Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia! | Dondoo 341

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia! | Dondoo 341

112 |07/09/2020

Midomo yako ni mikarimu zaidi kuliko njiwa, lakini moyo wako ni mwovu zaidi kuliko yule nyoka wa zamani. Midomo yako ni ya kupendeza hata kama wanawake wa Lebanoni, lakini moyo wako si mwema zaidi kuliko yao, na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu mno! Vitu Ninavyochukia ni midomo na mioyo ya wadhalimu tu, na matakwa Yangu kwa watu si ya juu zaidi ya yale Ninayotarajia kutoka kwa watakatifu hata kidogo; ni kwamba tu Natiwa kinyaa kwa ajili ya matendo maovu ya wadhalimu, nami Natumai kwamba waweze kutupilia mbali uchafu wao na kutoroka kutoka katika hatari waliyomo sasa ili waweze kusimama kutoka kwa hao wadhalimu na wawe watakatifu na kuishi na wale ambao ni wenye haki. Ninyi mko katika hali sawa na Yangu, lakini mmejaa uchafu; hamna hata mfano kidogo zaidi wa asili wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo. Aidha, kwa sababu kila siku mnaiiga mifano ya hao roho wachafu, mkifanya kile wanachofanya na kusema kile wanachosema, kila sehemu yenu—hata ndimi na midomo yenu—imelowezwa katika maji yao machafu, kiasi kwamba mmejaa madoa kama hayo kabisa, na hakuna sehemu yenu hata moja inayoweza kutumika kwa ajili ya kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika dunia ya farasi na ng’ombe kabisa, lakini kwa kweli hamhisi kufadhaishwa; mmejaa furaha na mnaishi kwa uhuru na bila matatizo. Mnaogelea huku na kule katika maji hayo machafu, lakini kwa kweli hamtambui ya kwamba mmeingia katika hatari kama hiyo. Kila siku, mnaandamana na roho wachafu na kuingiliana na “kinyesi.” Maisha yenu ni ya kishenzi sana, ilhali hujui kweli kwamba haupo katika ulimwengu wa wanadamu kabisa na kwamba hujidhibiti. Je, hujui kwamba maisha yako yalikandamizwa na roho hao wachafu zamani, au kwamba tabia yako ilishachafuliwa na maji machafu zamani? Je, unafikiri kwamba unaishi katika paradiso ya duniani, na kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha pamoja na roho wachafu, na kwamba umeishi pamoja kwa amani na kila kitu ambacho wamekuandalia? Jinsi unavyoishi inawezaje kuwa na maana yoyote? Maisha yako yanawezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukikimbia huku na kule kwa ajili ya wazazi wako, wazazi wa roho wachafu, lakini hujui kweli kuwa wale wanaokutega ni hao wazazi wa roho wachafu waliokuzaa na kukukela. Aidha, huna habari kwamba kweli ni wao ndio waliokupa uchafu wako wote; kile unachojua tu ni kwamba wanaweza kukuletea “furaha”, hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hususani hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa hasira, lakini wanakutendea kwa upendo na fadhila. Maneno yao huusitawisha moyo wako na kukuvutia sana kiasi kwamba unakanganyikiwa, na bila kutambua, unafyonzwa na unakuwa tayari kuwahudumia, ukigeuka kuwa njia yao ya kutoka na kuwa mtumishi wao. Huna malalamiko hata kidogo, bali uko tayari kuwafanyia kazi kama mbwa, kama farasi; unadanganywa na wao. Kwa sababu hii, huna majibu yoyote kabisa kwa kazi Ninayoifanya. Si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kuponyoka kutoka Kwangu kwa siri, na si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kutumia maneno matamu kupata kibali kutoka Kwangu kwa njia danganyifu. Kama inavyotokea, tayari ulikuwa na mpango mwingine, na mpangilio mwingine. Unaweza kuona matendo Yangu kidogo kama mwenye Uweza, lakini huna ufahamu hata kidogo kuhusu hukumu na kuadibu Kwangu. Hujui kuadibu Kwangu kulianza lini; unajua tu jinsi ya kunidanganya—lakini hujui kwamba Sitastahimili ukiukaji wowote kutoka kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu anayechukia uovu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitavumilia kutoroka kwako mbele ya macho Yangu, wala Sitavumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo Kwangu Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kwa kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi