Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 146

14/06/2020

Kuijua kazi ya Mungu si kazi rahisi: Unapaswa kuwa na viwango na malengo katika utafutaji wako, unapaswa kujua jinsi ya kutafuta njia ya kweli, na jinsi ya kupima kujua kama ni njia ya kweli au si ya kweli, na kama ni kazi ya Mungu au kinyume chake. Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la, iwapo maneno haya ni maonyesho wa ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu kwa Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake kwa Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni silika ya maisha ya ubinadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alikitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inampeleka mwanadamu katika maisha ya ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisia wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni kama mwanadamu ana maarifa mengi juu ya Mungu, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yake au la, na kumsogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili inaweza kupimwa kama ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisia badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama hukubaliani na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli. Ninasema maneno haya si kukufanya ukubali njia nyingine katika uzoefu utakaoupitia baadaye, wala si utabiri kwamba kutakuwa na kazi ya enzi nyingine mpya hapo baadaye. Ninayasema ili uweze kuwa na uhakika kwamba kazi ya leo ni kazi ya kweli, ili kwamba usiwe na uhakika nusu katika imani yako kwa kazi ya leo na kushindwa kuielewa kwa ndani. Kuna watu wengi ambao, licha ya kuwa na uhakika, bado wanafuata kwa mkanganyiko; uhakika kama huo hauna kanuni, na wanapaswa kuondolewa mapema. Hata wale ambao wapo motomoto katika imani yao wanakuwa na uhakika katika mambo matatu na mambo matano wanakuwa hawana uhakika, kitu kinachoonyesha kuwa hawana msingi. Kwa sababu tabia yako ni dhaifu sana na msingi wako hauna kina, hivyo huna uelewa wa kutofautisha. Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisia, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo ipo juu ya uelewa wa mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya uelewa wa kawaida wa mwanadamu, na haipitilizi ulelewa wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida kabisa, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake, ambayo yameharibiwa na Shetani, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Ni sawa na, kusema, maisha ya mwanadamu yanakuwa na kukua, na tabia ya upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha tabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa uelewa wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu. Umeamini katika Mungu kwa miaka yote hii, halafu bado huna uwezo wa kutofautisha kati ya njia ya kweli na njia ya uongo au kuweza kuitafuta njia ya kweli. Watu wengi hawapendi hata kusikia masuala haya; wanakwenda tu kule ambapo wengi wanakwenda, na wanarudia kile ambacho watu wengi wanasema. Ni kwa njia gani mtu huyu ni mtu anayetafuta njia ya kweli? Na ni kwa njia gani watu kama hao wanaweza kuipata njia ya kweli? Ikiwa utaelewa kanuni hizi muhimu, basi chochote kitakachotokea hutaweza kudanganywa. Leo, ni muhimu sana kwamba mwanadamu awe na uwezo wa kutofautisha mambo; hiki ndicho kinapaswa kuwa katika ubinadamu wa kawaida, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuwa nacho katika uzoefu wake. Ikiwa hata leo, mwanadamu bado hawezi kutofautisha kitu katika utafutaji wake wa ukweli, na hisia zake za kibinadamu bado hazikui, basi mwanadamu ni mpumbavu sana, na njia yake ni makosa na imepotoka. Hakuna tofauti hata ndogo katika maisha yako leo, na ingawa ni ukweli, kama unavyosema, umepata njia ya kweli, ni kweli umeipata? Umeweza kuwa na uwezo wa kutofautisha kitu chochote? Kiini cha njia ya kweli ni nini? Katika njia ya kweli, bado hujapata njia ya kweli, hujapata kitu chochote cha ukweli, ni sawa na kusema, hujapata kile ambacho Mungu anakitaka kwako, hivyo hakuna tofauti katika upotovu wako. Kama utaendelea kuwa katika njia hii, hatimaye utaondolewa. Kwa kuwa umefuata mpaka wa leo, inapaswa uwe na uhakika kwamba njia uliyoichukua ni njia sahihi, na hupaswi kuwa na mashaka sana. Watu wengi siku zote wanakuwa hawana uhakika na wanashindwa kufuata ukweli kwa sababu ya masuala fulani madogomadogo. Watu kama hao ni wale ambao hawana maarifa na kazi ya Mungu, ni wale ambao wanamfuata Mungu katika mkanganyiko. Watu ambao hawaijui kazi ya Mungu hawawezi kuwa wandani Wake, au kuwa na ushuhuda Wake. Ninawashauri wale ambao wanatafuta tu baraka na kufuata kile ambacho si dhahiri na dhahania kutafuta ukweli mapema iwezekanavyo, ili kwamba maisha yao yawe na maana. Msiendelee kujidanganya!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp