Wimbo wa Injili | Watu Wanapaswa Kutatuaje Kutoelewa Kwao Kuhusu Mungu? (Music Video) | Sauti za Sifa 2026

14/01/2026

1

Watu wakitaka kutatua kutoelewa kwao kumhusu Mungu, basi, lazima wapate kuzijua tabia zao wenyewe potovu, na kuchanganua na kupata kujua makosa waliyofanya, njia ya mchepuo waliyoifuata, na makosa na uzembe wao. Ni kwa njia hii tu ndiyo wataweza kuona asili yao wenyewe waziwazi na kupata maarifa juu yake. Zaidi ya hayo, lazima waone waziwazi kwa nini wanaifuata njia mbaya na kufanya mambo mengi sana ambayo yanakiuka kanuni za ukweli, na asili ya matendo haya ni nini. Zaidi ya hayo, lazima waelewe hasa nia na matakwa ya Mungu kwao yapi, kwa nini kila mara hawawezi kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, na kwa nini kila mara wanakwenda kinyume na nia Zake na kufanya kile wanachopenda.

2

Kwa kuwa una makosa haya, lazima uwe wazi moyoni mwako kuhusu ni mtazamo upi unaopaswa kuwa nao sasa, kile unachopaswa kutolea hesabu mbele za Mungu, na kile Anachotaka kuona. Lazima uyatambue mambo haya kwa kina kupitia maombi na kutafuta; kisha utajua jinsi unavyopaswa kufuatilia katika siku zijazo, na hutaathiriwa tena au kukandamizwa na makosa uliyofanya zamani. Lazima utembee katika njia iliyo mbele na utekeleze wajibu wako inavyopaswa, na usijikatie tamaa tena; lazima uibuke kabisa katika uhasi na kutoelewa.

3

Kwa upande mmoja, kutekeleza wajibu wako sasa ni kufidia makosa na uzembe wako wa zamani; huu ndio mtazamo unaopaswa kuwa nao angalau. Kwa upande mwingine, lazima ushirikiane kwa njia chanya na kwa namna ya utendaji, ufanye uwezalo kutenda vizuri wajibu unaopaswa kutenda, na kutimiza majukumu na kazi yako. Hiki ndicho kiumbe aliyeumbwa anapaswa kufanya. Haijalishi kama una mawazo yoyote kumhusu Mungu, au unafichua upotovu, au unaikosea tabia Yake, lazima utatue haya yote kwa kujitafakari na kutafuta ukweli. Lazima ujifunze kutokana na kushindwa kwako, na utoke kabisa katika kivuli cha uhasi. Mara tu unapoelewa ukweli na kuwekwa huru, bila kukandamizwa tena na mtu, tukio, au kitu chochote, basi utakuwa na imani ya kutembea katika njia iliyo mbele.

kutoka katika Neno, Vol. 3. Mihadhara ya Kristo wa Siku za Mwisho. Ni kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Mtu Anaweza Kusuluhisha Mawazo na Suitafahamu Yake Kumhusu Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp