Tenzi ya Rohoni | Fuata Maneno ya Mungu na Huwezi Kupotea (Music Video)

15/07/2020

Mungu anatumaini mnaweza kula na kunywa peke yenu,

na kila wakati muishi katika nuru ya uwepo wa Mungu,

na kwa njia mnayoishi, kamwe msiyaache maneno ya Mungu;

hapo tu ndipo mtakapoweza kujazwa na maneno ya Mungu.

Katika kila neno na tendo lako,

maneno ya Mungu hakika yatakuongoza mbele.

Ukimkaribia Mungu kwa dhati kwa kiwango hiki,

utaweza kuwasiliana na Mungu kila wakati,

na hakuna chochote ufanyacho kitakachoishia katika mkanganyiko

au kukuacha ukihisi usiyejua chochote.

Bila shaka utaweza kuwa na Mungu upande wako,

utaweza daima kutenda kulingana na neno la Mungu.

Bila shaka utaweza kuwa na Mungu upande wako,

utaweza daima kutenda kulingana na neno la Mungu.

Na kila mtu, jambo, na kitu unachokutana nacho,

neno la Mungu litakuonekania wakati wowote,

likikuongoza utende kulingana na mapenzi Yake.

Fanya kila kitu katika neno la Mungu,

na Mungu atakuongoza mbele katika kila kitendo chako;

hutapotea kamwe,

na utaweza kuishi katika nuru mpya,

na nuru mpya na nyingi zaidi.

Huwezi kutumia mawazo ya kibinadamu kufikira kuhusu cha kufanya;

unapaswa kutii mwongozo wa neno la Mungu,

uwe na moyo safi,

uwe kimya mbele za Mungu, na utafakari zaidi.

Usifadhaike kuhusu suluhisho kwa kile usichoelewa;

yalete mambo kama hayo mbele za Mungu mara nyingi,

na umtoelee moyo wa dhati.

Amini kuwa Mungu ndiye mwenyezi wako!

Lazima uwe na azimio kubwa kwa Mungu,

ukitafuta kwa nguvu huku ukikataa

visingizio, nia, na hila za Shetani.

Usikate tamaa. Usiwe dhaifu.

Tafuta kwa moyo wako wote; subiri kwa moyo wako wote.

Shirikiana kwa vitendo na Mungu,

na ujiondolee vikwazo vyako vya ndani.

Amini kuwa Mungu ndiye mwenyezi wako!

Lazima uwe na azimio kubwa kwa Mungu,

ukitafuta kwa nguvu huku ukikataa

visingizio, nia, na hila za Shetani.

Usikate tamaa. Usiwe dhaifu.

Tafuta kwa moyo wako wote; subiri kwa moyo wako wote.

Shirikiana kwa vitendo na Mungu,

na ujiondolee vikwazo vyako vya ndani.

Shirikiana kwa vitendo na Mungu,

na ujiondolee vikwazo vyako vya ndani.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp