Filamu ya Kikristo | “Wokovu” | Does Forgiveness of Sins Mean Full Salvation?

11/09/2018

Wokovu ni nini? Wale wanaoamini katika Bwana Yesu hufikiria kwamba ikiwa wataomba kwa dhati kwa Bwana, waungame dhambi zao, na kutubu, dhambi zao zitasamehewa, na watapewa wokovu, na Bwana Atakapokuja, wao watainuliwa moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni. Lakini je, wokovu kweli ni rahisi hivyo?

Shujaa katika filamu, Xu Zhiqian, ameamini katika Mungu kwa miaka mingi, akijitolea kwa shauku kwa Mungu, na kuacha kila kitu ili kutenda wajibu wake. Kwa ajili ya hili, alikamatwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti cha China. Baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, aliendelea kutekeleza wajibu wake, alipata uzoefu kidogo wa vitendo, na mahubiri yake na kazi ilitatua matatizo ya matendo kwa ndugu zake. Baadaye, mkewe pia alikamatwa, lakini hakulalamika, kuwa hasi, au kusambaratika.... Yote haya yalimshindia pongezi na sifa kutoka kwa ndugu zake. Xu Zhiqian anaamini kwamba ana uhalisi wa ukweli na kwamba hakuna tatizo kuingia katika ufalme wa mbinguni. Lakini punde tu, jaribio lisilotarajiwa lilimjia—mkewe anakufa chini ya mateso ya polisi wa CCP. Xu Zhiqian, akiwa na wasiwasi, ana dhana, kutoelewana, na malalamishi kuhusu Mungu, vilevile mawazo ya maasi dhidi ya na usaliti kwa Mungu.... Baadaye, wakati anapogundua anamsaliti Mungu, anaanza kutafakari, na kustaajabu kama watu ambao, kama yeye, hupitia majaribio na kisha kulalamika, hukosa kumwelewa Mungu, na humsaliti Mungu hakika huokolewa. Je, wao kweli wanastahili kuingia katika ufalme wa Mungu?

Baadhi ya taarifa katika video hii zinatoka kwa: Vidsplay.com

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp