Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 147

23/07/2020

Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji. Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda, ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima. Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi yake yote ilifanywa bila kupangwa. Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi ya miaka elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Binadamu kabla ya kuumba ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaeleza moja kwa moja kile Alicho; Hachemshi bongo kuunda mpango. Bila shaka, manabii wengi wameongelea unabii mwingi, lakini bado haiwezi kusemekana kwamba kazi ya Mungu siku zote imekuwa ya upangaji mpango wa dhati; unabii ulitolewa kulingana na kazi halisi ya Mungu. Kazi zake zote ni kazi halisi zaidi. Hutekeleza kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo Kwake Yeye, kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kwa ugonjwa; Anafanya uangalizi wakati akifanya kazi Yake; Anafanya kazi kulingana na uangalizi Wake. Katika kila awamu ya kazi Yake, Anaweza kuelezea hekima Yake tosha na kuelezea uwezo Wake tosha; Anafichua hekima Yake tosha na mamlaka Yake tosha kulingana na kazi ya enzi hiyo husika na kuruhusu watu wowote wale waliorudishwa na Yeye wakati wa enzi hizo kuweza kuiona tabia Yake nzima. Anawaruzuku watu na kutekeleza kazi Anayofaa kufanya kulingana na kazi ambayo lazima ifanywe katika enzi husika; Anawaruzuku watu kulingana na kiwango ambacho Shetani amewapotosha. Ilikuwa ni njia hii wakati Yehova aliweza kuwaumba mwanzo Adamu na Hawa ili kuwaruhusu kumdhihirisha Mungu katika nchi na kuwa na mashahidi wa Mungu miongoni mwa uumbaji, lakini Hawa alitenda dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka; Adamu alifanya vivyo hivyo, na kwa pamoja wakiwa kwenye bustani wakalila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hivyo basi, Yehova alikuwa na kazi ya ziada ya kutenda miongoni mwao. Aliuona uchi wao na kuifunika mili yao kwa nguo ziliyotengenezwa kutoka kwenye ngozi za wanyama. Kufuatia haya, Alimwambia Adamu “Kwa sababu umesikiliza sauti ya mkeo, na umekula kutoka kwa mti ule, ambao Nilikuamuru, nikisema, usile kutoka kwa mti huo: udongo umelaaniwa kwa sababu yako … mpaka urudi udongoni; kwani ulitolewa hapo: kwa kuwa wewe ni mavumbi, na utarudi mavumbini.” Kwa mwanamke Akasema, “Nitazidisha mara dufu maumivu yako na kupata kwako watoto; kwa maumivu utazaa wana; na tamaa yako itakuwa kwa mume wako, na yeye atatawala juu yako.” Kuanzia hapo aliwafukuza kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuwafanya kuishi nje ya bustani, kama vile binadamu wa kisasa afanyavyo sasa nchini. Wakati Mungu alipomwumba mwanadamu mwanzoni kabisa, Hakupanga kumfanya binadamu kujaribiwa na nyoka baada ya kuumbwa na kisha kuwalaani binadamu na nyoka. Kwa hakika hakuwa na mpango wa aina hii; ilikuwa tu maendeleo ya mambo yaliyompa kazi hii mpya miongoni mwa uumbaji Wake. Baada ya Yehova kutekeleza kazi Yake miongoni mwa Adamu na Hawa kwenye ardhi, binadamu waliendelea kuimarika kwa miaka elfu kadhaa, mpaka “Yehova akaona ya kwamba uovu wa mwanadamu ni mkuu ulimwenguni, na kuwa kila wazo la fikira za moyo wake ni ovu pekee daima. Na ikamghairi Yehova kwa sababu alikuwa amemfanya mwanadamu ulimwenguni, na ikamhuzunisha moyoni. … Ila Nuhu alipata neema katika macho ya Yehova.” Wakati huu Yehova alikuwa na kazi mpya zaidi, kwa ajili binadamu Aliowaumba ulikuwa umezidisha dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka. Kwa mujibu wa hali hizi, Yehova aliichagua familia ya Nuhu kutoka miongoni mwa watu hawa na kuwanusuru, na kutekeleza kazi Yake ya kuuangamiza ulimwengu kwa gharika. Binadamu wameendelea kukua kwa njia hii mpaka siku ya leo, wakiendelea kupotoka pakubwa, na wakati maendeleo ya binadamu yafikapo kilele, utakuwa ndio mwisho wa binadamu. Kuanzia mwanzo kabisa hadi mwisho wa ulimwengu, ukweli wa ndani wa kazi Yake siku zote umekuwa hivi. Itakuwa sawa na namna ambavyo binadamu atakavyoainisha kulingana na aina yake; mbali na kila mtu anayeamuliwa kabla kwa kundi kinachomfaa mwanzoni kabisa, watu wanawekwa kwenye kategoria kwa utaratibu baada ya kupitia mchakato wa maendeleo. Mwishowe, yeyote ambaye hawezi kuokolewa kwa uzima atarudishwa kwa mababu zake. Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa binadamu iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni mwa binadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo ambalo alikuwa ameliamulia kimakusudi awali; mtu anaweza kusema kwamba hali hii haikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya haya ndiyo Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali. “Hekima Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi ambavyo binadamu walizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; binadamu wamekuwa wakipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka sasa. Baada ya binadamu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayepotosha binadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajauruhusu tu binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia amewaruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atawaruhusu binadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu wenye maovu na kuwatuza wenye wema. Amepigana na Shetani hadi siku hii ya leo na Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo basi mbali na kufanya tu kila kitu mbinguni kunyenyekea kwa mamlaka Yake; pia Hufanya kila kitu nchini kupumzika chini ya kigonda Chake, na pia Huwafanya wale watenda maovu wanaoshambulia na kunyanyasa binadamu kujipata katika kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake. Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa binadamu, kwani Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya nchi, au kwenye ulimwengu kwa ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti Yeye, Aliwaumba binadamu kwenye nchi, na ilikuwa ni kwa sababu ya binadamu ndiyo Alianza rasmi vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na nchini huweza kushuhudia hekima ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule ukweli wa ndani katika kila awamu ya kazi, kuweza kuona hasa ni vipi unaweza kuelezea ule uweza wa Mungu na hasa ni vipi unavyoweza kuelezea ule uhalisia wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp