Ushuhuda wa Kikristo | Kukombolewa Kutokana na Umaarufu na Utajiri

18/08/2020

Mhusika mkuu ni kiongozi wa kanisa ambaye anakuwa na wivu anapoona kuwa Dada Xia, mwenzi wake katika wajibu wake, hushiriki ushirika bora juu ya ukweli kumliko yeye. Hawezi kujizuia ila kujilinganisha mara kwa mara na Dada Xia, na anapokosa kumpiku Dada Xia, anakuwa hasi, anafadhaika, na kukosa furaha. Kupitia kuhukumiwa na kufunuliwa na maneno ya Mungu, baadaye anakuja kugundua kuwa ufuatiliaji wake wa umaarufu, faida ya kibinafsi na hadhi ni makosa. Anaona wazi kuwa umaarufu na faida ya kibinafsi ni vifaa ambavyo Shetani hutumia kumpotosha na kumfunga mwanadamu, kwamba kufuatilia vitu hivi kumemfanya awe mwenye akili finyu, mbinafsi, na mwenye kustahili dharau, na kwamba anaishi bila mfano wowote wa binadamu. Anaanza kujichukia, kisha anatubu kwa Mungu, anaacha hamu yake ya umaarufu, faida ya kibinafsi na hadhi, na kufanya wajibu wake kwa njia ya unyenyekevu. Kisha anakuja kuhisi mwenye uhuru na mtulivu, na anagundua kweli kwamba hukumu na kuadibu kwa Mungu ni wokovu Wake kwa binadamu.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp