Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Swahili Christian Testimony Video "Katikati ya Majira ya Baridi"

Mateso ya Kidini   1251  

Utambulisho

Jina lake ni Xiao Li. Ameamini katika Mungu kwa zaidi ya muongo mmoja. Katika majira ya baridi ya mwaka wa 2012, alikamatwa na polisi wa Kikomunisti wa China katika mkutano. Wakati wa mahojiano, polisi walimshawishi, kumtisha, kumpiga na kumtesa tena na tena katika majaribio yao ya kumshawishi ili amsaliti Mungu kwa kufichua walipokuwa viongozi na fedha za kanisa. Hasa katika usiku mmoja baridi sana wakati ambapo halijoto ilikuwa nyuzi ishirini chini ya sifuri, alivuliwa nguo kwa nguvu akawa uchi, akaroweshwa maji ya barafu, akashtuliwa kwa umeme kwenye viungo vyake vya uzazi, na kunyweshwa maji ya haradali kwa nguvu na polisi... Alikuwa amepitia mateso ya kikatili na fedheha isiyowazika. Wakati wa mahojiano, alihisi kuumizwa na kudhalilishwa. Alimwomba Mungu bila tumaini muda baada ya muda. Neno la Mungu lilimpa nuru na mwongozo wa wakati wa kufaa. Kwa imani na nguvu aliyopata kutoka kwa neno la Mungu, alishinda mateso makali na maangamizi ya kishetani na akatoa ushuhuda mzuri sana wa kuenea pote. Kama maua ya plamu ya majira ya baridi, yeye alionyeshwa nguvu thabiti kwa kusitawi kwa fahari katikati ya dhiki kali, akitoa kumbukumbu ya kupendeza sana...

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu

Pakua Programu Bila Malipo

Video za Ajabu Zakuongoza Kuielewa Kazi ya Mungu