Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kufunua Mawazo ya Kidini | Dondoo 296

25/06/2020

Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Ni sehemu hizo tatu pekee ambazo zimefanywa moja ambazo ni Mungu kamili. Bila Baba Mtakatifu, Mungu asingekuwa mkamilifu. Vivyo hivyo, wala Mungu asingekuwa mkamilifu bila Mwana au Roho Mtakatifu. Katika mawazo yao, wanaamini kuwa Baba au Mwana pekee hawezi kuwa Mungu. Ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu tu kwa pamoja wanaoweza kuwa Mungu Mwenyewe. Sasa, waumini wote wa kidini, akiwemo kila mfuasi miongoni mwenu, anashikilia hii imani. Ilhali, ikiwa hii imani ni sahihi, hakuna anayeweza kuelezea, kwani daima mmechanganyikiwa kuhusu masuala ya Mungu Mwenyewe. Japo hizi ni fikra tu, hamjui kama ni sawa au mbaya, kwani mmeathiriwa vibaya na mawazo ya kidini. Mmeyakubali kwa kina haya mawazo ya kidini yaliyozoeleka, na hii sumu imezama kwa kina ndani yenu. Hivyo basi, hata kwa hili mmeanguka katika huu ushawishi wenye madhara, kwani Utatu haupo. Yaani, Utatu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu haupo. Hizi zote ni fikra za kawaida za mwanadamu, na imani za uongo za mwanadamu. Kwa karne nyingi, mwanadamu ameamini katika huu Utatu, ambao umebuniwa na mawazo katika akili za mwanadamu, ukatengenezwa na mwanadamu, na ambao haujawahi kuonekana na mwanadamu. Kwa miaka mingi, kumekuwa na watu maarufu wa kiroho ambao wameeleza “maana ya kweli” ya Utatu, ila maelezo hayo ya Utatu kama nafsi tatu dhahiri yamekuwa si yakini na hayapo wazi na yote yamepumbazwa na “ujenzi” wa Mungu. Hakuna mtu maarufu yeyote aliyewahi kutoa maelezo kamili; maelezo mengi yanafaa katika masuala ya mjadala na katika maandishi, ila hakuna hata mtu mmoja ambaye ana ufahamu kamili na wa wazi kuhusu maana ya Utatu. Hii ni kwa sababu huu Utatu huu mkuu ambao mwanadamu anashikilia moyoni kwa hakika haupo. Kwani hakuna aliyewahi kuiona sura ya Mungu au kubahatika kumtembelea katika makao Yake ili kuchunguza ni vitu gani vipo mahali ambapo Mungu anakaa, kubainisha wazi ni makumi mangapi ya maelfu, au mamia ya mamilioni ya vizazi yako katika “nyumba ya Mungu” au hata kuchunguza ni sehemu ngapi zimeuunga mwili wa asili wa Mungu, Kinachofaa hasa kuchunguzwa ni: umri wa Baba na Mwana, na vilevile Roho Mtakatifu; umbo la kila mmoja; hasa ni vipi Wanajitenganisha, na ni vipi Wanafanywa kuwa kitu kimoja. Kwa bahati mbaya, katika miaka hii yote, hakuna hata mtu mmoja ambaye ameweza kugundua ukweli wa haya mambo. Wote wanabuni tu, kwani hakuna hata mtu mmoja aliyewahi kwenda mbinguni kwa matembezi na kurejea na “ripoti ya uchunguzi” kwa wanadamu wote ili kuripoti kuhusu ukweli wa mambo kwa wale waumini wote wa kidini wenye bidii na wacha Mungu wanaojishughulisha sana na Utatu Mtakatifu. Bila shaka, mwanadamu hawezi kulaumiwa kwa kubuni na fikra hizo, maana kwa nini Yehova Baba hakuambatana na Yesu Mwana alipomuumba mwanadamu? Ingekuwa hapo mwanzoni kuwa wote waliitwa Yehova, ingekuwa bora zaidi. Ikiwa kuna wa kulaumiwa, wacha lawama iwe kwa kuteleza kwa muda kwa Yehova Mungu, ambaye hakuwaita Mwana na Roho Mtakatifu mbele Zake wakati wa uumbaji, ila badala yake Akafanya kazi Yake peke Yake. Ikiwa Wote Wangefanya kazi wakati mmoja, basi wasingekuwa kitu kimoja? Ikiwa, tangu mwanzo kabisa hadi mwisho, kungekuwa na jina moja tu Yehova pasipo jina la Yesu tangu Enzi ya Neema, au ikiwa Angeitwa bado Yehova, je, Mungu asingeepushiwa na wanadamu taabu ya huu utengano? Kwa hakika, Yehova hawezi kulaumiwa kwa haya yote; kama ni lawama, hebu na iwekwe kwa Roho Mtakatifu, ambaye kwa maelfu ya miaka Aliendelea na kazi yake kwa jina la Yehova, la Yesu, na hata la Roho Mtakatifu, Akiwachanganya na kuwakanganya wanadamu kiasi kwamba wanadamu wakashindwa kufahamu Mungu ni nani hasa. Iwapo Roho Mtakatifu angefanya kazi bila umbo au sura, aidha, bila jina kama vile Yesu, na mwanadamu asingemgusa wala kumuona, ila kusikia tu ngurumo za radi, basi si kazi hiyo ingekuwa ya manufaa zaidi kwa mwanadamu? Hivyo nini kinaweza kufanywa sasa? Fikra za mwanadamu zimerundikana juu kama mlima na kuenea kama bahari, kiasi kwamba Mungu wa sasa hawezi kuzistahimili kamwe na hajui la kufanya. Hapo nyuma wakati kulikuwa tu na Yehova, Yesu, na Roho Mtakatifu katikati ya hao wawili, mwanadamu tayari alikuwa amechanganyikiwa na jinsi ya kuvumilia, na sasa kuna ongezeko la mwenye Uweza, ambaye hata anasemekana kuwa sehemu ya Mungu. Ni nani anajua Yeye ni nani na Ameingiliana au kujificha kwa nani katika Utatu Mtakatifu kwa miaka mingapi? Mwanadamu anawezaje kulistahimili hili? Utatu Mtakatifu pekee ulitosha kumchukua mwanadamu milele kuueleza, lakini sasa kuna “Mungu mmoja katika nafsi nne.” Hili linaweza kuelezewa vipi? Unaweza kulieleza? Ndugu na dada! Mmeaminije katika Mungu huyu mpaka leo? Ninawavulia kofia. Utatu uliweza kuvumilika, na bado mnaendelea kuwa na imani isiyotikisika kwa huyu Mungu mmoja katika nafsi nne. Mmehimizwa muondoke na bado mnakataa. Ajabu iliyoje! Nyinyi ni watu wa ajabu! Mtu kweli anaweza kuendelea kuamini Mungu wanne na asiwaelewe; hamuoni kuwa huu ni muujiza? Sikujua kwamba mlikuwa na uwezo wa kutenda muujiza mkubwa kiasi hiki! Hebu Niwaambie hilo, kwa hakika, Utatu Mtakatifu haupo popote katika dunia hii. Mungu hana Baba wala Mwana, vivyo hivyo hakuna dhana ya chombo kitumiwacho kwa pamoja na Baba na Mwana: Roho Mtakatifu. Huu wote ni uongo mkubwa na haupo kabisa katika dunia hii! Hata hivyo uongo huu una asili yake na haukosi msingi kabisa, kwani akili zenu si punguani, na mawazo yenu hayakosi mantiki. Badala yake, ziko sawa na yenye ubunifu kwa kiasi kikubwa, kwamba haziwezi kuzuiwa hata na Shetani yeyote. La kusikitisha ni kwamba mawazo haya ni uongo mtupu na hayapo kabisa! Hamjaona ukweli halisi haswa; mnabuni na kujiundia dhana, na kuzitengeneza kuwa hadithi ili kuteka imani ya wengine kwa uongo na kupata mamlaka miongoni mwa wanadamu wapumbavu wasio na busara, ili kwamba waamini katika “mafundisho yenu ya kitaaluma” makuu na mashuhuri. Je, huu ni ukweli? Je, hii ndiyo njia ya uzima ambayo wanadamu wanafaa kupokea? Huu ni upuuzi! Hakuna hata neno moja linafaa! Katika miaka hii yote, nyinyi mmegawanya Mungu namna hii, na kuendelea kugawanywa zaidi katika kila kizazi kiasi kwamba Mungu mmoja amegawanywa kuwa Mungu watatu. Na sasa haiwezekani kabisa kwa mwanadamu kumuunganisha Mungu kuwa mmoja kwani mmemgawanya zaidi. Ingekuwa si kazi yangu ya upesiupesi kabla ya muda kuyoyoma, haijulikani mngeishi hivi kwa muda gani! Kuendelea kumgawanya Mungu namna hii, Anawezaje kuendelea kuwa Mungu wenu? Je, bado mngeendelea kumtambua Mungu? Je, bado mngemrudia? Ningechelewa hata kidogo, inaonekana kwamba mngewarudisha “Baba na Mwana,” Yehova na Yesu kwenda Israeli na mdai kwamba nyinyi wenyewe ni sehemu ya Mungu. Kwa bahati nzuri, sasa ni siku za mwisho. Hatimaye, siku Niliyoitarajia kwa hamu imewadia, na ni baada tu ya kuifanya hatua hii ya kazi kwa mikono Yangu ndipo kumgawanya kwenu Mungu Mwenyewe kumesitishwa. Isingekuwa hivi, mngezidisha, hadi kuwaweka Mashetani wote miongoni mwenu kwenye madhabahu kwa ibada. Hii ndiyo njama yenu! Mbinu yenu ya kumgawanya Mungu! Je, mtaendelea kufanya hivyo sasa? Hebu Niwaulize: Kuna Mungu Wangapi? Ni Mungu Yupi atawaletea wokovu? Je, ni Mungu wa kwanza, wa pili au wa tatu mnayemwomba? Ni nani kati Yao mnayemwamini? Je, ni Baba? Au ni Mwana? Au ni Roho? Niambie ni nani unayemwamini. Ijapokuwa kwa kila neno unasema unamwamini Mungu, mnachokiamini hasa ni akili zenu! Hamna Mungu mioyoni mwenu kabisa! Na bado akilini mwenu mna “Utatu Mtakatifu” kadhaa. Hamkubaliani na hili?

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp