Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kujua Kazi ya Mungu | Dondoo 181

24/06/2020

Kazi ambayo Mungu anafanya haiwakilishi uzoefu wa mwili Wake; kazi ambayo mwanadamu anafanya inawakalisha uzoefu wa mwanadamu. Kila mtu anazungumza juu ya uzoefu wake binafsi. Mungu Anaweza kuonyesha ukweli moja kwa moja, wakati mwanadamu anaweza tu kuonyesha uzoefu unaolingana na huo baada ya kupata uzoefu wa ukweli. Kazi ya Mungu haina masharti na haifungwi na muda au mipaka ya kijiografia. Anaweza kudhihirisha kile Alicho wakati wowote, mahali popote. Anafanya kazi vile Anavyopenda. Kazi ya mwanadamu ina masharti na muktadha; vinginevyo hana uwezo wa kufanya kazi na hawezi kudhihirisha uelewa wake wa Mungu au uzoefu wake wa ukweli. Unatakiwa tu kulinganisha tofauti baina yao ili kuonyesha kama ni kazi ya Mungu mwenyewe au kazi ya mwanadamu. Kama hakuna kazi inayofanywa na Mungu Mwenyewe, na kuna kazi tu ya mwanadamu, utajua kwamba mafundisho ya mwanadamu ni makuu, zaidi ya uwezo wa mtu yeyote yule; toni yao ya kuzungumza, kanuni zao katika kushughulikia mambo na uwezo wao katika kufanya kazi ni zaidi ya uwezo wa wengine. Nyinyi wote mnawatamani watu hawa wenye ubinadamu wa juu, lakini huwezi kuona kutoka katika kazi na maneno ya Mungu jinsi ubinadamu Wake ulivyo wa juu. Badala yake, Yeye ni wa kawaida, na Anapofanya kazi, Yeye ni wa kawaida na halisi lakini pia hapimiki kwa watu wenye mwili wa kufa, kitu ambacho kinawafanya watu wahisi kumheshimu sana. Pengine uzoefu wa mtu katika kazi yake ni mkubwa sana, au dhana na fikra zake ni za juu sana, na ubinadamu wake ni mzuri hasa; hivi vinaweza kutamaniwa na watu tu, lakini visiamshe kicho na hofu yao. Watu wote wanawatamani wale ambao wana uwezo wa kufanya kazi na ambao wana uzoefu wa kina na wanaweza kuutenda ukweli, lakini hawawezi kuvuta kicho, bali kutamani na kijicho. Lakini watu ambao wamepitia uzoefu wa kazi ya Mungu hawamtamani Mungu, badala yake wanahisi kwamba kazi Yake haiwezi kufikiwa na mwanadamu na haiwezi kueleweka na mwanadamu, na kwamba ni nzuri na ya kushangaza. Watu wanapopitia uzoefu wa kazi ya Mungu, uelewa wao wa kwanza kuhusu Yeye ni kwamba Hawezi kueleweka, ni mwenye hekima na wa ajabu na wanamheshimu bila kujitambua na kuihisi siri ya kazi Anayoifanya, ambayo inapita akili ya mwanadamu. Watu wanataka tu kuwa na uwezo wa kukidhi matakwa Yake, kuridhisha matamanio Yake; hawatamani kumpita Yeye, kwa sababu kazi anayoifanya inakwenda zaidi ya fikra za mwanadamu na haiwezi kufanywa na mwanadamu kama mbadala. Hata mwanadamu mwenyewe hayajui mapungufu yake, wakati Amefungua njia mpya na kumleta mwanadamu katika dunia mpya zaidi na nzuri zaidi, ili mwanadamu awe na mwendelezo mpya na kuwa na mwanzo mpya. Kile ambacho mwanadamu anakihisi kwa ajili Yake, sio matamanio, au sio matamanio tu. Uzoefu wao wa kina ni kicho na upendo, hisia zao ni kwamba Mungu kweli ni wa ajabu sana. Anafanya kazi ambayo mwanadamu hawezi kufanya, Husema vitu ambavyo mwanadamu hawezi kuvisema. Watu ambao wamepitia uzoefu wa kazi Yake siku zote hupitia uzoefu wa hisia isiyoweza kuelezeka. Watu wenye uzoefu wa kina hasa wanampenda Mungu. Siku zote wanahisi upendo Wake, wanahisi kwamba kazi Yake ni ya hekima sana, ni ya kushangaza sana, na hivyo hii inazalisha nguvu isiyokoma ndani yao. Si woga au upendo wa mara moja moja na heshima, bali hisia za ndani za upendo wa Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Hata hivyo, watu ambao wamepata uzoefu wa kuadibu Kwake na hukumu wanamhisi Yeye kuwa mtukufu na wa heshima. Hata watu ambao wamepitia uzoefu mkubwa wa kazi Yake pia hawawezi kumwelewa; watu wote wanaomheshimu wanajua kwamba kazi Yake hailingani na mitazamo ya watu lakini siku zote inakwenda kinyume na mitazamo yao. Haihitaji watu kumtamani kabisa au kuwa na mwonekano wa kujikabidhi Kwake, badala yake anataka wawe na heshima ya kweli na kujikabidhi kikamilifu. Katika nyingi ya kazi Yake, mtu yeyote mwenye uzoefu wa kweli anahisi heshima Kwake, ambayo ni ya juu kuliko matamanio. Watu wameiona tabia Yake kwa sababu ya kazi Yake ya kuadibu na hukumu, na kwa hiyo wanamcha mioyoni mwao. Mungu anapaswa kuchiwa na kutiiwa, kwa sababu uungu Wake na tabia Yake havifanani kama ule wa watu walioumbwa na vikuu juu ya vile vya watu walioumbwa. Mungu sio kiumbe Aliyeumbwa, na ni Yeye tu anayestahili kuchiwa na heshima na taadhima; mwanadamu hana sifa ya kupewa hivi. Hivyo, watu wote waliopitia uzoefu wa kazi Yake na kweli wanamjua wanampatia heshima. Hata hivyo, wale ambao hawaachani na mitazamo yao kuhusu Yeye, yaani, wale ambao hawamwoni Yeye kuwa Mungu, hawana uchaji wowote Kwake, na hata kama wanamfuata hawajashindwa; ni watu wasiotii kwa asili yao. Anafanya kazi hii ili kupata matokeo kwamba viumbe vyote vilivyoumbwa vinaweza kumcha Muumbaji, vimwabudu Yeye, na kujikabidhi katika utawala Wake bila masharti. Haya ni matokeo ya mwisho ambayo kazi Yake yote inalenga kuyapata. Ikiwa watu ambao wamepitia kazi hiyo hawamheshimu Mungu, hata kidogo, kama kutotii kwao kwa zamani hakutabadilika kabisa, basi watu hawa ni hakika wataondolewa. Kama mtazamo wa mwanadamu kwa Mungu ni kumtamani au kuonyesha heshima kwa mbali na sio kumpenda, hata kidogo, hivi ndivyo mtu bila moyo wa kumpenda Mungu anapofikia, na mtu wa aina hiyo anakosa hali za kumwezesha kukamilishwa. Ikiwa kazi kubwa sana hivi inashindwa kupata upendo wa kweli wa mtu, hii ina maana kwamba mtu huyo hajampata Mungu na kwa uhalisia hatafuti kuujua ukweli. Mtu ambaye hampendi Mungu hapendi ukweli na hivyo hawezi kumpata Mungu, achilia mbali kupata ukubali wa Mungu. Watu kama hao, bila kujali ni kwa kiasi gani wanapata uzoefu wa Roho Mtakatifu, na bila kujali jinsi gani wanapitia uzoefu wa hukumu, bado hawawezi kumcha Mungu. Hawa ni watu ambao asili yao haiwezi kubadilishwa, ambao wana tabia ya uovu uliokithiri. Wale wote ambao hawamchi Mungu wataondolewa, na kuwa walengwa wa hukumu, na kuadhibiwa kama tu wale ambao wanafanya uovu, watateseka hata zaidi ya wale ambao wamefanya matendo ambayo si ya haki.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp