Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu | Dondoo 453

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu | Dondoo 453

19 |01/09/2020

Kila mtu ambaye ameamua anaweza kumhudumia Mungu—lakini ni lazima iwe kwamba wale tu ambao wanayashughulikia kwa makini mapenzi ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu ndio wanaohitimu na walio na haki ya kumhudumia Mungu. Katika uzoefu wako, inaweza kuonekana kwamba watu wengi wanaamini ya kuwa kumhudumia Mungu kuna maana ya kueneza injili kwa bidii kwa ajili ya Mungu, kwenda barabarani kwa ajili ya Mungu, kutumia na kutoa sadaka kwa ajili ya Mungu, na kadhalika; hata zaidi, watu wa kidini huamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kukimbia hapa na pale wakiwa na Biblia mikononi mwao, wakieneza injili ya ufalme wa mbinguni na kuwaokoa watu kwa kuwafanya watubu na kuungama; kuna wakuu wengi wa kidini wanaofikiri kwamba kumhudumia Mungu ni kuhubiri makanisani baada ya kusoma katika chuo cha seminari, kuwafunza watu kwa kusoma sura za Biblia; ndugu zetu wengi huamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kukosa kuoa au kuolewa au kukuza familia, na kujitoa nafsi yao yote kwa Mungu; pia kuna watu katika maeneo ya umaskini wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kupokea uponyaji na kufukuza mapepo, au kuwaombea ndugu, au kuwahudumia; miongoni mwenu, kunao wengi wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kula na kunywa maneno ya Mungu, na kumwomba Mungu kila siku, na kutembelea makanisa kila mahali; na pia, kunao watu wanaosema kwamba kuishi maisha ya kanisa ni kumhudumia Mungu. Ilhali watu wachache wanajua maana ya kweli ya kumhudumia Mungu. Ingawa kunao wengi wanaomhudumia Mungu kama nyota angani, idadi ya wale wanaoweza kuhudumu moja kwa moja, na wanaoweza kutumikia mapenzi ya Mungu, ni hafifu—ndogo isiyo na maana. Kwa nini Ninasema hivi? Ninasema hivi kwa sababu wewe hufahamu kiini cha fungu la maneno “huduma kwa Mungu,” na unafahamu machache sana kuhusu jinsi ya kutumikia mapenzi ya Mungu. Leo, tunawasiliana hasa jinsi ya kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kuhudumu ili kutosheleza mapenzi ya Mungu.

Ikiwa ungependa kutumikia mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanapendwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza utaingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu. Na unapomhudumia ndipo Mungu atayapa nuru macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zao, kila upande ukipokea kutoka kwa uwezo wa wengine ili upungufu wao wenyewe, na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zao. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.

Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kupendwa na Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu atafanya hudhihirishwa kupitia kwa watu hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu. Ukishakuwa rafiki mwema wa Mungu ndipo utakapoweza kabisa kutawala pamoja na Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi