Wimbo wa Kusifu | Wimbo wa Upendo Mtamu (Music Video)

09/01/2020

Upendo Wako umefichwa moyoni mwangu,

unaniongoza kuwa karibu na Wewe kwa upendo.

Kwa kuufikiria moyo Wako moyo wangu unakuwa mtamu zaidi,

nakutumikia kwa moyo na akili zangu zote.

Maneno Yako yanauongoza moyo wangu,

na hatua zangu za upendo zinakufuata kwa karibu.

Nitatenda kulingana na mapenzi Yako,

kukuridhisha kunaufurahisha moyo wangu.

Sasa naishi katika ulimwengu mwingine,

Wewe na mimi tu pamoja.

Hakuna wasiwasi, hakuna kumbukumbu ya uchungu.

Maneno Yako yatakasa upotovu wangu,

na yameujaza moyo wangu.

Nakupenda, ee, nakupenda,

Maneno Yako yamekuwa maisha yangu.

Nina bahati sana kukamilishwa na Wewe

na nitakupenda na kukushuhudia Wewe milele.

Haleluya! Haleluya!

Haleluya! Sifa ziwe kwa Mungu!

Kwa upendo tunakwenda pamoja pasiwe na chochote cha kututenganisha,

mioyo yetu yote ina furaha.

Naelewa mapenzi Yako na kukutii kabisa,

sitaki kamwe tena kuasi hata kidogo.

Nitaishi mbele Yako hata zaidi, nami sitatenganishwa nawe kamwe.

Natafakari kwa kimya juu ya maneno Yako,

nathamini kile Ulicho nacho na ulicho.

Maneno Yako yatakasa upotovu wangu,

na yameujaza moyo wangu.

Nakupenda, ee, nakupenda,

Maneno Yako yamekuwa maisha yangu.

Nina bahati sana kukamilishwa na Wewe

na nitakupenda na kukushuhudia Wewe milele.

Haleluya! Haleluya!

Haleluya! Sifa ziwe kwa Mungu!

Haleluya! Haleluya!

Haleluya! Sifa ziwe kwa Mungu!

Umetoholewa kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp