Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 110

24/07/2020

Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.

Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake maovu. Kati ya vitendo vyote vya maovu ambavyo Shetani ametekeleza kwa binadamu—tangu jitihada zake za mapema za kudanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, na ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kutambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua hali halisi ya uovu wa Shetani; hakuna hata moja inayoshindwa kuthibitisha hoja kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata moja hushindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inasalimisha maovu yake, inadumisha maendelezo ya vitendo vyake vya maovu, inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Wao ni katili kwa Mungu, na ndio wale ambao hasira ya Mungu itaangamiza. Ingawaje Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake kali ni mbinu ya kutoa nje asili yake mbovu. Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila matumizi ya hasira ya Mungu huwa yanafichua sura halisi ya aibu ya Shetani; na pia kufichua na kuweka kwenye nuru matamanio ya maovu ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Kule kulipuka kwa hasira kali ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huwa ni ishara ya ulinzi na maendelezo ya mambo mazuri, na huwa ni ishara ya asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp