhalisia. Kama utathamini neno Lake, basi utaweza kutia katika matendo ukweli; ni hapo tu ndipo utakapokuwa na uhalisia. Hivyo basi lazima ule na kunywa neno la Mungu licha ya hali yoyote ile, kama una shughuli au la, kama hali ni mbaya au la, na kama unajaribiwa au la. Kwa jumla, neno la Mungu ndilo msingi wa uwepo wa mwanadamu. Hakuna yule anayeweza kugeukia neno Lake na lazima ale neno Lake kana kwamba ndilo milo ile mitatu ya siku. Linaweza kuwa suala rahisi hivyo kufanywa kuwa mtimilifu na kupatwa na Mungu? Iwapo unaelewa au hauelewi kwa sasa au kama una utambuzi wa kazi ya Mungu, lazima ule na kunywa zaidi ya neno la Mungu. Huku ndiko kuingia katika njia makini ya utendaji. Baada ya kulisoma neno la Mungu, harakisha kukitia katika matendo kile unachoweza kuingia ndani, na utenge kwa wakati huu kile huwezi kuingia ndani. Huenda kukawa na mambo mengi katika neno la Mungu ambayo huwezi kuyaelewa mwanzoni, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, pengine hata mwaka mmoja, utaweza. Kwa nini hali iko hivi? Hii ni kwa sababu Mungu hawezi kumfanya binadamu kuwa kamili kwa siku moja au mbili. Wakati mwingi, unapolisoma neno Lake, pengine huwezi kuelewa kwa wakati huo. Wakati huo, yaweza kuonekana kama maandishi tu; ni kupitia tu kipindi cha uzoefu ndipo unapoweza kuelewa. Mungu ameongea mengi, hivyo basi unafaa kufanya yale mengi zaidi unayoweza ili kula na kunywa neno Lake. Bila ya kutambua, utakuja kuelewa, naye Roho Mtakatifu atakupa nuru. Wakati Roho Mtakatifu humpa nuru binadamu, mara nyingi ni bila ya ufahamu wa binadamu. Hukupa nuru na kukuongoza unapokuwa na kiu na unapotafuta. Kanuni ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi imekita mizizi katika neno la Mungu ambalo unakula na kunywa. Wale wote ambao hawatilii umuhimu katika neno la Mungu na siku zote wana mwelekeo mwingine katika neno Lake, mwelekeo ule wa uzembe na kusadiki kwamba hakuna tofauti yoyote kama watalisoma neno Lake, ndio wale wasiokuwa na uhalisia. Si kazi ya Roho Mtakatifu wala nuru kutoka Kwake vinavyoweza kuonekana ndani yao. Watu kama hao wanasairi tu, na ni wanafiki wasiokuwa na kufuzu kwa ukweli, kama Bw. Nanguo wa hadithi ya mafumbo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp