Wimbo wa Injili | Sote Tuweze Kujua Uzuri wa Mungu (Music Video) | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Mungu atupe nuru, ili kwamba sote tuweze kujua uzuri Wake, tumpende Mungu wetu katika kina cha mioyo yetu, na kuonyesha upendo ambao sote tunao kwa Mungu katika nafasi zetu mbalimbali; Mungu atukirimu mioyo thabiti yenye upendo wa kweli Kwake—hili ndilo analotarajia Mungu. Sisi tuliozaliwa katika nchi hii ya uchafu tumeteseka sana kutokana na mateso ya joka kuu jekundu, na hivyo tukapata chuki kwake. Linazuia mioyo yetu impendayo Mungu na kuvutia kwa hila tamaa yetu ya matazamio ya baadaye. Linatushawishi kuwa hasi, kumpinga Mungu. Ni joka kuu jekundu ambalo limeharibu, limetupotosha, na kutuangamiza mpaka sasa, kufikia hatua kwamba hatuwezi kulipa upendo wa Mungu kwa mioyo yetu na, ingawa tunataka kumpenda Mungu mioyoni mwetu, hatuna udhibiti wa matendo yetu wenyewe na hatuna nguvu hata kidogo.

2

Sisi tuliozaliwa katika nchi hii ya uchafu tumeteseka sana kutokana na mateso ya joka kuu jekundu. Sisi sote ni waathirika wake. Kwa sababu hii, tunalichukia kabisa, na tunaweza tu kumngojea Mungu aliangamize. Tunapaswa kupania kufuata mapenzi ya Mungu—kumpenda Yeye. Hii ndiyo njia tunayopaswa kuitembea. Ndiyo jinsi tunavyopaswa kuishi maisha yetu. Ni lazima tufanye kufuata mapenzi ya Mungu kuwa lengo letu, na tuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, yenye kung'aa na matukufu. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kufa bila majuto—ni kwa kufanya hivi tu ndiyo tutahisi kupata faraja mioyoni mwetu. Mungu atupe nuru, ili kwamba sote tuweze kujua uzuri Wake, tumpende Mungu wetu katika kina cha mioyo yetu, na kuonyesha upendo ambao sote tunao kwa Mungu katika nafasi zetu mbalimbali; Mungu atukirimu mioyo thabiti yenye upendo wa kweli Kwake.

kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia … (2)

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp