Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kupata Mwili | Dondoo 101

17/07/2020

Kabla Yesu Hajatekeleza kazi yake, Aliishi tu katika ubinadamu Wake wa kawaida. Hakuna mtu ambaye angeweza kutambua kuwa Alikuwa Mungu, hakuna aliyegundua kuwa Alikuwa Mungu mwenye mwili; watu walimjua tu kama mwanadamu wa kawaida kabisa. Ubinadamu Wake wa kawaida ulikuwa uthibitisho kuwa Mungu Alipata mwili, na kwamba Enzi ya Neema ilikuwa enzi ya kazi ya Mungu mwenye mwili, si enzi ya kazi ya Roho. Ilikuwa uthibitisho kuwa Roho wa Mungu Alipatikana kikamilifu katika mwili, kwamba katika enzi ya kupata mwili kwa Mungu mwili Wake ungetekeleza kazi yote ya Roho. Kristo mwenye ubinadamu wa kawaida ni mwili ambao kwao Roho Hupatikana, Akiwa na ubinadamu wa kawaida, ufahamu wa kawaida, na fikira za wanadamu. “Kupatikana” kunamaanisha Mungu kuwa mwanadamu, Roho kuwa mwili; kuiweka wazi, ni wakati ambapo Mungu Mwenyewe Anaishi katika mwili wenye ubinadamu wa kawaida, na kupitia kwenye huo mwili, Anaonyesha kazi yake ya uungu—hii ndiyo maana ya kupatikana, au kupata mwili. Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu. Kwa sababu ilikuwa ni Enzi ya Neema, ilikuwa muhimu Kwake kuponya wagonjwa, na kwa njia hiyo Alionyesha ishara na miujiza, mambo ambayo yalikuwa kiwakilishi cha neema katika hiyo enzi; kwani Enzi ya Neema ilikitwa katika kutolewa kwa neema, ikiashiriwa na amani, furaha, na baraka ya vitu, vyote vikiwa zawadi za imani ya watu kwa Yesu. Hii ni kusema kuwa, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kutoa neema ulikuwa uwezo asilia wa mwili wa Yesu katika Enzi ya Neema, mambo haya yalikuwa ni kazi ya Roho iliyopatikana katika mwili. Lakini Alipokuwa Akitekeleza kazi kama hiyo, Alikuwa Akiishi katika mwili, Hakuenda nje ya mipaka ya mwili. Haijalishi ni matendo gani ya uponyaji Aliyotekeleza, bado Alikuwa na ubinadamu wa kawaida, bado Aliishi maisha ya kawaida ya binadamu. Sababu inayonifanya Niseme kuwa katika enzi ya kupata mwili kwa Mungu mwili ulitekeleza kazi yote ya Roho, ni kuwa haijalishi ni kazi gani Aliyoifanya, Aliifanya katika mwili. Lakini kwa sababu ya kazi Yake, watu hawakuchulia mwili Wake kuwa ulikuwa na kiini cha kimwili, kwani huu mwili ungefanya maajabu, na baadhi ya nyakati maalum ungefanya mambo ambayo yalivuka uwezo wa kimwili. Kwa hakika, haya matukio yote yalitokea Alipoanza huduma Yake, kama vile Yeye kujaribiwa kwa siku arobaini au kubadilishwa kule mlimani. Hivyo kwa Yesu, maana ya kupata mwili kwa Mungu haikukamilishwa, ila tu sehemu yake ilitimizwa. Maisha Aliyoishi katika mwili kabla ya kuanza kazi Yake yalikuwa ya kawaida tu katika hali zote. Alipoanza kazi Alidumisha gandaumbo la nje la mwili Wake tu. Kwa sababu kazi Yake ilikuwa onyesho la uungu Wake, ilipita kazi ya kawaida ya mwili. Hata hivyo, Mwili wa Mungu ulikuwa tofauti na wanadamu wenye nyama na damu. Kwa hakika, katika maisha Yake ya kila siku, Alihitaji chakula, nguo, usingizi, na makao kama mtu yeyote yule, Alikuwa na mahitaji ya lazima ya kawaida, Alifikiri na kuwaza kama mwanadamu wa kawaida. Bado watu walimchukulia kuwa mwanadamu wa kawaida, isipokuwa tu kwamba kazi Aliyoifanya ilikuwa ya ubinadamu usio wa kawaida. Kwa hakika, haijalishi Alifanya nini, Aliishi katika ubinadamu wa kawaida, na hata Alipotekeleza kazi, fikira zake zilikuwa za kawaida, mawazo yake yalikuwa ya wazi, hata zaidi ya wanadamu wa kawaida. Ilikuwa muhimu kwa Mungu mwenye mwili kufikiri kwa njia hii, kwani kazi ya uungu ilipaswa ionyeshwe na mwili ambao fikira zake zilikuwa za kawaida sana na mawazo yake wazi kabisa—ni kwa njia hii tu ndiyo mwili Wake ungeweza kuonyesha kazi ya uungu. Wakati wote wa miaka yote thelathini na tatu na nusu ambayo Yesu Aliishi duniani, Alidumisha ubinadamu Wake wa Kawaida, ila kwa sababu ya kazi Yake katika huduma Yake ya miaka mitatu na nusu, watu walidhani kuwa Alikuwa Amepita mipaka ya ubinadamu, kwamba Alikuwa wa rohoni zaidi kuliko hapo awali. Kwa kweli, ubinadamu wa kawaida wa Yesu haukubadilika kabla na baada ya Yeye kuanza huduma Yake; ubinadamu Wake ulikuwa sawa wakati wote, lakini kwa sababu ya tofauti kabla na baada ya Yeye kuanza huduma Yake, mitazamo miwili ilijitokeza kuhusiana na mwili Wake. Haijalishi watu walifikiria nini, Mungu mwenye mwili Alidumisha ubinadamu Wake asilia wa kawaida kipindi chote, kwani kwa sababu Mungu Alikuwa mwili, Aliishi katika mwili, mwili uliokuwa na ubinadamu wa kawaida. Hata ikiwa Alikuwa Anatekeleza huduma Yake au la, ubinadamu Wake wa kawaida usingeweza kufutika, kwani ubinadamu ndio kiini cha msingi cha mwili. Kabla Yesu hajaanza kutekeleza huduma Yake, mwili Wake ulibaki wa kawaida kabisa, ukishiriki katika shughuli zote za binadamu; Hakuonekana hata kidogo kuwa wa rohoni, Hakuonyesha ishara zozote za kimiujiza. Wakati ule Alikuwa tu mwanadamu wa kawaida sana Aliyemwabudu Mungu, japo dhamira Yake ilikuwa adilifu sana, ya kweli zaidi kuliko ya mtu yeyote. Hivi ndivyo ubinadamu Wake wa kawaida ulijionyesha wenyewe. Kwa kuwa Hakufanya kazi kabisa kabla ya kuianza huduma Yake, hakuna aliyemtambua, hakuna aliyegundua kuwa mwili Wake ulikuwa tofauti kabisa na miili ya watu wengine, kwa kuwa Hakutenda muujiza hata mmoja, Hakutenda hata chembe ya Kazi ya Mungu. Hata hivyo, baada ya kuanza kutekeleza kazi Yake, Alidumisha umbo la nje la ubinadamu wa kawaida na kuendelea kuishi katika mawazo ya kawaida ya binadamu, lakini kwa kuwa Alikuwa Ameanza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe, kuanzisha huduma ya Kristo na kufanya kazi ambayo wanadamu hai, wanadamu wenye nyama na damu, wasingeweza kufanya, basi watu walidhani kuwa Hakuwa na ubinadamu wa kawaida na Hakuwa mwili wa kawaida kikamilifu ila mwili usio kamili. Kwa sababu ya yale Aliyotekeleza, watu walisema kuwa Alikuwa Mungu katika mwili Ambaye Hakuwa na ubinadamu wa kawaida. Huu ulikuwa ufahamu wa kimakosa, kwani watu hawakuelewa maana ya Mungu kupata mwili. Huu ufahamu mbaya ulitokana na ukweli kuwa kazi iliyoonyeshwa na Mungu katika mwili ilikuwa kazi ya uungu, iliyoonyeshwa kupitia kwa mwili wenye ubinadamu wa kawaida. Mungu Alikuwa Amevishwa katika mwili, Alikaa ndani ya mwili, na kazi Yake katika ubinadamu Wake iliuziba ukawaida wa ubinadamu Wake. Kwa sababu hii, watu walidhani kuwa Mungu Hakuwa na ubinadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp