Christian Dance | Uhai wa Viumbe Vyote Hutoka kwa Mungu | Sauti za Sifa 2026
14/01/2026
1
Uzima ambao mwanadamu amepewa na Mungu hauna mwisho, hauzuiliwi na mwili, wakati, au nafasi. Hivyo ndivyo lilivyo fumbo la maisha aliyopewa mwanadamu na Mungu, na ni thibitisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake. Ingawa watu wengi huenda wasiamini kwamba uzima wa mwanadamu ulitoka kwa Mungu, mwanadamu bila kuepuka anafurahia yote yatokayo kwa Mungu, iwe anaamini au anakana uwepo Wake. Ikiwa siku moja, Mungu atabadili nia Yake ghafla, na kutaka kurudisha kila kitu kilichoko ulimwenguni na kuuchukua tena uzima Alioutoa, basi vyote havitaendelea kuwepo.
2
Mungu anatumia uzima Wake kukimu vitu vyote, vyenye uzima na visivyo na uzima, akivileta vyote katika utaratibu mzuri kwa uweza na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hauwezi kuwaziwa wala kufahamika na yeyote, na ukweli huu usioweza kueleweka ni udhihirisho halisi wa, na thibitisho la nguvu za uzima wa Mungu. Sasa hebu Nikuambie siri: Ukuu wa uzima wa Mungu na nguvu za uzima Wake hauwezi kupimika na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Hivi ndivyo ilivyo sasa, kama ilivyokuwa zamani, na ndivyo itakavyokuwa nyakati zijazo.
3
Siri ya pili Nitakayokufunulia ni hii: Chanzo cha uzima kwa viumbe vyote kinatoka kwa Mungu; bila kujali jinsi vinavyoweza kuwa tofauti katika umbo la uzima au muundo, na haijalishi wewe ni kiumbe hai wa aina gani, hakuna kiumbe anayeweza kwenda kinyume na mkondo wa uzima uliowekwa na Mungu. Kwa vyovyote vile, kile Ninachotaka ni mwanadamu aweze kuelewa hili: Bila utunzaji, ulinzi, na ugavi wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, hata ajitahidi vipi kwa bidii au kupambana kwa jitihada kubwa. Bila riziki ya uzima kutoka kwa Mungu, mwanadamu anapoteza thamani ya kuishi na maana ya maisha.
kutoka katika Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uzima wa Mwanadamu
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Aina Nyingine za Video