Filamu za Kikristo "Chama Hakijamaliza Kuzungumza" | Concrete Proof of the CCP Persecuting Christians

10/08/2018

Li Ming’ai ni Mkristo nchini China Bara. Yeye ni mwanamke mwadilifu ambaye anawaheshimu wakweze, humsaidia mumewe na kumuelimisha mtoto wake, na ana familia ya furaha na patanifu. Katika China, ambako ukanaji Mungu unatawala, hata hivyo, serikali ya Kikomunisti ya China daima huwakamata na kuwatesa ovyo ovyo watu wanaomwamini Mungu. Katika mwaka wa 2006, Li Ming'ai alikamatwa na kutozwa faini kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Baada ya Li Ming'ai kurudi nyumbani, polisi wa Kikomunisti wa China daima walimtisha na kumwogofya yeye na familia yake, na walijaribu kumzuia Li Ming'ai kuendeleza imani yake kwa Mungu. Siku moja, Li Ming'ai alipokuwa mbali na nyumbani akifanya mkutano, aliripotiwa na mtoa habari. Polisi walikwenda nyumbani kwa Li Ming'ai wakijaribu kumkamata. Alilazimika kuondoka nyumbani, na tangu wakati huo kwendelea, maisha ya Li Ming'ai ya kujificha kutoka mahali pamoja hadi pengine na kukimbia kutoka nyumbani yalianza. Polisi wa Kikomunisti wa China bado hawakuachana naye, daima wakiichunga nyumbani yake, na kusubiri fursa ya kumkamata. Jioni moja, Li Min’gai ananyemelea nyumbani kwa familia yake, lakini karibu mara moja polisi wanaharakisha kumkamata. Kwa bahati nzuri mtu fulani anamwonya, na Li Ming'ai anaepuka maafa.

Miaka mitatu baadaye, wakati Li Ming'ai anaendeleza imani yake na kufanya kazi yake mbali na nyumbani, anafuatwa na kukamatwa na polisi wa Kikomunisti wa China. Polisi wa Kikomunisti wa China wanatekeleza mateso na maudhi ya kikatili kwa Li Ming'ai , na kutumia upendo wa familia kujaribu kumshawishi. Wanatumia vitisho kama vile kumnyima mtoto wake haki ya kuhudhuria shule, na kuzuia upatikanaji wa kazi baadaye katika serikali ili mtoto aweze kujaribu kumlazimisha kuiacha imani yake kwa Mungu, kuwasaliti viongozi katika kanisa, na kutangaza fedha za kanisa. Wakati huu, Li Mingai anamwomba Mungu na kuweka imani yake kwa Mungu. Katika neno la Mungu anapata nuru na mwongozo. Anavumilia mateso na maudhi na polisi wa Kikomunisti wa China, anazitambua mbinu za Shetani, na kuamua kutomsaliti Mungu. Anakuwa shahidi kwa udhabiti kwa Mungu. Masaili ya Polisi wa Kikomunisti wa China hayazai matunda, na wao wanakasirika kwa aibu. Wanamwongoza Li Mingai akiwa amevaa nguo za mfungwa kwa nyumba yake ya kijijini, wakimtembeza ili wote wamuone. Wanafanya hivi ili kumdhalilisha, na kisha kujaribu kuwafanya jamaa zake wamshawishi kumsaliti Mungu, na kulisaliti kanisa. Li Ming’ai anaghadhibishwa sana na jinsi Wakomunisti wa China wanavyoona kuwa matatizo ya familia yake ni kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Akiwa amejaa hasira ya kudhulumiwa, Li Ming'ai kwa ghadhabu anafichua ukweli wa uovu wa jinsi serikali ya Kikomunisti ya China huwakamata na kuwatesa Wakristo. Anasema kuwa mwangamizi halisi wa familia za Wakristo ni serikali ya Kikomunisti ya China, ambayo ndiyo mhalifu mkuu wa jinai ambaye huwaletea watu kila aina za majanga. Kwa hiyo anawapa ushinde kikamilifu na kwa aibu Wakomunisti wa China.

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp