Filamu za Kikristo "Ukuaji" A Touching Testimony of Faith

09/07/2023

Liang Xinjing ni Mkristo ambaye anaishi maisha yenye furaha pamoja na mume na binti yake. Lakini kwa sababu ya jitihada nyingi za Chama cha Kikomunisti cha China za kuwatesa na kuwakamata waumini, mume wake anaanza kujaribu kuzuia imani yake, akihofia kwamba atafungwa, na kisha uwezekano wake wa kupandishwa cheo utaathiriwa. Liang Xinjing bado anasalia imara katika azimio lake la kumfuata Mungu, hata mume wake anapotumia ukali na hatimaye kusisitiza kutaka talaka. Muda mfupi baada ya kutalikiana, Chama cha Kikomunisti kinaanzisha operesheni nyingine kubwa ya kuwakamata Wakristo, na Liang Xinjing analazimika kukimbia eneo hilo. Polisi na watumishi wao wa "vikosi vya ukanda mwekundu" wanaendelea kumhoji na kumtishia bintiye, wakitaka kujua aliko. Binti yake anapata saratani ya limfu kwa sababu ya kuishi katika hali ya hofu na wasiwasi siku zote. Liang Xinjing anapopata habari hii, anazama katika hali ya kukata tamaa kabisa. Anamwomba na kumtegemea Mungu vipi ili kushinda dhiki hii, jaribu hili? Anajifunza nini kutokana nalo? Tazama Ukuaji ili ujue.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp